KWANINI SIUPENDI MUSWADA HUO?

January 29, 2007 at 3:29 pm 3 comments

“Democracy needs more free speech, for even the speech of foolish people is valuable if it serves to guarantee the right of wise to talk”
– David Cushman Coyle –
==== xxx ====xxx ==== xxx ====

Baada ya kuuelezea kwa ufupi jinsi maudhui yake yalivyo katika makala zangu mbili zilizotangulia, (zisome kwa kubonyeza hapa na hapa, kwa wale waliozikosa), leo hii nimeona kwanza kabla sijaendelea na kuuchambua muswada wenyewe, basi niseme wazi kwanini siupendi huu muswada. na Zifuatazo ndio sababu kuu na za msingi kwangu, zinazonifanya nisiupende muswada wenyewe;-

1. Muswada unampa Waziri mamlaka ya kuchagua sura au vifungu ambavyo anataka vitumike kwa wakati fulani. Kwanini vifungu vyoter visitumike kwa pamoja?

2. Kipengele cha usiri katika muswada huu kinavunja kanuni za utawala bora kuruhusu serikali na taasisi zake kutotoa habari bila vikwazo, mfano shughuli za baraza la mawaziri na michakato ya utungaji sera.

3. Muswada huu unajumuisha sheria za kikandamizaji ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu ikiwemo sheria ya magazeti (1976) na ile ya utangazaji (1993)

4. Muswada unampa Waziri mamlaka ya kuzuia habari kwa kisingizio cha kuathiri maslahi ya umma, ulinzi na usalama wa taifa bila kuweka bayana mambo hayo.

5. Uhuru wa habari uliomo katika muswada huo hauendani na kanuni za kimataifa za uhuru wa kupata habari.

6. Muswada huu unaruhusu kuibuka kwa genge la mafisadi kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya pia.

7. Unazuia habari muhimu za maendeleo ya jamii, sanjari na zile za utawala mbovu na ulaji wa fedha za wananchi kinyume na makusudo ya wanaotozwa kodi.

8. Utaratibu unaotamkwa hapa haumsaidii, kumhakikishia na kumlinda mwananchi wa kawaida katika kupata taarifa.

9. Muswada huu haumjali mwananchi wa kawaida kama mdau na sehemu muhimu ya habari.

10. Muswada huu unaiweka rehani taaluma ya habari kwani hauwahakikishii wanahabari na hususan waandishi usalama na uhuru wa kufanya kazi zao.

11. Muswada huu unakataza kuandikwa kwa habari zozote zenye kuhusiana na biashara za kimataifa.

Entry filed under: maskani.

Uhuru wa habari au uhuru wa viongozi mafisadi? Kazi ni Kazi tu bora mkono kwenda kinywani

3 Comments Add your own

 • 1. luihamu  |  January 29, 2007 at 6:29 pm

  Kamanda hongera kwa kuweza kushambua madaa hii.Nakutakia heri na mafanikio katika kuleta mwanga kwa sisi tuliokuwa gizani.Mungu azidi kukupa hekima na busara.Jah guidance and protection.

 • 2. James  |  January 30, 2007 at 11:09 am

  He!! Ina maana tusihoji upuuzi kama wa IPTL, TTCL, na makampuni mengine ambayo yanaingia yubia na serikali yetu kwa lengo la kutuumiza? Ina maana hatutatakiwa kuhoji wala kusoma tena habari za kiuchunguzi?

  maana kwa ninavyokuelewa hapo ni kuwa kama mwandishi akitaka kuandika habari ya uchunguzi labda itakuwa ile ya akina nani wanaizodoa serikali iliyoko madarakani au?

  Unajua serikali yetu haijui kama paka ingawa ni mnyama mdogo, ukimfunga mahali halafu ukaanza kumchengesha na kumpa mateso akiamua kukugeuka shughuli yake hapo, ni afadhali upambane na simba mwituni.

  Hatuutaki na hao waandishi wenzenu wanaoupa chapuo naomba wachunguzwe na PCB, nina wasiwasi kuwa kuna rushwa ya namna fulani ndani ya hilo

 • 3. ndesanjo  |  January 30, 2007 at 8:02 pm

  Msangi,
  Muswada huu nimekuwa nausikia kijuujuu. Nimefaidika na jinsi ulivyoweka wazi vipengele vya kizandiki.

  Tangu lini serikali ikaweka mazingira ya kurahisisha na kuwezesha vyombo vya habari kuwa huru? Nani kawapa kazi hiyo ya kutuambia mwanzo na mwisho wa mipaka ya uhuru wetu wa kujieleza (ambao sio tu tumepewa na katiba bali utashi wetu kama binadamu).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
January 2007
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031