hatuna la Kujutia

May 21, 2006 at 2:54 pm 4 comments


Kwa hakika zilikuwa ni dakika 15 zenye machungu sana, lakini hakuna la kujutia. Sina uhakika kama kweli walistahili nasi hatukustahili, lakini nina uhakika kuwa hatimaye Kombe lilienda mikononi mwao. Nazungumzia pambano la fainali ya mwaka huu ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya baina ya Arsenal na Barcelona, lililofanyika katika uwanja wa State -de- France.

Najua kuwa walirejea jijini kwao wakiwa na furaha tele na pia wakichukuliwa kama ni mabingwa kweli kweli, lakini halimaanishi kuwa vijana wa Arsenal walirejea London wakiwa vichwa chini, kwamaana walidhihirisha wazi kuwa licha ya Barcelona kuweza kuzifanya timu zingine kuonekana za kawaida sana, wao Arsenal waliweza kuifanya Barcelona kuonekana timu ya kawaida kabisa.

Nadhani watakuwa waungwana zaidi kwa kumpongeza wazi mwamuzi wa fainali ile, Terje Hauge, kwa “kucheza nafasi muhimu sana” katika ushindi wao huo, kwasababu hata yeye mwenyewe amekiri kuwa alivurunda (ita vyovyote upendavyo lakini haitabadili maana), na kwangu mimi, mwamuzi yule ameonyesha tena umuhimu wa wadau hawa muhimu katika soka kujitizama sana pindi wanapokuwa wamepewa dhamana kama ya kuchezesha pambano kama lile. na ninadhani pia hatutokuwa na mtu wa aina yake wakati wa fainali zijazo zitakazofanyika katika jiji la Athens, Ugiriki.

Kwa hakika tuna jambo moja tu la kufikiria, nalo ni kukosa kombe, na kwa uhakika huo huo, tuna mambo kadhaa ya kujivunia kutokana na mchezo ule, kutokana na shujaa wetu ambaye Bw. Dein alikataa kumuuza kwa dau lolote lile, kukubali kudondoka wino katika mkataba wake mpya utakaompa haki ya kuendelea kuwa mshika bunduki za maangamizi kwa miaka minne zaidi.

Waswahili husema; Asiyekubali kushindwa si mshindani” nami naamini hivyo kwasababu tusingekubali leo hii Barcelona wasingekuwa mabingwa.

Entry filed under: maskani.

InGeKuWa ViPi?! Ndugu zangu wapendwa!! Nilikuwa na wiki la maojnz…

4 Comments Add your own

 • 1. Beka - Tanga  |  May 21, 2006 at 4:00 pm

  Kwa kuwa mstaarabu tu ni lazima nikiri kuwa sikuwahi kuwa mpenzi wa Arsenal kikamilifu, lakini pia inapotokea zikapambana timu za England na mataifa mengine huwa napenda zile za England, ilinifadhaisha hata mimi, niliondoka kwenda kulala mara baada ya kadi nyekundu ile ambayo nadhani ilikuwa ya kipuuzi kupita kiasi.

 • 2. mwandani  |  May 22, 2006 at 4:45 pm

  Jambo la kusikitisha ni kwamba wanasema mpira magoli. Chenga twawala haifui dafu.

  Nawapa hongera vijana wa Arsenal, kuwadhibiti Barcelone kwa muda mrefu, wakiwa wachache, mpaka dakika 15 za mwisho.

  Naungana na mkuu wa FIFA aliyesema refa angefuata kawaida za uamuzi na kutoa advantage badala ya kadi nyekundu – Arsenal icheze na watu 11.

  Niliamka kuangalia mechi iliyonipunguzia raha siku nzima. haidhuru, kiwango cha Arsenal kilikuwa ni cha hali ya juu, na Henry nasikia atabaki.

 • 3. zemarcopolo  |  May 22, 2006 at 7:24 pm

  pole msangi yote mambo tu katika mpira…je unadhani mwaka huu Ronaldinho atasherehekea mara mbili?

 • 4. fotomaton para bodas murcia  |  September 16, 2014 at 11:24 pm

  Fully sympathize with the writer of this website. Very good content. I subscribe. To continue, has totally loved the blog.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
May 2006
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031