Hawa wamepona, wangapi wamekufa?

November 6, 2007 at 12:01 pm 3 comments

muhimbiliNi habari ambayo ilinisikitisha sana kama si kunistua sana kwakweli. Mgonjwa wa kichwa anapasuliwa mguuni na yule wa mguu anapasuliwa kichwani. Sijui nishangae au nijiulize au.

Ikiwa hukukutana na habari hiyo ambayo ilitoka katika gazeti la Mwananchi la siku ya Jumatatu ya Novemba 5, basi bofya hapa uisome habari hiyo kikamilifu na kisha bofya hapa kujua kilichofuatia baada ya habari ile.

Uzembe huu katika Taasisi ya mifupa ya Muhimbili, ni wa aina yake kwakweli, na kwakuwa inaelezwa kuwa yanatokea mambo haya mara kwa mara, tunajiuliza ni wangapi wamepoteza maisha kutokana na uzembe huu?

Entry filed under: maskani.

Tangulia Dube, duniani hapakukustahili!! Waraka wa Butiku kwa Mkapa huu hapa

3 Comments Add your own

 • 1. msangi  |  November 6, 2007 at 12:08 pm

  Na unajua kuwa Profesa Maseru ambaye ni mkuu wa kitengo hicho alipoulizwa alisema nini kuhusu tukio hilo?

  “Ni kweli kuna tukio la aina hiyo hapa hospitalini, lakini kuna taratibu nimeanza kuzichukuwa na sasa hivi ninapozungumza nawe nipo kwenye kikao cha kuunda tume ya kufuatilia na siwezi kukiri au kukataa kuwa ni uzembe, ndiyo maana tunaunda tume ya kuchunguza suala hilo na pia nimeishapeleka taarifa wizarani”

 • 2. AUGUSTUS FUNGO  |  November 8, 2007 at 3:05 am

  Mwanangu inatisha tutakimbilia wapi kama watu tunaowategemea kama hao wanafanya uzembe mkubwa namna hiyo?yaani nafikiria nashindwa hata cha kuwafanya kwa kweli,yaani sijui ni maruhani au jamani watu masikini wanatoka mbali wakitegemea huduma bora kumbe wanafuata mauti.nakubaliana na wewe msangi hao ni wale walio lia tukawasikia je,wale ambao hawakuwa na pakusemea ni wangapi?jamani hospitali hizi zimulikwe,kwakweli ni aibu kwa tanzania na dunia nzima.hatua zichukuliwe kunusuru maisha ya watanzania.Bbc wameifanyia coverage nzuri sana..Namsikitikia aliyepasuliwa kichwa. msangi ee hebu tuwaulize unaanzaje kupasua kichwa wakati hamna tatizo lolote hata wewe hushangai?bila kuangalia cheti kinasemaje?jamani mnatiua.
  Mungu awajalia afya njema majeruhi

 • 3. Jeff Msangi  |  November 8, 2007 at 6:54 pm

  Rama,
  Hii habari bado inanipa bumbuazi la akili na pia moyo.Nashindwa kuamini lakini sina budi kufanya hivyo ili niweze kuiona kesho.Cha kusikitisha ni kwamba hapatokuwa na compesation ya aina yoyote na wala hatua kali hazitochukuliwa.Watacheza na ile kanuni yao..muda ndio dawa,baada ya muda watasahau…tutapelekwa hivi hadi lini?Maana huu ni uzembe na sio makosa ya kibinadamu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,061 hits
November 2007
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930