Kwanza Tujipongeze

March 29, 2006 at 2:36 pm 12 comments

Hii ni mahususi kwa mashabiki wenzangu wote wa Arsenal kokote kule waliko duniani. Kwa hakika ulikuwa usiku wa aina yake, kumkaribisha tena aliyekuwa nahodha na shujaa wetu kwa misimu tisa mfululizo hadi msimu uliopita, Patrick Vieira, lakini pia kuonyesha kile ambacho kocha wa Vijana hao wa Kaskazini mwa London, Arsene Wenger, amekuwa akikizungumza siku zote kuwa kulikuwa na umuhimu wa kuvipa vipaji vyake nafasi ya kuonyesha makali yao.

Hakika ulikuwa usiku wa aina yake kwa kijana chipukizi Cesc Fabregas, ambaye aliweka kando umri wake na kuweza kuliongoza vyema jahazi la Wapiga Bunduki wa London, kuibuka na ushindi mnono wa bao 2-0 dhidi ya Juventus (Bibi Kizee wa) Turin , katika pambano la kwanza baina ya mawili yatakayowakutanisha katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa bara la Ulaya.

Shukrani za kipekee pia zinastahili kumwendea beki mwafrika kutoka Ivory Coast, Kolo Toure, kwa kazi nzuri aliyoifanya, sanjari na wachezaji wote wa klabu hiyo. Hata hivyo, mapambano bado yanaendelea…….

Advertisements

Entry filed under: maskani.

Kizazi chetu kipya, Dini zetu za kisasa na Hatma yetu Siku 100 za staili ya MBWA (Management By Walking Around)

12 Comments Add your own

 • 1. MK  |  March 29, 2006 at 5:25 pm

  Kweli nina wapongeza vijana wa Arsenal kwa kuwabana Juventus maana hile match ilikuwa tough yaani Arsenal wameonesha domination karibia dakika zote 90.

  Kama mwendo ukiwa ni ule ule na Milan, Barcelona, Internazionale wakibanwa kama Real Madrid na Juventus walivyo banwa basi mnaweza mkalichukua Kombe maana Lyon na Villarreal sio wagumu kama hao wazee watatu.

  Msikate tamaa Arsenal mtafika tu, Lakini msije mkadhani game is over maana hawa jamaa wana uwezi wa kubadilisha matokeo dakika yoyote sasa mkae mkao wa kula mkienda the Stadio Delle Alpi hapo ktk mji wa Turin nchini Italy muwe macho msije mkalia kilio kisicho isha.

  Kama mkija mkachukua kombe basi itakuwa History maana sijawaona ktk hii orodha. Jitaidini muweze kuweka History.

  Habari za Arsenal bonyeza hapa. Picha za Arsena bonyeza hapa.

  Nashukuru,
  ©2006 MK

 • 2. Anonymous  |  March 29, 2006 at 6:14 pm

  Msangi,
  Huu ni upuuzi..wewe na Arsenal wapi na wapi bwana.Ushawahi hata kufika huko London?Kwanini wabongo tunakuwa wapumbavu na watumwa namna hii?Hivi huko Arsenal kuna hata mtu anajua nchi inayoitwa Tanzania?Wangekuwa na wao ni mashabiki wa Barcelona na Juventus ungeisikia wapi hiyo Arsenal?Tuziunge mkono timu za kwetu kwa hali na mali na maarifa.Acha upuuzi huu Msangi

 • 3. Anonymous  |  March 29, 2006 at 7:15 pm

  Ni upenzi tu jamani na mimi naipenda sana hii timu tusionane wabaya.Naipenda hii timu jamani.

  Kupendaga hizi timu wajameni sio kuwa tumesahau za nyumbani hii nina maanisha Binadamu upenda vingi.

  Na haya ni mawazo yangu jamani, Naipenda hii timu.Tuache jaziba zisizo na miguu.Kwani hatupo ktk uditekta kusema kwamba hatuna haki ya kupenda tutakacho. Kila mtu na mapenzi yake sasa tusilazimishane mengine wajameni. Ni mimi OBANDO LYIMO

 • 4. Anonymous  |  March 29, 2006 at 7:30 pm

  Bravo Arsène Wenger

  Bravo vijana wa Highbury:

  GK –> Goalkeeper
  MF –> Midfielder
  DF –> Defender
  FW –> Striker

  No. Position Player
  1 GK Jens Lehmann
  2 MF Abou Diaby
  3 DF Ashley Cole
  7 MF Robert Pirès
  8 MF Fredrik Ljungberg
  9 FW José Antonio Reyes
  10 FW Dennis Bergkamp
  11 FW Robin van Persie
  12 DF Lauren
  13 MF Alexander Hleb
  14 FW Thierry Henry (captain)
  15 MF Francesc Fàbregas
  16 MF Mathieu Flamini
  17 MF Alexandre Song (on loan from Bastia)

  18 DF Pascal Cygan
  19 MF Gilberto Silva
  20 DF Philippe Senderos
  21 GK Mart Poom

  No. Position Player
  22 DF Gaël Clichy
  23 DF Sol Campbell
  24 GK Manuel Almunia
  25 FW Emmanuel Adebayor
  27 DF Emmanuel Eboué
  28 DF Kolo Touré
  29 MF Sebastian Larsson
  32 MF Theo Walcott
  33 FW Nicklas Bendtner
  34 DF Matthew Connolly
  36 MF Johan Djourou
  37 DF Ryan Garry
  38 DF Kerrea Gilbert
  41 FW Arturo Lupoli
  42 GK Vito Mannone
  43 MF Ryan Smith
  44 MF Fabrice Muamba
  45 FW Anthony Stokes

  Fingers Crossed kombe hilo linanukia. Emmanuel Kamugisha – Mkereketwa.

