Siku ya Wambeya Duniani

October 26, 2005 at 4:07 pm 6 comments

Kaka yangu mmoja wanamuita Chesi Mpilipili, katika moja ya kazi zake za hivi karibuni alizozifanya wakati wa maadhimisho ya SIKU YAKE, ambayo kwa kawaida huadhimiswa kila Jumapili kwenye ukumbi wa Majira, aliniacha hoi alipoelezea kushangazwa kwake na huu utitiri wa SIKU, hamaanishi kuwa zimeongezeka katika kuunda wiki, mwezi au mwaka, bali anamaanisha hizi SIKU za kuadhimisha matukio fulani fulani.

Anasema yeye enzi zake wakati anakua kulikuwa na SIKU chache sana, anasema mbili tatu hivi, zikizidi sana ni tano na ambazo zilikuwa zikihanikizwa kwenye vyombo vya habari kiasi kwamba haikuwa taabu hata kujulikana kwake. Enzi hizo, anasema kuwa ilikuwa jambo la kawaida sana kusikia vyombo vya habari vikihanikiza “Wiki ijayo kutakuwa na maadhimisho ya SIKU Fulani na mwezi ujao ni maadhimisho ya SIKU Fulani. Na anasema zilikuwa chache sana kiasi kwamba si ajabu ilikuwa rahisi sana kwa mtu kuweza kuweka kwenye kumbukumbu za ubongo wake kuwa mwaka una SIKU ngapi.

Lakini sasa…. imekuwa nongwa, sio tu kuwa vyombo vya habari vimeamua kuzichunia hizo SIKU, bali pia nazo zimekuwa nyingi mno kiasi kwamba inakuwa vigumu sana hata kuweza kuzijua na zingine anahisi zinabuniwa tu na baadhi ya watu wakilala na wake zao majumbani mwao wakishauriana kuwa kesho iwe SIKU YA KULA PIZZA, basi itakuwa na kesho yake mtu ukiamka utasikia (kupitia mabalozi wao, wakiongea na waandishi wa habari pale jijini Dar), kuwa Leo ni maadhimisho ya SIKU ya ula Pizza Ulimwenguni, na hata Wabongo wataadhimisha siku hiyo ingawa wanazisoma kwenye matangazo au kuziona kwenye picha za kihindi.

Ndio, kwani hujui kuwa kuna SIKU za Kutoana Ngeu, Siku za Wanaovaa Magauni, Siku za Walalahoi (?) Siku za Watembea peku, Siku za Kadhaa na Kadhaa. na kwa Ushauri wa kakangu Chesi mwenye nywele za Kipilipili, anaona ni aheri basi Wadanganyika nao wakapendelewa na hao Watunga siku wakapewa vijisiku kadhaa hizi kama SIKU ya Hafla za Jikoni (Kitchen Party?), Siku ya Kufumuana Magumi (Boxing Day?), Siku ya Unyago, Siku ya Kusasambua, Siku za Miduara, Siku ya Ndoa za Mkeka, Siku ya Kufukuzana (Sendoff?), Siku ya Waezekaji (Wawekezaji?), Siku ya nanihii…..na Siku ya nahinii pia.

Na hizo bado ni chache sana kwa maana hujagusa Siku ya Wanaodaiwa na ile ya Wadai, hujazungumzia kabisa Siku ya Mvua na ile ya Kiangazi, na wala hujazungumzia Siku ya Wambeya kule Uswahilini na ile ya Wastaarabu kule Uzunguni na zingine nyingi ambazo hata wewe unazijua.

Hakika bilashaka naamini kwa Utitiri huu wa SIKU, utafika wakati tutakuwa na SIKU ya Ndesanjo, SIKU ya Reginald na hata SIKU YA SIKU ZOTE au SIKU YA KILA SIKU…..

Alamsiki ngoja nami niwahi nyumbani maana leo ni SIKU YANGU !!

Entry filed under: maskani.

Mbona Uchaguzi wetu mnaufanyia Uchafuzi? Ama hakika huku nini Kufa Kufaana

6 Comments Add your own

 • 1. Anonymous  |  October 26, 2005 at 4:54 pm

  I was just browsing and found your blog. Very Nice! I
  have a candle kit making site. You can find everything about candle kit making as well as candle supplies, gel candles, jar candles, and how to make your own candles. You’ll find it very informative. Please visit, check it out and enjoy!
  Rod

 • 2. Ndesanjo Macha  |  October 27, 2005 at 6:34 am

  Na pia siku ya “Yahaya, mpe huyo…”
  Siku hii mnaijua?

 • 3. Husna Ally  |  October 27, 2005 at 7:34 am

  @ Ndesanjo
  Siku ya Yahaya? ndio ipi nayo hiyo tena wajameni? kweli hizi siku zimekuwa nyingi mpaka zinakifu sasa,

 • 4. Husna Ally  |  October 27, 2005 at 7:40 am

  @ Msangi:
  Hivi huwa hivi vituko unavikusanyia wapi kaka Msangi, napenda jinsi unavyojenga hoja zako….some times zinaweza kuonekana za kijinga kijinga lakini kimsingi zina mantiki ndani yake na ni challange kwa watu kujifunza

 • 5. Boniphace Makene  |  October 27, 2005 at 11:04 pm

  Hey men maana kila siku kuiga iga. Hadi noma, mimi nimezaliwa sina habari ya Birthday lakini mwanangu hapa mademu wa kujichonga wa Bongo sasa asipopewa zawadi ya birthday jua mapenzi yameshakufa! Ooh come on Msangi! Sijui vipi tu

 • 6. Anonymous  |  October 28, 2005 at 7:44 am

  hata katuni watu huwa wanazichora ili kuelimisha kaka……kazi nzuri sana nimeipenda na nimeifurahia hakika inachekesha lakini tutafakari kweli ikiwa sisi kama Watanzania, je kuna haja ya kuwa na siku zote hizi? Kama ni kuwa nazo basi nasi tuwe na siku za kikwetu kwetu…Siku ya Azimio la Arusha kama sio Azimio lililoshindwa…Siku ya Ujamaa na Kujitegemea na zingine kama hizi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
October 2005
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31