Blog Tanzania….blog.co.tz….na Ndoto za Mike za kila Mwandishi kuwa na Blogi yake

January 19, 2006 at 12:16 pm 4 comments

Bilashaka huu utakuwa ujumbe wa kufurahisha sana kwa wana-Blogi wa Kitanzania, na hususan wale ambao kwa muda sasa tumekuwa katika mchakato wa kutaka kuziunganisha Blogi zote za Kiswahili, (mradi ambao ulianzishwa na kufuatiliwa pamoja na kutiliwa uzito wa kipekee na ndugu yetu Maitha Kaihaso) sanjari na kusaka neno muafaka la kiswahili kwa ajili ya neno la Blogi, tunalotumia sasa, mradi ambao kama sikosei, aliuanzisha Da Mija.

Kwa wale ambao wale ambao walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu sana kampeni za Tanzania wakati ule, nadhani watakuwa waliwahi kulisikia jina la MIKE MUSHI. Huyu, alikuwa kijana wa Kitanzania ambaye alionyesha kipaji cha aina yake baada ya kutengeneza tovuti ambayo ilikuja kumsaidia sana Rais wa Tanzania wa sasa, Bw. Kikwete, kuingia madarakani. (Ingawa wenyewe wanaweza kukataa sasa hivi).

Baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza tovuti ile ya kampeni iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Kikwete Shein.com, kisha akatengeneza ya Kijana Mike, amekuja na wazo jipya. Amekuja na BLOG TANZANIA ama blog.co.tz. Awali taarifa kuhusu Blog.co.tz, nilizipata kupitia ujumbe ambao Mike alikuwa amenitumia, na sijui aliwatumia ‘ma-Bloga’ wangapi, ila kwa wale ambao hawakubahatika kuupata wanaweza kuusoma hapa.

Kisha nikafanya naye mazungumzo kupitia “yahoo chat” kwa mara mbili hivi, Soma mazungumzo ya mara ya kwanza kuhusu Blog.co.tz hapa, kisha soma mazungumzo ya awamu ya pili kuhusu suala hilo hapa. Na baada ya hapo, nadhani kama mwenyewe alivyopenda, nikaona ni wakati muafaka kuwaeleza wale wote ambao hawakuupata ujumbe huu, na ambao wanataka kujua ndoto za Mike, za kutaka kila mwandishi Mtanzania kuwa na Blogi yake.

Nisisahau, pia kuwa, Mike, ametaka kuwasiliana kwa ukaribu sana na Bw. Macha (Ndesanjo), Boniface ( Makene kama sikosei), na Wana-Blogi wote wa Kiswahili kokote waliko. Na naamini kabisa BLOG TANZANIA….blog.co.tz, ni ukurasa mpya kwa ajili ya kuendeleza pale tulipokuwa tunahitaji kupaendeleza.

HONGERA MIKE, INGAWA NDOTO ZAKO ZAWEZA CHUKUA MUDA KUTIMIA

Entry filed under: maskani.

Kikwete…Lowassa…Wana-Mtandao Ndugu zangu Wapendwa…

4 Comments Add your own

 • 1. Mike Mushi  |  January 19, 2006 at 5:20 pm

  Kwanza kabisa napenda kumshukuru mwana msangi kwa ushauri mkubwa aliokuwa ananipa.. kwa kweli kwa hilo sikutegemea..

  mimi nilitokea kumpenda ndesanjo nilipokuwa nasoma makala zake katika gazeti la mwananchi… baada ya kuwa nasoma.. kila siku naona link ya blog yake chini ya makala hiyo… siku moja nikasema ngoja nifungue niangalie kuna nini..

  basi kwanzia hapo ndipo nlipoanza kupenda blog. na ndipo hapo nilipoanza kufanya kazi yangu ya kutengeneza blog.co.tz ilikuwa mwaka jana mwezi june..

  Mwezi january mwaka huu nikawa nimesha kamilisha hiyo project nikasema ngoja nitumie baadhi ya wana blog ninao ona blog zao nione watapokeaje..

  Kweli nilipata email ya kwanza baada ya lisa limoja toka kwa Boniface Makenene.. kisha Msangi akanitumie.. nikawa nimefurahi tukaongea sana tuu.. akanipa ushauri nini chakufanya vile vyote alivyo niambie nipo njia kuvyitekeleza vyote kwa kweli..

  Nashukuru sana Bw. Msangi.

 • 2. Boniphace Makene  |  January 19, 2006 at 11:25 pm

  Msangi nimefarijika sana maana nilibanwa na masuala ya Teknolojia hapa na ratiba. Hili ni suala la muhimu nadhani sasa tuongeze nguvu ya kuwasiliana tunagalie namna ya kuwezesha watu wengi zaidi kupata blogu zao. Vipi kuhusu suala la kuwatafuta wanafunzi wa vyuo vya juu nina wazo hilo nikifika Tanzania kuwatafuta lakini kwa sasa tuongeze bidii kwa rafiki zetu na wote tunaowaelewa.

  Mike nitakuandikia muda si mrefu. Nilipata mail yako na bado sijaingia kubadili temperate yangu ili kuongeza viunganishi.

 • 3. Reginald S. Miruko  |  February 16, 2006 at 9:34 am

  umepotea sana

 • 4. mark msaki  |  March 5, 2006 at 12:54 pm

  kina mushi wanajitahidi sana. niliwahi lakini kujaribu kulog siku moja nikakwama mahala. lakini nitaweza tu siku moja…tatizo langu huwaga ni muda!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
January 2006
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031