Ni kweli Prof. Charles Bwenge, lakini……….??

June 9, 2006 at 10:36 am 3 comments

Sijui ni wasomaji wangu wangapi ambao ni marafiki wa Profesa Charles Bwenge, lakini naamini huenda wapo na kama wapo basi naomba wanifikishie ujumbe huu kwake, kwamba “Kijiji cha Wana-Blogi wa Kitanzania kinamhitaji sana katika makazi yao kwasababu tayari nyumba yake imeshaandaliwa ikiwa na kila kitu ndani yake, anachotakiwa kufanya yeye ni kuhamia tu basi”

Profesa Charles Bwenge, ni mmoja kati ya waandishi ambao nimekuwa nikiwahusudu sana kwa kazi zao. Amekuwa akiandika sana katika gazeti la Rai na mara nyingi, nimekuwa nikisoma kazi zake. Ingawa kuna kazi zake nyingi sana ambazo ningeliweza kuzizungumzia, kwa leo napenda niizungumzie zaidi kazi aliyoaiandika katika gazeti hilo toleo namba 661, yenye kichwa cha habari “MAKAO MAKUU YA SERIKALI YA TANZANIA YAKO WAPI, DAR ES SALAAM AU DODOMA?”

Katika makala yake hiyo, Prof. Bwenge, anachagiza makala yake kwa maelezo aliyoyakuta katika tovuti ya Tanzania, kuhusiana na kile kinaitwa MJI MKUU ambapo ananukuu maelezo toka katika tovuti hiyo yakisema “Ukiwa na idadi ya takriban wakazi 300,000 (1998), mji wa Dodoma ulioko umbali wa km 309 magharibi mwa Dar es salaam, ndio makao makuu ya siasa na utawala. Dar es salaam ni mji mkuu wa biashara na uchumi”

Maelezo hayo kutoka katika tovuti ya Serikali, yanampa prof. Bwenge maswali kadhaa kubwa likiwa “Kama ndivyo mheshimiwa Kikwete na Serikali yake wanafanya nini Dar es salaam?” Swali ambalo naamini si tu kuwa limedumu katika vichwa vya Watanzania, bali pia kuwa linaulizwa kwa muda wa miaka nenda rudi sasa.

Pengine tu nami naweza kuongeza maswali kadhaa kwa Serikali zilizotangulia na hii ya Ari, Nguvu na Kasi mpya, kwamba “Mlichaguliwa kwa ajili ya kuwaongoza waliowachagua au kwa ajili ya kupata uhalali wa kusimamia biashara zenu na vitega uchumi vyenu vilivyoko ndani ya Mji Mkuu wa biashara na uchumi?”

Nimalizie tu kwa kumwambia Prof. Bwenge kuwa, ukumbi wa majadiliano katika magazeti yetu bado ungali finyu sana, na hili linasababisha maswali ya muhimu kama hayo kutokuwa na uwanja mpana wa kujadiliwa kwa uwazi (sana sana watu watajadili vichwani mwao na kwenye vikao vya stuli ndefu), lakini ukija huku kwenye Blogi, utakuwa umewatendea haki zaidi wasomaji wako kwa maana utawapa mwanya wa kujimwaga kwa kadiri watakavyo kujadili miswada muhimu kama hiyo.

Entry filed under: maskani.

Ndugu zangu wapendwa!! Nilikuwa na wiki la maojnz… Watalii wazalendo

3 Comments Add your own

  • 1. Mija Shija Sayi  |  June 9, 2006 at 10:47 pm

    Msangi umefikiria jambo la maana sana. Tunahitaji watu kama hao pia ili tuweze kukomaa zaidi.

  • 2. severine  |  June 12, 2006 at 3:45 pm

    Nimefurahishwa sana,kwa jitihada yako kubwa la kumwalika prof,Bwenge naye ablogu!Huwa nafuatilia sana makala zake anazotoa kwenye gazeti la Rai.Ni makala nzito na ambazo zimefanyiwa utafiti wa kutosha.Kama unavyosema kwa kiasi kikubwa akijiingiza kwenye blogu ,tutapata nafasi ya kuchangia na kutoa maoni kuhusiana na mada zake nzuri.Tafadhali endeleza ushawishi wako bw.Msangi ili tumuone huyu jamaa hewani siku za karibuni!

  • 3. Jeff Msangi  |  June 13, 2006 at 8:21 pm

    Ahsante Msangi kwa habari hii na kumkaribisha Prof.Ukiliangalia vizuri suala la Dodoma na jinsi ambavyo serikali yetu inatumia mabilioni ya shilingi kwa ndoto hii isiyoisha utagundua kwamba hatuna viongozi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

  • 35,061 hits
June 2006
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930