Archive for September, 2007

Tangazo…tangazo…tangazo

Asubuhi hii nimepokea ujumbe huu toka kwa babkadja sankofa. Tafadhali usome kwa makini na uufanyie kazi.

Naomba ubonyeze hapa  AU www.zafaa.com halafu bonyeza link ya NOMINATE HERE. Ukifunguka huo ukurasa naomba uende kwenye category ya BEST DOCUMENTARY FEATURE, pale kuna filamu tatu, ya kwetu (ya Watanzania) ni PLAY YOUR PART – TANZANIA. Naomba uipigie kura ili ishinde tuzo za African Academy Awards. Naomba uwaambie na watu wengine wengi, ikiwezekana weka tangazo kwenye blogu yako kama unayo. SAMBAZA HABARI HII KABLA GIZA HALIJAINGIA.

Filamu ya PLAY YOUR PART inapambana na Filamu kutoka Zambia na moja kutoka Uganda. Hadi sasa PLAY YOUR PART inaongoza kwa kura. Tafadhali ongeza idadi ya kura zile ili kilio cha wakina mama na watoto wanaopoteza
maisha kwa sababu ya afya mbaya ya uzazi kisikike zaidi. PIGA KURA kwa PLAY YOUR PART

Asante sana.

To the English Speaking Friends:

Please visit www.zafaa.com or click here and on the category “BEST DOCUMENTARY FEATURE” vote for the film “PLAY YOUR PART” from Tanzania. Your vote will add to the voice of the mothers and children who are fighting for the better maternal health.

September 30, 2007 at 10:46 am Leave a comment

Nani kaiona ndege ya JK ikipaa?

http://sidymic.blogspot.com/Mwanablogu Reginald Simon Miruko aka Dogo wa Blogu ya KISIMA CHA FIKRA, siku hizi amekuwa mvivu kidogo katika kutuletea mambo mapya, lakini pale anapopata nafasi huibuka na tafakuri za kufa mtu. Kama huamini,  itakubidi usikie swali alilouliza kuhusu ndege ya uchumi ya JK. Nimenukuu ujumbe wake hapa chini:-

“Baada ya kushika madaraka ya juu kabisa nchini, Rais JK alisema ndege ya uchumi ya aliyokuwa ameiwasha Mtangulizi wake, Mkapa, ameikuta kwenye runway ikitaka kuruka. Alifafanua zaidi kuwa kazi yake kubwa itakuwa ni kuirusha ili Tanzania ipae.
Yeye hajatamka lolote hadi sasa, lakini ‘mbia wake’ Ed ameshatamka kuwa ndege hiyo imeshapaa muda mrefu. Mimi sijaiona, ila nadhani imerudi kuegeshwa au haikuwa na mafuta. Wewe je, umeiona?
Mwanakijiji mmoja naye amesema hajaiona, lakini ofisi ya Ed imejibu kwa besi kuwa ndege hiyo imesharuka muda mrefu…kalagabao wasioiona labda wana dhambi au hawatumii rada ya mtumba iliyonunuliwa kwa bei mbaya”

Katika kulipa hilo msisitizo, ‘Bloga’, mwingine ambaye ni msanii wa uchoraji, Said Michael, naye alipandisha katuni mnayoiona katika makala hii, kuhusu ndege ya uchumi ya JK.

Jamani nyie mmeiona ikipaa hiyo ndege? labda nami niulize, maana hata mie sijaiona!!

September 29, 2007 at 1:57 pm 1 comment

Kwa haya ya Buzwagi, Tanzania tunaelekea Ukombozi wa kifikra

Yalianza kama utani na wenye nguvu zao bilashaka walidhania ulikuwa ni moto wa kifuu, lakini kumbe haikuwa hivyo. Huu wa sasa kama twaweza kuuita moto basi ni wa nyikani na ambao unawaka katika nyika yenye nyasi kavu.

Nazungumzia hili sakata la Mkataba wa Buzwagi, ambalo lilianzishwa kule mjini Dodoma, wakati wa kikao cha bajeti cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. na ambalo kwa siku za hivi karibuni limekuwa kinara wa mambo ambayo yanalitikisa Taifa la Tanzania.

Pengine si busara sana kuuzungumzia kwa kina mkataba huo kwasababu naamini wengi wetu tumeshasikiliza masimulizi ya kila aina kuuhusu na wengine tumefanikiwa kuuona kabisa na kuupitia mstari hadi mstari, kifungu hadi kifungu. Kwa wale ambao watakuwa hawajabahatika kuusoma au kusikia lolote kuuhusu wanaweza kupata fursa hiyo kwa kubonyeza hapa.

