Archive for December 17, 2005

Hureeeeeeeeee!!

SISHANGILII kwasababu ya kushindwa au kuwashinda, laa, bali kwasababu biashara yangu ilichanganya kwa kiasi cha kutosha sana tu. Lakini kwakuwa msimu wake umeisha, nimeona nibadilishe biashara yangu, na sasa nitaanza biashara yaaaaa…….!!! Ah ngoja kwanza nimalize kuisajili maana jamaa wasije wakanijia juu. Lakini nikiwadokeza tu itakuwa ni biashara ambayo inawahusu jamaa zangu waliofanikiwa kupata tiketi za kwenda kule kwenye lile jumba la duara Dodoma kwa ajili ya kutuwakilisha katika kuongeza viraka kwenye katiba yetu.

Kama kuna biashara ambayo unaweza kunishauri nikaifanye…nzuri zaidi ya niwazayo, au bidhaa ambazo naweza kuongeza kwenye zile nilizokuwa nazo…….karibu sana unidokezee.

December 17, 2005 at 5:37 pm 4 comments


Blog Stats

  • 35,058 hits
December 2005
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031