KUMRADHI……KUMRADHI……KUMRADHI

December 28, 2006 at 5:27 pm 1 comment

Wapendwa wasomaji wangu, napenda kuwaomba radhi kwa usumbufu wowote mtakaoupata katika kipindi cha siku mbili tatu pindi mtakapokuwa mkitembelea blogi hii. Kuna matengenezo ya kiufundi yenye lengo la kuboresha mambo katika kijiwe hiki ambayo yanaendelea. Matengenezo haya yatakamilika ndani ya siku mbili. Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu na nawaomba tena radhi kwa usumbufu mtakaoupata katika siku hizi mbili.

Entry filed under: maskani.

Sababu nakupenda rais wangu Tuna UHURU lakini mbona hatuko Huru

1 Comment Add your own

 • 1. Rashid Mkwinda  |  December 29, 2006 at 6:14 pm

  Duu huu ukarabati ni koboko maana naona ilikuwa renovation ya hali ya juu naona kuna parafujo nyundo na vimbwanga kibao vilivyotumika katika ukarabati huu haya basi ukarabati huu uendane na mapmbo mapya kwa mwaka 2007 na kuacha ya 2006 bali yaliyopita yawe kama kumbukizi kwa kuboresha yajayo.

  Mengi twataraji katika ukarabati huu, isiwe kama ukarabati wa SIRIKALI ya awamu ya nne katika nchi ya Wadanganyika waishio katika ardhi ya saba ilhali wengine wakiishi katika sayari yenye nuru na mwanga kuelekea matumaini ya Sayansi na Tekelinalokujia.

  Twataraji mambo mapya kwa mwaka mpya yenye lengo la changamoto za utandawazi unaotaka kuufanya uhuru wa vyombo vya habari kuhodhiwa na SIRIKALI ya awamu ya nne, eti inaandaliwa sera ya kudhibiti vyanzo vya habari…itakuwa patamu kweli utakapo hitaji kupata taarifa fulani katika sekta nyeti serikalini na kuambiwa msemaji mkuu ni Waziri ambaye kwa wakati huo aidha yuko bungeni au katika jimbo lake la uchaguzi ilhali wananchi wakihitaji taarifa zinazoihusu sekta hiyo.

  Mie nakwambia patamu kweli kweli hapo bali ukarabati huu uwiane na hali halisi ya maisha ya Mdanganyika anayeghilibiwa na kupimwa viatu mwaka huu baada ya miaka mitano anaulizwa alikuwa anavaa kiatu saizi gani kama alivyonena msanii Mrisho Mpoto katika wimbo wake wa SALAMU ZANGU KWAKO mjomba….na sijui kaishia wapi au ndio wamekwisha mpiga mchanga wa macho asitoe hisia zake zingine maana alikuwa anaamsha walio lala.

  Lakini angalia changamoto utakazozitoa katika ukarabati wako huu mpya usije ukafanya watumiaji wa Blog tukafungiwa kusema lolote maana ndiko tunakoelekea katika uhuru wa habari unaotaka kutiwa kifungoni

  Maasalaaam!!!!!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 34,787 hits
December 2006
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031