Archive for July 12, 2006

Hongereni Italia lakini……………..

Sina uhakika kama kweli walistahili kubeba kombe lile, lakini jambo pekee ambalo nina uhakika nalo ni kuwa hatimaye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 zilizokuwa zikifanyika nchini Ujerumani, zimemalizika kwa timu bora kutwaa ubingwa.
Yalikuwa ni mashindano ambayo yalikuwa na kila aina ya machungu kwa baadhi ya washabiki na hasa wale ambao timu walizokuwa wakishabikia zilitolewa mapema au katika hatua yoyote ile, lakini hatimaye ilikuwa ni lazima apatikane mshindi, na asingeweza kupatikana kama baadhi ya timu zisingefungwa.
Kwa ujumla, hata hivyo, wapenzi wa mchezo huu hawakukosa la kujifunza, kufurahisha, kukarahisha na mengine mengi kutoka katika timu 32, zilizoshiriki mashindano hayo, ambazo naambiwa pia zilitengeneza habari 32. Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa matukio yote mazuri katika michuano hiyo, tukio la kipekee na la aina yake ambalo halitasahaulika ni lile la aliyekuwa nahodha wa Ufaransa, Zinedine Zidane, kumlima kichwa cha tumbo beki wa Italia, Marko Materazi.
Kumekuwa na tafsiri nyingi sana kuhusiana na tukio lile, lakini kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia uchezaji wa nahodha huyo ambaye mechi ile ilikuwa ya mwisho kwake, watakubaliana nami kuwa kulikuwa na kitu kikubwa zaidi ambacho masikio yake yalikisikia toka kwa beki yule wa Italia kilichomkasirisha kwa namna ile, na hapa ndipo linapokuja swali la Je, Soka imefanikiwa kuondoa mbegu za ubaguzi na chuki baina ya wanaohusika katika mchezo hjuo kwa kiwango kinachokubalika?
Bravo Italia…….Bravo Ufaransa…..Bravo Zinedine Zidane kwa kutwaa kiatu cha dhahabu. Ukweli ni kuwa dunia itakukumbuka kwa mema ulioifanyia soka.

July 12, 2006 at 11:19 am 2 comments


Blog Stats

  • 35,058 hits
July 2006
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31