InGeKuWa ViPi?!

April 30, 2006 at 5:25 pm 8 comments

Unadhani ingekuwa vipi?

Kama siku moja Mungu akiamua kuyafumua mapaa ya nyumba hapa duniani wakati wa usiku wa manane? Na unadhani ingekuwa vipi ikiwa katika hali ya nyumba hizo kuwa wazi kwa juu, Mungu akashusha nuru ya ghafla japo kwa dakika kama tano tu hivi kusudi muone kinachotokea ndani ya nyumba za watu usiku huo wa manane?

Ingekuwa vipi kama vijana wa Kitanzania wangeamua kwa dhati kabisa kuacha kushinda vijiweni wakikoka ganja na badala yake wakawa wanashinda katika viunga vya mahakama wakisikiliza uendeshaji wa kesi mbalimbali?

Ingekuwa vipi siku Sirikali ikiamua kuhalalisha bangi na kupiga marufuku sigara? Unadhani bei ya bidhaa hiyo ingekuwa kubwa na kuzidi kuwatajirisha wanaoifanya kwa kasi kubwa kiasi cha sasa?

Ingekuwa vipi Sirikali ingehalalisha Gongo na kupiga marufuku bia tulizozizoea kwa sasa? Unadhani vifo vinavyotokana na Gongo vingepungua kwasababu vingi vinatokana na wahusika kuinywa kwa kuikomoa kwakuwa kesho wanaweza kuja wakakuta mama muuza yuko Lupango?

Ingekuwa vipi kama Sirikali ingeamua kuwa kuanzia sasa mabadiliko yote yatakuwa yakifanyika kuanzia vijijini kuelekea mijini na sio kinyume chake? na unadhani Ingekuwa vipi kama leo nisingekuuliza Ingekuwa Vipi?…….. UTAJIJU!!

Entry filed under: maskani.

Mafanikio ya China na Azimio lililotelekezwa Tanzania hatuna la Kujutia

8 Comments Add your own

 • 1. Jeff Msangi  |  April 30, 2006 at 11:06 pm

  Maswali muhimu,yanafungua fikra fulani ambazo huwa zinakuwa zimelala.

 • 2. ndesanjo  |  May 2, 2006 at 6:47 pm

  Ingekuwa vipi polisi wangetiwa rumande, mahakimu kuhukumiwa, viongozi kuongozwa, walimu kufundishwa, makasisi na mashehe kuhubiriwa, wazazi kujifunza toka kwa watoto…ingekuwa vipi?

 • 3. John Mwaipopo  |  May 2, 2006 at 9:41 pm

  Yoote umeongea lakini umenikuna sana uliposema kuhusu Gongo. Nalihusudu sana. Hivi kijeti bado shilingi 900/=. Nikifika Mbeya breki ya kwanza kwa mama muuza. Jasiri haachi asili.

 • 4. Reginald S. Miruko  |  May 3, 2006 at 8:36 am

  Ingekuwa vipi kama wote mnaochangia mada hii mngetoa majibu badala ya kuuliza tena maswali?

 • 5. charahani  |  May 3, 2006 at 1:35 pm

  Ingekuwa vipi Bongo ingekuwa New York, ingekuwa vipi wanawake wangekuwa wanaume, ingekuwa vipi matajiri wangekuwa masikini… Falsafa hii ni kali sana sijui tuirejeshe

 • 6. Mija Shija Sayi  |  May 4, 2006 at 9:10 pm

  Ingekuwa hatari tupu!!!!

 • 7. MK  |  May 5, 2006 at 1:54 pm

  Ingekuwa vipi Afrika ingetawala mabala yote duniani?

  Ingekuwa vipi kama Afrika ingekuwa na Amani na bara Tajiri duniani?

  Ingekuwa vipi kama Tanzania kusingekuwa na matabaka ya kidini, kisiasa, masikini na matajiri?

  Ingekuwa Vipi kama Binadamu wote duniani tungeishi kwa Amani na Upendo?

  Ingekuwa Vipi kama kila binadamu tunge thaminiana na kusaidiana kwa dhati?

  Ingekuwa Vipi kama kungekuwa hakuna shule wala mitihani?

  Ingekuwa Vipi kama kusingekuwa na utawala wa kisheria?

  Ingekuwa Vipi kama Yesu akirudi leo?

  Ingekuwa Vipi kama Mungu aseme hakuna hukumu ya mwisho na ametusamehe wote?

  Ingekuwa vipi kama ukiweza kuacha kutenda dhambi?

  Ingekuwa vipi kama dawa ya Ukimwi ingepatikana?

  Ingekuwa vipi kama kusingekuwa na maradhi, Uzee na Vifo?

  Ingekuwa vipi kama duniani kusingekuwa na maumivu, majonzi na matatizo mengi?

  Ingekuwa vipi kama ukitoa 10% ya mshahara wako kusaidia wasio jiweza?

  Ingekuwa vipi?

 • 8. SIMON KITURURU  |  May 21, 2006 at 10:47 am

  Nivizuri kujiuliza haya maswali lakini ukweli ni kwamba tunaishi leo katika hali halisi ya leo .Ujanja ni kujaribu kufikia maamuzi ambayo yanatatua matatizo ya leo na pia kujaribu kujenga mifumo nchini ambayo itatatua matatizo ambayo yata jitokeza hapo baadaye kutokana na mwelekeo wa jamii na mapungufu yaliopo leo. Kuna mambo mengi ambayo ni tatizo sasa hivi matatuzi yake yangeweza kupatikana kama mitazamo ya matatuzi ya matatizo ingeweza kubadilishwa.Mfano badala ya kupiga marufuku gongo, basi wafundishe waitengenezayo kuitengeneza katika vipimo salama.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
April 2006
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930