Siku chache baada ya Moto wa Mwanjelwa

December 16, 2006 at 1:55 pm 4 comments


PICHANI: ni mabaki ya ndege aliyokuwa amepanda mheshimiwa Akukweti baada ya kupata ajali katika kiwanja kidogo cha ndege jijini Mbeya.

Siku chache baada ya moto uliounguza “mikoba” ya waheshimiwa fulani fulani pale Mwanjelwa, na mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi za Kitanzania kwa baadhi ya wafanyibiashara, akaja Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Mheshimiwa Juma Akukweti, si akaja Mbeya kuona ukubwa wa madhara yaliyotokana na moto huo na kisha kuwapa pole waathirika wa janga hilo!!!

Alipokuwa anataka kuondoka siku hiyo jioni hali ya hewa ikakataa, haikuruhusu apae na ka-ndege kake, akalazimika kuondoka alfajiri ya kesho yake yaani siku ya Jumamosi ya tarehe 16/12/2006. Kwa bahati mbaya sana akakumbana na dhahama la aina yake, ka-ndege kake kakashindwa kumudu kuruka, kakaenda kuvamia nyumba za wakazi zipatazo tatu na kulipuka.

Mungu epushia mbali, mheshimiwa akanusurika japo alipata majeraha yenye kumpa maumivu makali hasa sehemu za kichwani, na yeye na timu ya waliokuwa kwenye ndege hiyo wakawahishwa hospitali ya rufaa ya mkoani Mbeya kwa matibabu.

Kweli uswahilini noma, unajua wazushi wakaanza kudai huko mitaani eti jamaa hakutoa pole bali kuwabeza waathiurika wa moto ule kwa kuwaambia “Tulishawaambia mhame hapa lakini”, kwahiyo?? Huku uswahilini wanadai eti ajali ilitokana na chuki za wakazi aliowapa ukweli kuwa walishaambiwa wahame hawakusikia ndio maana moto ukawafanya kitu mbaya.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mwandishi mwenzangu Theresia Nyantori, wa idara ya Habari na Maelezo (au porojo?), aliyepoteza uhai wake katika ajali hiyo.

i{content: normal !important}i{content: normal !important}i{content: normal !important}

Entry filed under: maskani.

Mbeya, Kunani paleeee, mbona kila kitu kinawaka? Sababu nakupenda rais wangu

4 Comments Add your own

 • 1. MACHWEO  |  December 17, 2006 at 7:42 pm

  Ni habari ya kusikitisha iliyotokea na ninaungana na ndugu wa marehemu, familia na waandishi wote katika msiba uliotokea.
  Ni kweli ajali hutokea hata katika nchi zilizoendelea lakini nadhani siku moja ukweli utadhihirika kwamba kulikuwa na kitu.
  hivi kweli siku hiyo moja tu ilitosha kuwapa pole waliopoteza mali zao au waziri alikuwa na haraka ili kufanya kazi kama viongozi makini waliooneshwa katika shairi la Marwa

 • 2. Geka  |  December 17, 2006 at 7:44 pm

  Bwana Msangi! Kwa sasa blog yako ni nzuri, nzuri sana. Inapendeza si tu kwa mtazamo wa macho bali hata kilichomo kinavuta macho kusoma, picha sikuzote zinamkaribisha msomaji mapema, endelea na kazi mzee

 • 3. MK  |  December 18, 2006 at 11:39 am

  Inasikitisha kusikia ajali hii mbaya imetokea, Pia napenda kuwapa pole kwa familia za watu walio poteza maisha au kupata majeruhi.

  Wote tupo gizani kwamba nini tatizo la kuanguka kwa hii ndege. Ukweli utapatikana kama wakiweza kupata Black box ili kujua mazungumzo ya mwisho ya marubani na kujua nini ilikuwa tatizo zaidi.

  Nadhani serikali itaweza kutoa hizo sababu mapema iwezekanavyo.

  Mwisho, Napenda kutoa tena pole kwa familia na wote walio kumbwa na hili tatizo.

  Nashukuru.

 • 4. Rashid Mkwinda  |  December 20, 2006 at 2:51 pm

  Unajua nini mie nilimuona dada Tedy siku moja kabla ya tukio lile alikuwa akihaha namna ya kutuma taarifa zake gazetini, kwa bahati mbaya siku hiuo kulikuwa na umeme wa mgawo ikabidi atumie fursa hiyo kutuma kupitia Kompyuta yake ya mkononi(Lap Top)na kutafuta sehemu yenye Internet ambapo katika hotel moja kulikuwa na mtandao.

  Inasikitisha dada Tedy alifanikiwa kutuma picha zake zikiwemo zile za soko la Mwanjelwa na baadhi kule Mbarali akiwa na Waziri Akukweti.

  Hakujua kama siku hiyo ndiyo itakuwa mwisho wake wa kuliona jua, ila nakumbuka alinieliza mchele wa Kyela unapatikana wapi na kwa Shngapi nadhani alitumia fursa hiyo kununu mchele kwa ajili ya siku kuu ya X-MASS.

  Masikini dada Tedy hakufanikiwa hata kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mbeya bali ndege hiyo ambayo ilionekana wazi kusheheni mizigo ilishindwa kupaa na kuungua moto.

  Mungu ailaze pema roho ya Dada Tedy AMEN!!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 34,787 hits
December 2006
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031