Mkataba huu ambao uliibuliwa rasmi Bungeni na Bw. Zitto Kabwe, umeibua mambo mengine mengi huku mara leo ukisikia limeibuka hili, kesho limeibuka lile na ni wazi kuwa kwa mwenendo huu yapo mengi ambayo yataibuka kutokana na Mkataba wa Buzwagi

Vuguvugu kuhusiana na Mkataba huu limekuwa likisambaa nchini kama vile moto unavyosambaa katika sehemu iliyomwagwa petroli, na bila shaka hili ndilo msingi wa makala yangu ya leo. Tunajifunza nini kutokana na sakata la Mkataba huu?

 Kwa zaidi ya miaka 40 toka Tanzania kupata uhuru wake uliokuwa mikononi mwa wakoloni wa Kiingereza, nchi hii imekuwa ikitajwa kuwa moja ya nchi zilizo masikini sana duniani. Hili limekuwa likijitokeza licha ya uongo (sababu umekuwa hauendani na taarifa za wachunguzi) ambao tumekuwa tukishurutishwa kuukubali toka kwa viongozi wetu kuwa nchi inaendelea kukua kiuchumi.

Kwa muda wote huo, wimbo wa wale tunaowapa jukumu la kututawala, umekuwa ni ule ule wa mipango mingi ya kiuchumi na hasa ile ya kuwakwamua wananchi kutoka katika lindi la umasikini inashindwa kutekelezeka kutokana na uhaba wa bajeti. Bajeti hiyo hiyo ambayo kila mwaka imekuwa ikisomwa inaambatana na vibwagizo vya kukua kwa uchumi.

Mwananchi wa kawaida kabisa nchini Tanzania, ameendelea kuwa masikini wa kutupwa kila uchao huku akiwa katika ardhi ambayo imejaaliwa madini ya kila aina. Ardhi ambayo imejaaliwa rutuba ya kila namna.

Haya yamekuwa yakiendelea kutokea wakati mwananchi huyo huyo akishuhudia jinsi ambavyo daraja baina ya yeye mwenye kukabiliana na machungu ya umasikini huo na yule ambaye amekuwa akimtetea kuwa hana njaa, likiendelea kukua kila uchao.

Ni katika mazingira haya haya ambapo mwananchi huyo huyo mwenye kuishi katika kiwango cha chini ya shilingi 100 kwa siku, amekuwa akishuhudia pia wale anaowategemea wamtetee jinsi ambavyo wanazidi kumtoa kabali za kimaisha badala ya kile alichowachagulia.

Yapo mengi sana ambayo yamekuwa yakitokea na ambayo mara jkadhaa yamekuwa yakinifanya nifikirie Busara, Uwezo na Utashi walionao hawa tunaowaita viongozi wetu. Viongozi wetu wengi wangekuwa waliosoma sana huenda ningeamini kuwa kusoma sana kuna matatizo tena makubwa sana, lakini laa, wengi wao ni wa elimu ya kawaida tu mbona.

Tunaweza kujadili mengi sana hapa, mengi yasiyo na ukomo sababu wanayotutendea ni mengi sana, lakini jambo moja tu ambalo ningependa sana walifahamu, kulijua na kuliweka akilini mwao ni kuwa kuna kitu huitwa ishara za nyakati.

jambo pekee ambalo ningependa kuwafahamisha viongozi wangu hawa ambao nawapenda sana ni kuwa haya yanayoendelea kujiri hivi sasa kuhusiana na mkataba wa Buzwagi,  hayaji kwasababu ya upumbavu wa Watanzania. Yanakuja kwasababu Watanzania tumechoshwa na hali hii.

Ikiwa hamtaweza kusoma ishara za nyakati, ikiwa hamtakuwa tayari kukiri kuwa kama ni kula mmekula na sasa mmevimbiwa matumbo, ikiwa hamtataka kuwa wakweli na kutambua kuwa Watanzania sio wapumbavu kwa kiwango mnachodhania, hakika ipo siku mtajuta na kujutia matendo yenu. Mtajutia kuziba masikio yenu.

….itaendelea…

September 25, 2007 at 6:16 pm Leave a comment

Jamani nimeshindwa mnisamehe

Wakati natoa tangazo la kuhamisha kijiwe hiki toka kule blogspot, nilitangaza pia kuwa nimeanzisha kijiwe cha picha kupitia hukuhuku wordpress. naomba niseme kuwa nimechemka kupandisha picha katika wordpress.

Kutokana na hali hiyo basi, kijiwe cha picha mbalimbali nitakazokuwa nazipata huko mitaani ninakokatiza zitakuwa zikipatikana kupitia http://www.nilichokiona.blogspot.com/

Tayari kuna matukio kadhaa huko ambayo si busara ukiyakosa. Unajua ilikuwaje mpiganaji Mbowe alipotembelea jiji la Mbeya? Unajua kuwa basi la Sabco limechinja tena watu 27, ikiwa ni chini ya miezi miwili toka lichinje tena watu 12 mkoani Mbeya?

Tembelea kijiwe changu cha picha uyaone haya live. Bonyeza hapa.

September 8, 2007 at 3:10 pm Leave a comment


Blog Stats

  • 35,058 hits
September 2007
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930