Archive for September 14, 2006

Sauper=Mzushi……..IRINnews nao je?

KWA siku ya leo sikuwa na mpango wowote wa kuandika jambo lolote lile hadi pale nilipojikuta (wakati natembelea mtandao), navutiwa na habari ya kuwepo kwa filamu nyingine ambayo inaelezea uozo wa Tanzania, ambayo ilikuwa ikitarajiwa kuzinduliwa Marekani jana. Hapa ilikuwa katika mtandao wa Irinnews, na nikajikuta naingia katika ukurasa wao wa filamu mbalimbali

Nazungumzia Filamu inayozungumzia utumikishwaji wa watoto katika machimbo ya Mererani, watoto ambao kule kwenyewe machimboni ni maarufu kwa jina la Nyoka. Kama nilivyosema kuwa sikuwa na nia ya kuandika leo, na sitopenda niandike mengi zaidi ya dokezo hili na maswali kadhaa.

– Je, mheshimiwa sana JK, ataizungumzia filamu hii akiwa Marekani au atasubiri aje aoiongelee akiwa anaongea na Watanzania kupitia wazee wa Arusha?

– Sauper na filamu yake ya Mapanki tulimwita mzushi na kila aina ya jina mtu alilopendelea katika kupinga alichokionyesha, je, hawa nao ni wazushi?

– Ikumbukwe kuwa filamu hii ilitarajiwa kuzinduliwa wakati mheshimiwa JK akiwa yuko ama tayari ndani ya Marekani, au njiani akitokea Cuba kuelekea huko, je, atawaeleza nini Watanzania walioko Marekani? Ndesanjo nadhani utatujuza kilichojiri maana yuko karibu na maeneo yako ya kujidai.

– Tutafungua webu, blogi na tovuti ngapi kupingana na hili nalo? Tutatumia kiasi gani katika kutengeneza filamu nyingine kwa ajili ya kuipinga hii?

Kwa wale wanaotaka kuona vipande vya filamu hii ya Mererani, kwa kutumia programu ya windows media player, wanaweza kubofya hapa, na wale wanaotumia RealPlayer wabonyeze hapa kuangalia.

Aluta kontinyua…twiwonaga…

September 14, 2006 at 2:45 pm 8 comments


Blog Stats

  • 34,786 hits
September 2006
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930