Archive for January 19, 2006

Blog Tanzania….blog.co.tz….na Ndoto za Mike za kila Mwandishi kuwa na Blogi yake

Bilashaka huu utakuwa ujumbe wa kufurahisha sana kwa wana-Blogi wa Kitanzania, na hususan wale ambao kwa muda sasa tumekuwa katika mchakato wa kutaka kuziunganisha Blogi zote za Kiswahili, (mradi ambao ulianzishwa na kufuatiliwa pamoja na kutiliwa uzito wa kipekee na ndugu yetu Maitha Kaihaso) sanjari na kusaka neno muafaka la kiswahili kwa ajili ya neno la Blogi, tunalotumia sasa, mradi ambao kama sikosei, aliuanzisha Da Mija.

Kwa wale ambao wale ambao walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu sana kampeni za Tanzania wakati ule, nadhani watakuwa waliwahi kulisikia jina la MIKE MUSHI. Huyu, alikuwa kijana wa Kitanzania ambaye alionyesha kipaji cha aina yake baada ya kutengeneza tovuti ambayo ilikuja kumsaidia sana Rais wa Tanzania wa sasa, Bw. Kikwete, kuingia madarakani. (Ingawa wenyewe wanaweza kukataa sasa hivi).

Baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza tovuti ile ya kampeni iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Kikwete Shein.com, kisha akatengeneza ya Kijana Mike, amekuja na wazo jipya. Amekuja na BLOG TANZANIA ama blog.co.tz. Awali taarifa kuhusu Blog.co.tz, nilizipata kupitia ujumbe ambao Mike alikuwa amenitumia, na sijui aliwatumia ‘ma-Bloga’ wangapi, ila kwa wale ambao hawakubahatika kuupata wanaweza kuusoma hapa.

Kisha nikafanya naye mazungumzo kupitia “yahoo chat” kwa mara mbili hivi, Soma mazungumzo ya mara ya kwanza kuhusu Blog.co.tz hapa, kisha soma mazungumzo ya awamu ya pili kuhusu suala hilo hapa. Na baada ya hapo, nadhani kama mwenyewe alivyopenda, nikaona ni wakati muafaka kuwaeleza wale wote ambao hawakuupata ujumbe huu, na ambao wanataka kujua ndoto za Mike, za kutaka kila mwandishi Mtanzania kuwa na Blogi yake.

Nisisahau, pia kuwa, Mike, ametaka kuwasiliana kwa ukaribu sana na Bw. Macha (Ndesanjo), Boniface ( Makene kama sikosei), na Wana-Blogi wote wa Kiswahili kokote waliko. Na naamini kabisa BLOG TANZANIA….blog.co.tz, ni ukurasa mpya kwa ajili ya kuendeleza pale tulipokuwa tunahitaji kupaendeleza.

HONGERA MIKE, INGAWA NDOTO ZAKO ZAWEZA CHUKUA MUDA KUTIMIA

January 19, 2006 at 12:16 pm 4 comments


Blog Stats

  • 35,058 hits
January 2006
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031