Msaada jamani!!

August 11, 2007 at 10:52 am 2 comments

Leo hii, asubuhi sana na mapema nilipoingia ofisini kwangu, jambo la kwanza kabisa kulifanya ilikuwa kusoma barua nilizotumiwa na wasgirika mbalimbali kama ilivyo kawaida yangu. Moja kati ya ujumbe ambao nilikutana nao ni huu hapa chini kumhusu binti aliyeko pichani, ambao nitauweka kama ambavyo niliukuta.

 

===

Ukimuona kwa sura, ni msichana mzuri mwenye macho ya kuvutia, lakini masikini hana raha ya maisha! Mtoto Sofia James Mwiga (17, pichani)mkazi wa Manispaa ya Tabora nchini Tanzania anaishi kwa mateso kufuatia ugonjwa wa ajabu wa kuvimba miguu hali iliyomfanya ajione mpweke machoni mwa jamii huku akishindwa kuanza shule.


Licha ya baba yake kumtafutia matibabu kwa zaidi ya miaka 10 bado hajafanikiwa kwani kila Daktari anayemfanyia uchunguzi hutoa maelezo kuwa hapa Tanzania hawezi kufanyiwa oparesheni isipo kuwa nje ya nchi ambako kuna Wataalam na vyombo vya kitabibu vya kisasa.

Kutokana na umasikini alionao baba mtu ameshindwa kumsaidia badala yake amebaki akisubiri miujiza ya mungu ishuke pengine atapata mfadhili atakaye weza kumsaidia kupata matibabu hivyo anawaomba wasamaria wema popote duniani waweze kumsaidia kuokoa maisha ya mtoto wake huyo.


Hivi sasa mtoto huyu yupo katika hospitali ya Lugalo, jijini Dar es salaam akisubiri atakayeweza kujitokeza na kumsadia kupata matibabu sahihi nje ya nchi, kwa mujibu wa mdaktari, anahitaji operation ya kuondoa nyama hizo zilizozidi.

cheki anavyoumia

Mungu kama amekupa, basi kumbuka na wenye shida. Naamini kunamtu hapo anaweza kubadili masiha ya msichana huyu kwa uwezo wake mola! namba ya simu ya baba mzazi wa msichana huyu ni +255 753 916690.

Akiwa na jamaa

Nilipomaliza kuusoma ujumbe huo niliwasiliana na mwenye namba hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Francis Aloyce Mwiga, ambaye ni baba wa wa binti huyo na akanieleza kuwa tatizo hilo lilimuanza mwaka 1998, lakini halikuwa kubwa sana, hadi mwaka 2005 ndipo hali ilipofumuka ghafla na hadi kufikia hali aliyo nayo binti huyo kwa sasa.

Alinipa ruhusa ya kupandisha ujumbe huu katika blogi yangu na ruhusa kwa yeyote atakayeupata kujitahidi kwa kadiri awezavyo kusambaza kwa watu wengine ili binti huyu ambaye ni dada yetu na rasilimali muhimu kwa Taifa la Tanzania, aweze kusaidiwa.

KUTOA NI MOYO JAMANI. MWENYE NACHO HAKIKA NI VYEMA AKASAIDIA WASIO NACHO. MSAADA WENU UNAHITAJIKA KUSAIDIA MAISHA YA BINTI YETU HUYU.

Entry filed under: Jamii, maskani.

Washindwe na walegee!! Msanii wa Bongo Fleva ndani ya Blogu

2 Comments Add your own

 • 1. freddy55  |  August 23, 2007 at 1:55 am

  Ramadhani,
  Pongezi sana kwa kutoa makala haya. Ingekuwa vizuri sana kama ungeweza kunitumia picha asilia niziweke katika blogu yangu kwa lugha ya Kiingereza. Maana wafadhili wengi hawasomi Kiswahili.
  Hapo hapo unaweza kutuma habari hizi katika anuani ifuatayo kwa ndugu na jamaa wa mtoto huyu wajaribu kuwaandikia hawa watu kutoka Tanzania maana ni rahisi zaidi kupata msaada ikiwa barua inatoka alipo mgonjwa na mapicha. Kampuni hii hapa chini inasaidia watoto wadogo duniani.

  FACING THE WORLD
  5a London House
  Serviced Offices
  266 Fulham Road
  London SW10 9EL
  UINGEREZA.
  Simu : (+44) 207- 352-0052

  Usisahau kunitumia picha na habari zaidi halafu nitaunganisha.

  Barua pepe yangu: kitoto2004@yahoo.co.uk

  Heko kwa kazi nzuri.

  Ndimi
  Freddy Macha

 • 2. Rama Msangi  |  August 23, 2007 at 12:55 pm

  Kaka yangu Freddy, nashukuru sana kwa ujumbe na wito wako. Nitawasiliana na mzazi wa kijana huyu kwa njia ya simu kisha nitamwelekeza cha kufanya. Naamini atawaandikia kwasababu wanahitaji sana msaada wa kumsaidia kijana huyo. Wasamaria zaidi wanakaribishwa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
August 2007
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031