Archive for May 29, 2006

Ndugu zangu wapendwa!! Nilikuwa na wiki la maojnz…

Ndugu zangu wapendwa!!

Nilikuwa na wiki la maojnzi makubwa kwa kumpoteza mmoja kati ya babazangu wakubwa, ambaye alikuwa nguzo muhimu sana kwa familia yetu kwa ujumla. Baba yangu huyo mkubwa, Ally Shaban Msangi, alifariki Jumatatu ya tarehe 22/05/2006, akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akiendelea na matibabu ya tatizo la jino, ambalo lilimsumbua kwa zaidi ya miezi mitatu.

Kwa hali jinsi ilivyo kuwa, kwa hakika pengine hilo ndilo lilikuwa jema kwake yeye, kwa maana alishateseka na maumivu kiasi cha kutosha, lakini kwa namna yoyote ile kifo chake hakika limekuwa pigo kubwa lisilomithilika maishani mwangu na wanafamilia wenzangu kwa ujumla. Ninawashukuru wote wale ambao walishirikiana nami katika kipindi hiki kigumu sana, na hasa rafiki yangu na kipenzi changu Pamella.

Nawashukuru wote kwa ujumla wenu maana ni vigumu sana kuwataja wote hapa, na Mungu atawalipa kwa kila mliloshirikiana nami. Ni njia ya kila mwanadamu kuelekea maisha ya Ahera, na hakika kila mwanadamu ataipita. (Kul-nafsi dhaalikatul mauti)

Tulimpenda sana mzazi wetu, lakini Muumba amempenda zaidi yetu, na tunaamini atamlaza mahali pema peponi mzazi wetu.

May 29, 2006 at 2:03 pm 8 comments


Blog Stats

  • 35,058 hits
May 2006
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031