Archive for May 21, 2006

hatuna la Kujutia


Kwa hakika zilikuwa ni dakika 15 zenye machungu sana, lakini hakuna la kujutia. Sina uhakika kama kweli walistahili nasi hatukustahili, lakini nina uhakika kuwa hatimaye Kombe lilienda mikononi mwao. Nazungumzia pambano la fainali ya mwaka huu ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya baina ya Arsenal na Barcelona, lililofanyika katika uwanja wa State -de- France.

Najua kuwa walirejea jijini kwao wakiwa na furaha tele na pia wakichukuliwa kama ni mabingwa kweli kweli, lakini halimaanishi kuwa vijana wa Arsenal walirejea London wakiwa vichwa chini, kwamaana walidhihirisha wazi kuwa licha ya Barcelona kuweza kuzifanya timu zingine kuonekana za kawaida sana, wao Arsenal waliweza kuifanya Barcelona kuonekana timu ya kawaida kabisa.

Nadhani watakuwa waungwana zaidi kwa kumpongeza wazi mwamuzi wa fainali ile, Terje Hauge, kwa “kucheza nafasi muhimu sana” katika ushindi wao huo, kwasababu hata yeye mwenyewe amekiri kuwa alivurunda (ita vyovyote upendavyo lakini haitabadili maana), na kwangu mimi, mwamuzi yule ameonyesha tena umuhimu wa wadau hawa muhimu katika soka kujitizama sana pindi wanapokuwa wamepewa dhamana kama ya kuchezesha pambano kama lile. na ninadhani pia hatutokuwa na mtu wa aina yake wakati wa fainali zijazo zitakazofanyika katika jiji la Athens, Ugiriki.

Kwa hakika tuna jambo moja tu la kufikiria, nalo ni kukosa kombe, na kwa uhakika huo huo, tuna mambo kadhaa ya kujivunia kutokana na mchezo ule, kutokana na shujaa wetu ambaye Bw. Dein alikataa kumuuza kwa dau lolote lile, kukubali kudondoka wino katika mkataba wake mpya utakaompa haki ya kuendelea kuwa mshika bunduki za maangamizi kwa miaka minne zaidi.

Waswahili husema; Asiyekubali kushindwa si mshindani” nami naamini hivyo kwasababu tusingekubali leo hii Barcelona wasingekuwa mabingwa.

May 21, 2006 at 2:54 pm 4 comments


Blog Stats

  • 34,787 hits
May 2006
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031