Mkapa; Hivi huku sio kujitega wenyewe?

October 13, 2005 at 2:34 pm 7 comments


Niko hapa kwenye kompyuta yangu, nikiwa nasikiliza muziki mmojawapo kati ya hii mingi tuliyonayo hapa nchini inayoitwa ya kizazi kipya. Hapa nasikiliza wimbo wa ‘SIWAELEWI’ ulioimbwa na marehemu Vivian Tillya (Mungu amlaze mahali pema peponi) enzi za uhai wake.

Nawakumbuka pia hawa jamaa zetu ‘Wanasi-hasa’, ambao baadhi yao mishipa yao ya shingoni inakaribia kupasuka, kila mmoja akijitahidi kuhanikiza uongo na uwezo wake alionao (hivi sasa lakini) wa kuweza kuondoa matatizo ya “Wadanganyika” katika muda mfupi sana tu, kila mmoja kwa staili ya aina yake.

Wengine wana ile staili ya majiko ya kizamani ya mafiga matatu; “Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya,” japo sijui ni ya kuelekea wapi maana kukimbia sio lazima iwe kwenda mbele tu.
Wapi pia wanaotumia staili ambazo hazitofautiani sana na zile za ‘Vidume’ vyetu vya pale TMK; “Hakuna kulala Mpaka kieleweke” nadhani kweli hawawezi kulala maana walilala miaka yote mitano iliyopita unadhani watashindwa kukesha siku 70 za kuhanikiza usanii wao majukwaani?

Lakini wakati jamaa hao wakiendelea huko, kwa upande mwingine kaka yetu Ben, ambaye amejijengea umaarufu wa aina yake duniani kwa sera zake za kutaka “Kuupiga teke Ukapa uliokithiri miongoni mwa Wadanganyika” yeye anaendelea na yake huku. Anaendelea kusaka wadau wa kuhakikisha sera yake hiyo inatekelezeka kwa “Uwazi na Ukweli” na hivi karibuni eti aliteketeza milioni 100 hivi za Kibongo kumnunulia Papa Benedicto wa 16, vinyago kadhaa vya kutokea ukanda wa Lupaso na kumpelekea kule kwenye maskani yake Vatican.
Wapo wapinzani wake ambao wameshaanza kuchonga kuhusu hili lakini hawa bilashaka hawajui kuwa huu ni aina ya ukarimu ambao unatumika kwa ajili ya kumvutia Papa ili naye siku moja afikirie kuja “Kuezeka”… naambiwa ni “Kuwekeza” kumbe…hapa hapa Bongo (potelea mbali hata kama uwekezaji wenyewe utakuwa wa kiroho tu), ili “Wadanganyik”a wapate nafasi ya kujiajiri.
Wakati hayo yakiendelea, nakumbuka pia kuwa kuna hawa jamaa zetu wapatao 600, ambao kimsingi wanawakilisha wenzao karibu au zaidi kidogo ya milioni 2 kote nchini, ambao kwa bahati mbaya sana walipitiwa na hili Pepo linaloitwa Ukimwi, ambao wamesema kuwa Nnjuluku, mshiko au Ngawira” zao zilizotolewa na “Sirikali” zisipowafikia hadi mwishoni mwa Novemba ya mwaka huu, watatuonyesha kwa kiasi gani walivyo wakarimu kwa kuanza kutugawia bure bure virusi vyao licha ya uchoyo wetu kwa fedha zetu.
Unashangaa? Ndio hali ilivyo hivyo. Kaka Ben anateketeza milioni 100 kutafuta wawekezaji ambao watakuja kufanya kazi kwa nchi ambayo wananchi wake wamegawiana virusi bila hiayana tena kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya. Tena basi hawa jamaa wamepania kuonyesha ukarimu wao kwa utaratibu wa Hakuna Kulala hadi Kieleweke. Je huku sio ndio KUJITEGEA mabomu sisi wenyewe lakini?
oohhh Dada yangu Vivian, kaka yako huku baaado SIWAELEWI Wadanganyika

Entry filed under: maskani.

Eti unasemaje? Mashujaa daima Hawafi – 2Pac Shakur

7 Comments Add your own

 • 1. Anonymous  |  October 14, 2005 at 2:18 pm

  Kaka! hivi hawa wenye virusi walivyotishia kutuambukiza , watafanya kweli? Itabidi tupanue maana ya neno ugaidi. Vitisho vikubwa. Makala yako maridadi sana.

  Tunga

 • 2. Richard  |  October 14, 2005 at 2:32 pm

  Kama nyie mnafanya kweli kwanini wao wasifanye kweli? Hivi milioni 100 alizotumia Mkapa zingeweza kuwaokoa wangapi kama kweli idadi yao ni au zaidi kidogo ya milioni 2? Yaani kaaaazi kweli kweli

 • 3. Jacqie  |  October 14, 2005 at 2:34 pm

  Ni kwasababu yu kwenye msafara wa Mamba, Kenge na mijusi wakubwa wakubwa watakuwemo tu lakini hakika mimi nawaambia watekeleze azma yao. Huo ni utani wa wazi wazi ati.

  Kaka msangi naomba mail yako

 • 4. Msangi RS  |  October 14, 2005 at 2:37 pm

  @Jacqie:
  Nashukuru kwa maoni yako lakini mbona umekuwa vuguvugu sana? Kuwa wa moto kabisa au wa baridi, sasa wewe utakuwa kwenye kundi la Kenge au mijusi wakubwa huh!! Anwani yangu inapatikana kwenye blogi juu ya picha yangu

 • 5. msangirs  |  October 14, 2005 at 2:40 pm

  @Richard.
  Nadhani ni vyema nikakushukuru sana kwa kuwa msomaji wangu na mchangiaji wa mada hii, ila nakuomba kitu kimoja ndugu yangu, kutumia maneno ya moja kwa moja kwa mchangiaji mwenzako nadhani sio nzuri sana. Mfano ungeweza kabisa kutumia neno Wanafanya kweli badala ya Mnafanya kweli
  Tuko pamoja daima

 • 6. Indya Nkya  |  October 14, 2005 at 9:30 pm

  Milioni 100 vinyago? ni vya kimakonde au vya wapi? nadhani wauza vinyago matatizo yao yameisha hakiamungu

 • 7. Ramadhani Msangi  |  October 15, 2005 at 12:13 pm

  @Idya nkya:
  thubutuuu!! matatizo yataisha wapi? Tena sio ajabu kuwa wao wamembulia kiasi kisichofika hata 10,000 za kibongo. Bajeti hiyo kwa mujibu wa watoa habari hiyo ilijumuisha kurusha ndege yake ya bilioni ngapi vile sijui! naona hata uvivu kutamka

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
October 2005
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31