Sauper=Mzushi……..IRINnews nao je?

September 14, 2006 at 2:45 pm 8 comments

KWA siku ya leo sikuwa na mpango wowote wa kuandika jambo lolote lile hadi pale nilipojikuta (wakati natembelea mtandao), navutiwa na habari ya kuwepo kwa filamu nyingine ambayo inaelezea uozo wa Tanzania, ambayo ilikuwa ikitarajiwa kuzinduliwa Marekani jana. Hapa ilikuwa katika mtandao wa Irinnews, na nikajikuta naingia katika ukurasa wao wa filamu mbalimbali

Nazungumzia Filamu inayozungumzia utumikishwaji wa watoto katika machimbo ya Mererani, watoto ambao kule kwenyewe machimboni ni maarufu kwa jina la Nyoka. Kama nilivyosema kuwa sikuwa na nia ya kuandika leo, na sitopenda niandike mengi zaidi ya dokezo hili na maswali kadhaa.

– Je, mheshimiwa sana JK, ataizungumzia filamu hii akiwa Marekani au atasubiri aje aoiongelee akiwa anaongea na Watanzania kupitia wazee wa Arusha?

– Sauper na filamu yake ya Mapanki tulimwita mzushi na kila aina ya jina mtu alilopendelea katika kupinga alichokionyesha, je, hawa nao ni wazushi?

– Ikumbukwe kuwa filamu hii ilitarajiwa kuzinduliwa wakati mheshimiwa JK akiwa yuko ama tayari ndani ya Marekani, au njiani akitokea Cuba kuelekea huko, je, atawaeleza nini Watanzania walioko Marekani? Ndesanjo nadhani utatujuza kilichojiri maana yuko karibu na maeneo yako ya kujidai.

– Tutafungua webu, blogi na tovuti ngapi kupingana na hili nalo? Tutatumia kiasi gani katika kutengeneza filamu nyingine kwa ajili ya kuipinga hii?

Kwa wale wanaotaka kuona vipande vya filamu hii ya Mererani, kwa kutumia programu ya windows media player, wanaweza kubofya hapa, na wale wanaotumia RealPlayer wabonyeze hapa kuangalia.

Aluta kontinyua…twiwonaga…

Entry filed under: maskani.

TANZANIA: Tumechoshwa na mnavyowafanyia raia wetu Nawatakia Eid Njema wasomaji wangu wote

8 Comments Add your own

 • 1. ndesanjo  |  September 15, 2006 at 10:57 am

  Rama,
  Kiungo cha hiyo filamu mbona sijakiona?

 • 2. Jeff Msangi  |  September 17, 2006 at 2:48 am

  Rama,
  Mimi pia nimeiona hiyo mini-documentary na kubaki kinywa wazi.Nilitumiwa kupitia mtandao fulani wa waandishi wa habari Tanzania na nje.

  Najaribu kujiuliza,serikali yetu itasema nini safari hii? Nadhani haya ni maswali ambayo ni lazima yapatiwe majibu.

 • 3. charahani  |  September 18, 2006 at 6:32 pm

  Msangi unadhani huyu jamaa atarudia tena kukurupuka na kutoa tamko, weeeee sasa hivi yuko makini wewe sababu siku zile alipotoa tamko kesho yake akaenda kule mwaloni akakuta mapanki kibaoooo. Hazungumzii ng’oo, ukweli uanuma sana brother!!

 • 4. msangimdogo  |  September 19, 2006 at 5:51 pm

  Kwa wachangiaji wangu wote:

  Mtanisamehe bure tu kwasababu mara kadhaa nimekuwa nikipandisha kazi ambazo viungo ninavyokuwa nimeweka vinakuwa havifanyi kazi, hali hii imekuwa ikitokana na matatizo au hitilafu kiasi za kiufundi katika kompyuta yangu. Hata hivyo, nimejitahjidi sana kurekebisha tatizo hili na hivi sasa natarajia kuwa kila kitu kitakuwa shwari.

  NDESANJO: viungo ambavyo awali ulishindwa kuvipata nimeviweka sasa na vinafunguka bila matatizo yoyote.

  Nawashukuru sana kwa kunitembelea na kunipa changamoto za kuendelea kudondosha mambo katika jumba langu

 • 5. SIMON KITURURU  |  September 20, 2006 at 11:12 am

  Msangi , tuko wengi tunaopitia hapa kwako kila wakati ingawa hatuachi commets.Dondosha mambo tu.

 • 6. mwandani  |  September 20, 2006 at 3:49 pm

  Nadhani inabidi tukubali mambo ya uwazi kwa njia zote ikiwamo njia filamu.
  Siyo sisi pekee tunatengenezewa filamu. hata kina kichaka wanatengenezewa filamu kwenye masuala ya utata.
  Nimeiona filamu hii kupitia kwenye kiungo cha IRIn wakati ilipotangazwa. Ni wazi kulikuwa na uhariri hasa ukiangalia ule mchezo wa mpira kati ya mtoto wa mererani na mfanyakazi wa NGO – nadhani mchezo ule uliandaliwa kwa ajili ya “happy ending”. Lakini mbwembwe za uhariri haziondoi ukweli kuwa kuna cha moto bongo na watoto wanabeba mizigo mizito ya kusaidia familia.

 • 7. Anonymous  |  September 21, 2006 at 2:16 am

  kutoacha comment kuna mfanya muandishi kupata uvivu wa kuandika sababu hajui kama ana wasikilizaji. Ni vizuri kuacha comment maana nina uhakika kuna chochote la kuchangia.

 • 8. Anonymous  |  September 22, 2006 at 3:04 pm

  Sio lazima kila anayetembelea kasri hili awe na cha kusema, baadhi ya nyakati mtu unakuwa huna la kusema kwahiyo unajikuta umetembelea mahali na kushuhudia tu yaliyosemwa au kutokea mahali husika bila kusema neno. Hata hivyo si kila mara pia mtu atakosa la kusema

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 34,787 hits
September 2006
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930