Hongereni Italia lakini……………..

July 12, 2006 at 11:19 am 2 comments

Sina uhakika kama kweli walistahili kubeba kombe lile, lakini jambo pekee ambalo nina uhakika nalo ni kuwa hatimaye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 zilizokuwa zikifanyika nchini Ujerumani, zimemalizika kwa timu bora kutwaa ubingwa.
Yalikuwa ni mashindano ambayo yalikuwa na kila aina ya machungu kwa baadhi ya washabiki na hasa wale ambao timu walizokuwa wakishabikia zilitolewa mapema au katika hatua yoyote ile, lakini hatimaye ilikuwa ni lazima apatikane mshindi, na asingeweza kupatikana kama baadhi ya timu zisingefungwa.
Kwa ujumla, hata hivyo, wapenzi wa mchezo huu hawakukosa la kujifunza, kufurahisha, kukarahisha na mengine mengi kutoka katika timu 32, zilizoshiriki mashindano hayo, ambazo naambiwa pia zilitengeneza habari 32. Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa matukio yote mazuri katika michuano hiyo, tukio la kipekee na la aina yake ambalo halitasahaulika ni lile la aliyekuwa nahodha wa Ufaransa, Zinedine Zidane, kumlima kichwa cha tumbo beki wa Italia, Marko Materazi.
Kumekuwa na tafsiri nyingi sana kuhusiana na tukio lile, lakini kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia uchezaji wa nahodha huyo ambaye mechi ile ilikuwa ya mwisho kwake, watakubaliana nami kuwa kulikuwa na kitu kikubwa zaidi ambacho masikio yake yalikisikia toka kwa beki yule wa Italia kilichomkasirisha kwa namna ile, na hapa ndipo linapokuja swali la Je, Soka imefanikiwa kuondoa mbegu za ubaguzi na chuki baina ya wanaohusika katika mchezo hjuo kwa kiwango kinachokubalika?
Bravo Italia…….Bravo Ufaransa…..Bravo Zinedine Zidane kwa kutwaa kiatu cha dhahabu. Ukweli ni kuwa dunia itakukumbuka kwa mema ulioifanyia soka.

Entry filed under: maskani.

Makamba!! Yaani ni kaaazi kweli kweli Serikali ya Viwango na ‘hang-over’ ya Mapanki

2 Comments Add your own

 • 1. P. Situmbeko Nalitolela  |  July 16, 2006 at 12:11 pm

  marekebisho madogo tu kaka Msangi ni kuwa…
  Zidane hakutwa kiatu cha dhahabu; tuzo hii huchukuliwa na mfungaji bora ambaye kwa mwaka huu alikuwa Miroslav Klose wa Ujerumani.

  Zizou alitwa mpira wa dhahabu… tuzo ambayo hutunikiwa mchezaji bora wa michuano husika ya kombe la dunia.

  Nikiwa mshabiri mkubwa wa Zidane nitakuwa wa kwnza kusema kuwa sina uhakika sana kama alistahili tuzo hiyo. Kwa maoni yangu ilikuwa kujikosha kwa waandishi wa habari waliomchagua (asilimia kubwa wakiwa wazungu) ambao daima hupenda kuepka utata unaoletwa na majadiliano juu ya hoja hii ya ubaguzi katika mpira (na nyanja nyinginezo katika ulimwengu huu wa kwanza).

  Ninaamini kwa Zidane kama wachezaji wengineweo kadhaa alicheza vyema. Ila kutwaa kwake tuzo ya mchezaji bora ninaamini kuwa kwa kiasi kikubwa kulichangiwa na yeye kupewa kadi nyekunduu katika mchezo wake wa mwiso wa ushindani kulikosababishwa na yeye kusikia maneno toka kwa Marco Materazzi wa Italia ambayo kwa namna 1 au nyingine hakumfurahisha shujaa huyu wa ufaransa.

  Hisia kubwa miongoni mwa wapenzi wa soka hasa wa nchini ufaransa ni kuwa “matusi” hayo yalikuwa ymeelemea katika ubaguzi wa rangi na kidini. Hivyo ili kuondosha aibu hiyo, “paneli” inayokaa kuchagua mshindi was mpira wa dhahabu ilimpendekeza ZZ kutwaa mpira huo. Bado tunasikilizia lakini neno la mwisho toka FIFA. Maana kama alivyotukumbusha mchemfu wetu Blatter kuwa kamati ya utendaji ya FIFA inayo uwezo wa kuzuia tuzo hiyo.

  Ngoja tuone.. na nina hamu sana kujua ukweli juu ya yale yaliyosemwa siku ya siku kupelekea kichwa kile kitakatifu kutua juu ya kifua cha Marco kwa nguvu mithili ya radi.

  Nikiwa naangalia mbele na kungojea Suazi 2010 ni wenu.. P. S. Nalitolela

 • 2. MACHWEO  |  August 12, 2006 at 2:16 pm

  Ulichoandika kuhusu MAPANKI ni sahihi kabisa, mtayarishaji wa filamu hiyo anaweza kuwa kaweka chumvi kwenye uingizaji wa silaha, lakini mambo mengine ni ukweli tena usio na kutu, ningependa sana kama makala hii ikasomwa nawengi kwa kuituma katika gazeti lolote linalowafikia wengi.
  Maoni ya wabunge nayo ni yakushangaza nimemsikiliza Cheyo Momose huyu hana cha maana zaidi ya kutaka kujipendekeza tu au labda kwa vile yeye na wenzake kwanza hawayajui hayo mapanki ndo maana wanacomment kitu kama hicho. Mbunge wa busega kasema kweli watu wanakula haya mabaki lakini wanafaidika nayo pia. Viongozi wetu ni wanafiki, hii ndo hulka yao wanadhani kwamba kwa vile wao wala na kuacha makombo basi na watu wengine wanafanya vivyo hivyo. Mapanki yapo na watu wanayala sana tena sana mheshimiwa hata akasirike vipi sisi watu wa kawaida tunamuunga mkono bw. Sauper kwa kuanika kile watawala hawataki kioneshwe na kutambulika kwa jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
July 2006
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31