 • 5. Bakari Ally  |  March 31, 2006 at 10:05 am

  Kuna sababu nyingi sana za kukipenda kitu na moja ya sababu hizo inaweza kuwa kujifunza kupitia kitu hicho…Watanzania hatutaki kukubali kuwa kupitia kwa wenzetu walioendelea tunaweza kabisa kujifunza mambo mengi na yenye faida kwetu, badala yake tunataka tuvichukie…huu ni wivu, tena wivu usiokuwa wa kimaendeleo…..kama hujui, hujui tu, na kama mwenzako anajua, basi anajua tu, kubaliana na ukweli huo ndio utaweza kujifunza

  Tuache kujilazimisha kupenda vyetu eti tu kwasababu ni vyetu……Bravo Msangi…..Bravo Arsenal

 • 6. mwandani  |  March 31, 2006 at 10:33 am

  Na mie natoboa siri, naipenda Arsenal – gunners! Kwa sababu wamesaidia sana kubadili sura ya kandanda. Kuna mechi walicheza bila muingereza hata mmoja uwanjani.
  pengine nampenda zaidi Henry. hebu nimsie King Honree.

 • 7. ndesanjo  |  April 2, 2006 at 7:05 pm

  Kama mtu unapenda soka kupindukia, ni vigumu sana kujizuia kuacha kushabikia timu za nchi nyingine kutokana na kiwango cha chini kabisa cha timu zetu. Sababu inayofanya Waingereza, kwa mfano, wakawa wanashabikia timu za Uingereza badala ya timu za Italia au Uhispania, ni ukweli kuwa wao nao wana timu nzuri zenye kiwango cha juu kama timu za nchi nyingine. Sasa kwanini wakimbilie timu hizo? Lakini kwetu ni tofauti. Timu zetu bado safari ni ndefu sana. Makocha hawana mafunzo ya kutosha, wachezaji hawana ujira wa kuaminika, hawana bima, makocha hawalipwi, viwanja vibovu, vyama, wizara na taasisi zinazohusika ni sifuri, n.k. Watu wanaodiriki kutumia fedha zao kutazama mechi uwanja wa taifa, kwa mfano, ni vigumu sana wakatazama mechi kama za kombe la Ulaya au ligi za Uingereza, Italia, n.k. wakaacha kushabikia timu fulani. Ni kazi ngumu mno, hasa kama sababu yenyewe ya kuacha kushabikia timu hizo ni kuwa hizo timu sio za Tanzania. Sababu pekee ni kama timu hizo hazina viwango vya juu vya soka, hapo itakuwa rahisi kujizuia. Lakini kama timu zenyewe zinacheza soka la dunia nyingine kabisa ukilinganisha na timu zetu…hutazuia mtu kujichagulia timu kama alivyofanya Msangi.

  Je timu yangu ipi? Mimi timu yangu sio ya soka…bado ninaishabikia JKT Buhemba!

 • 8. MK  |  April 3, 2006 at 2:16 pm

  Samahani ingawa haya siyo maneno yanayo endana na kichwa cha habari lakini naomba nitoe tangazo langu kuhusu blog.

  TANGAZO:

  Baada ya uchunguzi wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog).

  Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

  Jawabu la hili swali unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa.

  Kama ukipata tatizo au maswali zaidi naomba niandikie na nitakujibu asap.

  Nashukuru,
  ©2006 MK

  Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

 • 9. mwandani  |  April 3, 2006 at 2:32 pm

  tatizo jingine inakuwa vigumu sana au haiwezekani kabisa kuangalia mechi za mpira wa Tanzania kwenye televisheni hapa ninapoishi. Listi ya Simba Sports siijui tangu wakati nambari moja mambosasa, mbili daud salum tatu…
  ni rahisi kuona mpira kwenye televisheni na kushabikia, kutathmini uchezaji wa timu na wachezaji.
  kama Bongo wangekuwa wanarusha filamu za mechi kwenye televisheni bila ya shaka ningefuatilia kwa karibu, ningeweza kuwajua wacheza, ningeweza kununua fulana zenye namba zao, picha zao nk.
  Vile sina hakika na uoneshaji wa mechi za mpira wa timu za Tanzania pale nyumbani siwezi kuwasemea walioko pale.

 • 10. Beka - Tanga  |  April 6, 2006 at 3:41 pm

  THE GUNNERS NEVER OUT GUNNED

 • 11. Martha Mtangoo  |  April 7, 2006 at 11:34 am

  Hivi Wee MK unatulazimisha tupende timu za Tanzania wakati zimejaa maloloso kibao, sasa we uliona wapi viongozi wa klabu wanatishia kugoma eti kwa sababu ya Mgao wa pesa? utakuwa unahamu tu ya kushabikia Simba na Yanga za Bongo ambazo zinaganga njaa? we acha bwana mambo mengine yatia kichefuchefu, Kwani Kaka Rama ina maana ulikuwa hujui kama Arsenal ni Bingwa Msimu huu? kaa mkao wa kusubiri Kombe hilo!!!!!!!!!!!!

 • 12. Martha Mtangoo  |  April 7, 2006 at 11:39 am

  Aaaah MK sAMAHANI UNAJUA HUYU MTU AMBAYE HAJULIKANI KANINTIA HASIRA MPAKA MWISHO YANI SAHAMANI SANA KWA KUTUMIA JINA LAKO PASIPO RUKSA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 34,350 hits
March 2006
M T W T F S S
« Feb   Apr »
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031