Archive for March 29, 2006

Kwanza Tujipongeze

Hii ni mahususi kwa mashabiki wenzangu wote wa Arsenal kokote kule waliko duniani. Kwa hakika ulikuwa usiku wa aina yake, kumkaribisha tena aliyekuwa nahodha na shujaa wetu kwa misimu tisa mfululizo hadi msimu uliopita, Patrick Vieira, lakini pia kuonyesha kile ambacho kocha wa Vijana hao wa Kaskazini mwa London, Arsene Wenger, amekuwa akikizungumza siku zote kuwa kulikuwa na umuhimu wa kuvipa vipaji vyake nafasi ya kuonyesha makali yao.

Hakika ulikuwa usiku wa aina yake kwa kijana chipukizi Cesc Fabregas, ambaye aliweka kando umri wake na kuweza kuliongoza vyema jahazi la Wapiga Bunduki wa London, kuibuka na ushindi mnono wa bao 2-0 dhidi ya Juventus (Bibi Kizee wa) Turin , katika pambano la kwanza baina ya mawili yatakayowakutanisha katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa bara la Ulaya.

Shukrani za kipekee pia zinastahili kumwendea beki mwafrika kutoka Ivory Coast, Kolo Toure, kwa kazi nzuri aliyoifanya, sanjari na wachezaji wote wa klabu hiyo. Hata hivyo, mapambano bado yanaendelea…….

March 29, 2006 at 2:36 pm 12 comments


Blog Stats

  • 35,058 hits
March 2006
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031