Maisha Bora kwa kila Mtanzania, ndani ya siku 100 na ushee

April 16, 2006 at 8:49 am 2 comments

Mpika-Kula, mwenye maskani yake katika kitongoji cha Chanji ndani ya Manispaa ya Sumbawanga, akiwa anatafakari ndoto za kuwa miongoni mwa Watanzania wanaotarajiwa kushirikishwa katika Mpango wa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania

Maskani ya Wapika-Kula wengine ambao pia wanawazia Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kama yalivyoahidiwa kwao na Sirikali yao ya awamu ya nne, chini ya mheshimiwa saaaaaaaana JMK

Entry filed under: maskani.

Azimio la Dodoma na ujio wa Teknolojia mpya Mafanikio ya China na Azimio lililotelekezwa Tanzania

2 Comments Add your own

 • 1. Rashid Mkwinda  |  April 16, 2006 at 2:38 pm

  Haya ndiyo maisha ya WADANGANYIKA wa zama hizi,WADHULUMIKA wa kula za Desemba 14 na WAFITINIKA wa miaka mitano ijayo ndani wimbi la umaskini kwa miongo minne na ushee, shida ya maji safi, umeme, maradhi, ujinga, umaskini uliopea, huku akina yakhe wakiendelea kuketi katika vibaraza vya kahawa wakipiga domo bila kujua watakula nini siku hiyo, ilhali watoto wao wakiachishwa masomo kwa ajili ya kuozwa ili kujikimu kimaisha ambapo watoto wa wakubwa wakipelekwa nje ya nchi kusoma kwa gharama kubwa.

  Akina yakhe wa Chanji huko Sumbawanga mkoani Rukwa wao nnndio hata habari hawana kama kuna siku wataondokana na wimbi hili la ukandamizwaji wa aina yake, hapo alipo mzee huyu nadhani sidhani kama mtoto wake anaenda shule ikiwa hali ndio hiyo, Du!! Afana aleik hii ni hatari lakini salama, sasa tufanyeje ndiyo tumezaliwa katika Jamhuri ya Wadanganyika tutaendelea kudanganywa hadi tunaingia kaburini wa vitegemezi vyetu navyo vitaendelea kudhulumika hadi…… ni fitina ya karne na karne labda Nabii Issa(YESU) aje kuukomboa ulimwengu, vinginevyo tutaendelea kumenyeka hivyo hivyo, na kuendelea kuwa wakimbizi katika nchi yetu iliyojaa rasilimali tusizoweza kuzitumia na kuamua kuwauzia wawekezaji nje ya nchi…

  Patamu hapo….huyu Bw. Msangi kweli ama fikra za aina yake unapenda kuwakuna watu kunako mtima wa moyo na kutaka kuwaliza na hatimaye kufikiria kuwa wakimbizi kuondoka kabisa katika nnnchi hii ya Wadhulumika….hapana sishawishi watu waanze kukimbia nchi, tuna kila kitu cha kujivunia isipokuwa ni mbinu mbadala za kuweza kuzitumia rasimali hizo zimekosa viongozi wabunifu.

  Tutaendelea kuwa hivyo hivyo ooho mkalaghe Bahoo!!!!!

  Wakatabahu

 • 2. severine  |  April 23, 2006 at 1:33 pm

  ni kweli bado kwa kiasi kikubwa sana sisi bado ni wadanganyika!Kuna tofauti kubwa mno ka ti ya hizo picha mbili na kwa kuweza kutuonyesha hizo picha mbili umefanya jambo la maana sana bwana msangi!
  Maisha bora kwa kila mtanzania yatafankiwa akuondoa hiyo tofauti!au tutaendelea kubakia kwenye udanganyika !

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,061 hits
April 2006
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930