Una ushahidi wa yanayojiri Kenya?
January 10, 2008 at 3:04 pm 1 comment
Ni hulka ya binadamu, kujifunza kupitia makosa. na hili ndilo linalojitokeza nchi jirani na hapa kwetu TZ.
Wakati ambapo hakuna mtu ambaye alidhania kuwa yanayojiri nchini Kenya hivi sasa yangetokea, na wakati kila mtu akiwa anasikitika kutokana na hayo yanayoendelea huko, kwa upande wa pili, wanablogu wa nchini humo wameonyesha mchango wao mkubwa sana katika kuona hali inabadilika.
Jitihada za mwanzo kabisa zilikuwa zile za kuhakikisha kuwa dunia inatambua kilicho, kinacho na hata kitakachotokea nchini mwao, kwa kutusambazia habari na matukio mbalimbali kwa kadiri walivyoweza. jitihada ya karibuni kabisa imekuwa ni kuanzishwa kwa zana inayoitwa Ushahidi.
Kwa sasa pengine sitokuwa na mengi sana kuihusu zana hii, maana nami niliipitia juu juu tu baada ya kupata taarifa hizi kupitia kwa kaka yangu Ndesanjo wa Jikomboe. ambaye naye aliipata kupitia kwa Mwafrika Mweupe….nitawaomba tu muitembelee na muone mambo yanayoendelea huko.
Na wakati mkifanya hivyo, ni vyema tukakumbushana umuhimu wa kuungana na kuzidi kuiombea heri nchi ya Kenya.
Entry filed under: maskani.
1. Ushahidi Updates - SMS, Red Cross, Flickr, etc... | White African | January 11, 2008 at 12:34 am
[…] bloggers: Una ushahidi wa yanayojiri Kenya? Ushahidi + Ukurasa Maalum Wa Kenya + Action Alerts […]