…na sasa ni siku ya Wayahudi, ya waafrika wenye njaa ni lini?

November 2, 2005 at 6:31 pm 4 comments

Wakati fulani fulani huwa navunja utamaduni wetu sisi Watanzania, ule utamaduni ambao umekuwa ukihanikizwa sana na watu kuwa Watanzania hatupendi Kusoma (kujisomea?) na katika moja ya nyakati ambazo nilipokuwa natekeleza kuvunja utamaduni huu, nilipokuwa napitia taarifa ya Umoja wa Mataifa nilivutiwa sana na taarifa moja aliyoitoa Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bw. Koffi Annan, kuhusiana na Bara la Afrika.

Katika chapishi lake moja ambalo aliwahi kulitoa, katibu huyo alisema kuwa AFRIKA HAIWEZI KUWA HURU AU KUENDELEA IKIWA NA NJAA. Lakini cha ajabu hawa jamaa hawakuamua hata kuweka siku ya kutokomeza hiyo njaa inayolikabili Bara la Afrika, na badala yake nikakutana tena na chapisho jingine la Umoja huo eti Umoja huo umeamua kuwa Januari 27 ya kila mwaka, sasa itakuwa Siku ya Wayahudi, kuwakumbuka maelfu ya Wayahudi walioteketezwa enzi hizo za utawala wa jamaa mmoja ambaye alidhani kuwa Dunia yote inaweza kuwa mikononi mwake.

Je Waafrika tulio na njaa na bara letu, tuna umuhimu wa kuwa na siku kama hii kweli?

Entry filed under: maskani.

Unaijua TUKALEWAPI.Com….? Suala la Zanzibar…TUZUNGUMZE tuache KUSEMA

4 Comments Add your own

 • 1. Anonymous  |  November 2, 2005 at 7:01 pm

  Blog is good. Dont’t stop. No better time than now to stop on this website about scommesse sportive . You’ll find only scommesse sportive

 • 2. mwandani  |  November 3, 2005 at 1:01 pm

  Waafirika waliokufa kwa mamilioni utumwani na wakati wa ukoloni hawana siku… Hapa Australia Maaborijino waliouwawa na kufanyishiwa hawana siku…
  Mapalestina hawana siku… hakuna mwengine anayeombwa samahani wala kupewa siku zaidi ya hao mabwana

 • 3. Hamad Rashid  |  November 3, 2005 at 4:59 pm

  ni jukumu la vyombo vya habari na hasa ninyi msiokuwa na mipaka kulivalia njuga hili suala sasa…inawezekana kabisa kuwa huu ndio wakati wake wa kulikomesha au nyinyi ndio mkawa wa kulipigia kelele…kazeni buti

 • 4. BABUU,  |  November 6, 2005 at 12:46 pm

  sawa babuu,hilo linaeleweka hatakama kwetu tunatakiwa kuwa na hiyo siku bado kuna watu watajitahidi kwa nguvu zao zote au kupitia kwa watu wao ambao wanajipanga kwa kila jambo ili wawe wapishi wa siku hiyo nahatimae kuchukua mafuta yakupikia mchele na mazagazaga kibao kisha kuludisha katika imaya zao na watu wangine kubaki na njaa zao au kuambalua kula vyakula chukuchuku hatimaye kupata magonjwa ya tokanayo kula vyakula visivyo na plotini mwilini watru hawa hawaliziki niwalafi hata ukiwalundikia majumbani kwao kwani hawajui kuwa wataviacha hapahapa duniani tu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
November 2005
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930