Archive for January 10, 2008

KENYA: Mabadiliko hayabadiliki..

Mazungumzo ya kusaka muafaka baina ya pande zinazosababisha umwagaji damu nchini Kenya yamevunjika. Soma hapa au hapa kujua ilikuwaje.

 Nimekuwa nikifuatilia mambo yanayoendelea kwa jirani zangu hawa, kupitia njia mbalimbali zikiwemo za mawasiliano na vyombo vya habari. Katika kipindi hiki kigumu sana, miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana ni jamaa zangu waandikao mtandaoni ama Bloggers.

Mwana blogi Thinkersroom, ameandika makala kadhaa zenye kunivutia kuzisoma na bilashaka nawe msomaji wangu ungependa kuziona habari hizo. Bonyeza hapa kusikia kile anachosema huyu jamaa. na pia bonyeza hapa kusoma kile anachosema bloga mwingine, Kenyananalyst.  

 Lakini wakati hayo yanaendelea, rafiki yangu mmoja ambaye nitamtaja jina baadae kama akiniruhusu anasema mabadiliko ni lazima nchini Kenya… kwa maneno yake anasema kuwa Mabadiliko hayabadiliki

January 10, 2008 at 7:45 pm 1 comment

Una ushahidi wa yanayojiri Kenya?

Ni hulka ya binadamu, kujifunza kupitia makosa. na hili ndilo linalojitokeza nchi jirani na hapa kwetu TZ.

Wakati ambapo hakuna mtu ambaye alidhania kuwa yanayojiri nchini Kenya hivi sasa yangetokea, na wakati kila mtu akiwa anasikitika kutokana na hayo yanayoendelea huko, kwa upande wa pili, wanablogu wa nchini humo wameonyesha mchango wao mkubwa sana katika kuona hali inabadilika.

 Jitihada za mwanzo kabisa zilikuwa zile za kuhakikisha kuwa dunia inatambua kilicho, kinacho na hata kitakachotokea nchini mwao, kwa kutusambazia habari na matukio mbalimbali kwa kadiri walivyoweza. jitihada ya karibuni kabisa imekuwa ni kuanzishwa kwa zana inayoitwa Ushahidi.

Kwa sasa pengine sitokuwa na mengi sana kuihusu zana hii, maana nami niliipitia juu juu tu baada ya kupata taarifa hizi kupitia kwa kaka yangu Ndesanjo wa Jikomboe. ambaye naye aliipata kupitia kwa Mwafrika Mweupe….nitawaomba tu muitembelee na muone mambo yanayoendelea huko.

Na wakati mkifanya hivyo, ni vyema tukakumbushana umuhimu wa kuungana na kuzidi kuiombea heri nchi ya Kenya.

January 10, 2008 at 3:04 pm 1 comment


Blog Stats

  • 34,787 hits
January 2008
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031