Athman Idd ‘Chuji’; Laana ya Simba au?

October 12, 2007 at 9:41 pm 4 comments

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Idd, almaarufu kwa jina la Chuji, ambaye alizua tafrani ya aina yake mwanzoni mwa mwaka huu wa 2007, wakati wa usajili baada ya kuvigonganisha vilabu viwili vya Simba na Yanga, bado anaendelea kukumbwa na balaa linalohatarisha uhai wa kipaji chake cha uchezaji soka.

 Mchezaji huyo ambaye alichipukia katika klabu ya Polisi Dodoma, ambaye baada ya sakata lake kuamuliwa na shirikisho la soka la Tanzania (TFF), hivi sasa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kutaka kumshushia kipigo mwamuzi wakati klabu yake ya Yanga ilipopambana na Coastal Union ya Tanga.

 Ikumbukwe kuwa, toka mchezaji huyo atoke klabu ya Simba na kuhamia kwa watani wao Yanga, hajawahi kufanya jambo lolote la maana kwasababu kipindi hicho chote amekuwa akikumbwa na mikasa ya hapa na pale, mingine ya kujitakia na mingine yenye kuzua uyaya.

Katika moja ya mechi chache sana alizoweza kuichezea Yanga, Athuman Idd, alijikuta matatizoni baada ya kuwanyooshea kidole cha kati mashabiki waliokuwa wakimzomea katika uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Hiyo ilikuwa ni siku chache sana baada ya TFF, kuingilia kati na kuuvunja mkataba baina yake na Simba, na hivyo kumuidhinisha kwenda Yanga, baada ya mvutano wa muda mrefu uliomkosesha mechi nyingi kiasi cha kutemwa katika tumi ya Taifa (Taifa Stars).

Ilionekana kama vile kiungo huyo mkabaji na mwenye mapafu yenye kujitosheleza, angerejea katika timu yake kutokana na kile kilichoonekana kutulia kwake, na washabiki kudhania kuwa amekua na amejua nini maana ya kuwa mchezaji maarufu, lakini kumbe haikuwa hivyo.

Siku tatu tu baada ya taarifa za TFF kusomeka magazetini kuwa ametulia, kiungo huyo kumbe alikuwa na yake mambo, na akajikuta tena akiingia katika tuhuma za kumpiga mwamuzi na sasa atakaa tena nje ya uwanja kwa miezi mitatu.

Swali ni kuwa, hivi huyu kijana ana matatizo gani? Ni laana ya kuondoka Simba na kuhamia Yanga inayomtafuna (maana huwa wanasema vilabu hivi ukitoka kimoja kwenda kingine ndio umekwisha), au ni nini hasa kinamkumba?

Entry filed under: maskani.

Tangazo…tangazo…tangazo Mtukufu Mwalimu, wanafunzi wako wamekuwa watukutu

4 Comments Add your own

 • 1. lucille  |  July 23, 2010 at 3:19 pm

  please try to put the profiles of our players in the web so that we it will make it much easier for exposing them.

 • 2. lucille  |  July 23, 2010 at 3:20 pm

  chuji kifaa cha ukweli nalikubali sana soka lako uko juuuuuuuuuuu kupita maelezo kaka.

 • 3. salum jumanne  |  November 10, 2010 at 8:37 am

  Chuji ni bonge la mildfielder, sema ndo hivyo tena bangi nyingi kwa sana. Ila point ya msingi ni kwamba, akiacha kujisikia atakuwa bonge la proffessional player in the world,NI HAYO 2.

 • 4. salum jumanne  |  November 10, 2010 at 3:06 pm

  Sio laana wala nini, bali ndo hivyo tena bado hajatulia, na kimsing kama nlivyosema hapo kabla kuwa akiacha mambo yake ya bangi, mambo yatakuwa poa sana kwa upande wake. But he is the heavy weight player and no body can judge it.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
October 2007
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031