ya ditopile: tulishindwa kusoma ishara za nyakati?

November 6, 2006 at 9:20 am 8 comments


Duh, ni kama vile yametimia, kwasababu tuliokuwa tukiyaona haya mambo kwa mtazamo wa kipekee, lazima tuseme kuwa tulijua kuwa hili ndilo litakalofuatia, na kwakweli naweza kukiri kuwa haikunishangaza sana niliposikia taarifa hizi jana.
Alikuwepo sijui RPC wa wapi vile nasikia aliwachapa WAPIKAKULA bakora, kama vile anaviadabisha vitegemezi vyake nyumbani. Wakaibuka sijui wale maraisi wa wilaya (DCs), sikumbuki wangapi vile nao tukasikia wamewalamba watu vibao.
Tupo ambao tulihoji, tupo ambao tulitilia mashaka kasi hii, lakini nani alisikia? Na matokeo ya kutokufungwa gavana huku tukijua wazi kuwa asilimia kubwa ya magari yaliyoko katika msafara huu hayako salama, ndio haya sasa ya kina komredi Dito.
Huyu huyu ambaye ni (au alikuwa?) mkuu wa mkoa wa Tabora, huyu huyu ambaye aliwahi kusema kuwa yeye ni Born Town, kwa maana kazaliwa Dar, kasomea shule ya msingi Dar, Sekondari Dar na kila kitu Dar. Na ndio hukohuko ambapo amefanya madudu ya hali ya juu. Soma taarifa za kuhusu ufedhuli wake alioufanya wa kuua raia (mpigakura) kisa? Eti nasikia alikwangua VX lake.
Bonyeza hapa kusoma kwa kiingereza, na hapa na hapa kwa kiswahili.
Picha kwa hisani ya kaka Michuzi

Entry filed under: maskani.

Mkutano wa wana-blogi wa kitanzania Wasamaria wetu na usamaria wa vyombo vya habari

8 Comments Add your own

 • 1. Rashid Mkwinda  |  November 6, 2006 at 11:08 am

  Inasikitisha na kwa kweli haiingii akilini kwa kitendo hiki kilichofanywa na na huyu anayejiita Born Town aka Brother Ditto.

  Nilipata kumsikia mwanafalsafa mmoja akisema kuwa, ”Mvinyo wa mali na madaraka ni ulevi mbaya kuliko ulevi wa tembo” na hapa imedhihiri ulevi wa madaraka na mali ulivyokuwa mbaya.

  Naamini mlevi wa tembo akijilewea tembo lake hawezi kuwa na kiburi bali atajiendea kujilalia na zaidi atajichafulia sarawili yake kwa kujikojolea ama kujinyea,umedhihiri ubabe na ufisadi wa ulevi wa mali na madaraka eti kwa kuwa mtu umepewa fadhila ya kuwa mkuu wa kitengo fulani katika jamii basi na uchukue madaraka mkononi?

  Hapana huu ni mtihani kwa JK kwani nimesikia wana usuhuba wa karibu watu hawa mie nadhani ndicho Brother Ditto anachojivunia kwa nini athubutu kufanya mambo haya ya kishetani?

  Kiburi cha baadhi ya viongozi kujiona wao ni Miungu Watu ndicho kinachodhihiri katika anga hili la Wadudi muumba wa mbingu na nchi,na tuone hatima ya hili jambo.

  Haingii akilini!! hivi Brother Ditto alishindwa angalau basi kuondoa upepo wa gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu?kiburi hiki kakitoa wapi? Ok basi na angechukua nambari za gari kisha akatoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika mimi nadhani sheria ingechukua mkondo wake na mkosaji angechukuliwa hatua za kinidhamu.

  Inauma sana ngoja angalau nisimame hapa nitazungumzia kwa urefu mada hii kibarazani kwangu.

 • 2. luihamu  |  November 6, 2006 at 2:19 pm

  Inauma sana Mzee Msangi,huyu dereva hakuwa na silaa sasa inakaweje huyu muuaji ampige risasi.Kama Saddam kahukumiwa kifo kwa sababu ya kuua rai Iraqi naomba haki itendeke.Wana bloggu hebu tutafakari huyu dereva anafamilia inayomtegemea yeye,watoto wakusomesha,maskini alikuwa anatafuta rizki mwishowe kapigwarisasi pasipo hatia inauma sana.

 • 3. Anonymous  |  November 6, 2006 at 11:38 pm

  Yataenda na kwisha kwani Zombe yupo wapi? Kafungwa au? Huyu na Zombe wote wanyongwe.

 • 4. Anonymous  |  November 7, 2006 at 2:31 pm

  mheshimiwa hapo juu, ni kweli kuwa yatakwisha lakini ni lini na yatakuwa yamesababisha hasara kiasi gani kwa roho za watu wasio na hatia?

  Msangi, ni kweli kuna suala la kutokusomwa kwa ishara za nyakati, leo hii nimeona kwenye gazeti moja eti watu wa kituo cha kutetea haki za binadamu kitawapandisha kizimbani Ma-DC wawili waliowalima vibao wananchi.

  Lakini hivi haya ndio matokeo ya Ngurdoto au?

 • 5. Anonymous  |  November 7, 2006 at 5:23 pm

 • 6. Anonymous  |  November 12, 2006 at 5:54 am

  Why did you stop posting?

  Stop by and see me… I need a flag from your country. 🙂 You don’t even have to leave a comment.

  Thanks!

 • 7. dom  |  November 13, 2006 at 2:43 am

  Hi nice blog , I have no Idea what you’re saying , but , Stop by and see me… I need a flag from your country. 🙂 You don’t even have to leave a comment.

  Thanks!

 • 8. Anonymous  |  November 22, 2006 at 5:36 pm

  Haya ya Dito ni kuonesha jinsi gani Rais Kikwete anavyojali urafiki bila kuzingatia uwezo na heshima ya mtu kwenye jamii. Hii ni serikali ya kulipana fadhila(Nepotism)na haya ndio matokeo yake na hata hawa wmadc wanapiga watu ni haya ya CCM kujali zaidi ukada na si sifa za kielimu na utashi wa mtu.
  Nakwambia tunahitaji mapinduzi ya kweli na kuing’oa hii CCM manake wamefanya hii nchi kama mali ya wachache nadhani.
  Tumekwisha sie tulio na akili timamu, tuchague: kulamba miguu au tujikakamue basi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
November 2006
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930