Eti unasemaje?

October 4, 2005 at 6:45 pm 11 comments

Nina mlolongo mkubwa sana wa watu wa kuwashukuru hadi hivi sasa, ingawa kwa hakika bado safari yangu ndio kwaaaanza inaanza, lakini haidhuru kwa wale ambao wameniwezesha kufikia kituo cha basi ni haki yao kupata pongezi zangu za dhati.

Naandika maandishi haya nikiwa niko mkoani Mbeya na hususan Mbeya mjini, baada ya kupata uhamisho wa kikazi, ulionitenganisha na mji niliokuwa nimeuzoea sana na kuupenda mno licha ya kuwa kila dakika hata nyakati za mvua sio ajabu kukuta vumbi likitimuka, nazungumzia Dodoma.

Naam, niko Mbeya, katika mkoa ambao siku kadhaa zilizopita sikumbuki ni ngapi maana sikjuwahi kuwa na urafiki wa karibu na mahesabu, uliwahi kuwa gumzo kutokana na biashara ya kuchuchunana ngozi baina ya hawa hawa Wana wa Adamu, Astakafirulahi laadhimu.

Kwa hakika ni kamji ambako bilashaka kamekuwa na maendeleo makubwa sana kiasi cha kustahiki kuitwa jiji, na bilashaka ndio maana hata hiyo biashara ikatoweka kimya kimya japo naambiwa kuwa bado ipo maana majasiri huwa hawaachi asili ati.

Ni mji ambao maisha kwa ujumla sio ya gharama sana kama nilikokuwa nimetoka, kwa maana shughuli mbalimbali zinaendelea hapa ziwe za kilimo, biashara na zinginezo nyiingi sana. Unaweza kupata kila kitu hapa Mbeya ikiwa tu utaweza kuendana haraka sana na wakazi wa mji huu ambao bado wanakasumba fulani ya kaukabila. Lakini ukiwajulia tu, wewe aahhh maisha murua kabisa.

Nikiwa bado najipanga namna ya kutoka nikiwa makazi mapya, nadhani niwakaribishe saaaaaana Mbeya.

Entry filed under: maskani.

Endeleeni kupiga mayowe, Ipo siku mtasikika Mkapa; Hivi huku sio kujitega wenyewe?

11 Comments Add your own

 • 1. Mija Shija Sayi  |  October 6, 2005 at 11:10 pm

  Asante, tumekwisha karibia.

 • 2. Jamila (tga)  |  October 7, 2005 at 2:59 pm

  Hakika ni miaka zaidi ya arobaini sasa toka uhuru upatikane na hakuna matunda yoyote tulopata. kweli haya ni matundu ya uhuru, bora mkoloni angekuwepo tu

 • 3. jackson  |  October 7, 2005 at 3:01 pm

  Awali tuliambiwa tufunge mikanda na hadi sasa hatujaambiwa kufungua, lakini maisha ndio yanazidi kuwa ya shida sana, kweli kaka haya ni matundu tena naamini ni makubwa kweli kweli ya uhuru

 • 4. Musisi  |  October 7, 2005 at 3:03 pm

  aisee hii kali kaka, hivi huwa unawaza nini hasa, ulianza na jamaa waliokunywa uji wa mgonjwa, ukasema kuku ni kuku tu, sasa umekuja na matundu ya uhuru, duh mshkaji hivyo vijimaneno vyako mwisho. Bug ups kamanda

 • 5. Anonymous  |  October 7, 2005 at 3:04 pm

  Kaa mkao wa hasara ndugu yangu, nchi hii imeshaposwa hata upige kelele vipi ni kama wamefunga masikio yao, si unaona ndio maana sasa wamefikia hatua ya kuwabonda nyie waandishi. Shauri yako Mapuri asije akakutoa baruti huku mtandaoni. Kaza uzi ndugu

 • 6. Hemed  |  October 7, 2005 at 3:06 pm

  mmmmh Meya, kutoka Dom, mbona mabadiliko makubwa sana ndugu, nilidhani walau utakimbilia Dar hivi wewe umekimbilia Mbeya, huo ndio uzalendo haswa sio kukimbilia mijini kila kukicha

 • 7. Rehema  |  October 7, 2005 at 3:08 pm

  Angalia sana hawakawii kugeuza wenzao malighafi hao wakakuchuna ngozi shauri yako.

 • 8. mheshimiwa mbunge kijana  |  October 7, 2005 at 3:10 pm

  Kuna mikumbo ya ghasia humo humo ndani, kuna kila aina ya fujo lakini si ndio tunavyoishi watanzania kwa kudanganywa kuwa tunaendelea maana tumeshindwa kureact ati, tutaambulia matundu kweli kweli

 • 9. Mwakyesa D  |  October 7, 2005 at 3:14 pm

  Ukutifiki??? namaanisha unasemaje hapo kwa kinyakyusa, karibu sana mbeya ipo siku nitakutafuta hadi nikuone maana nimekuwa msomaji wako tu kwa muda mrefu sasa

 • 10. Jeff Msangi  |  October 8, 2005 at 1:34 am

  Kaka,habari za Mbeya.Hukutaka kutuambia mapema ili tuje tukusaidie kupakiza mizigo lakini taarifa yako hii naichukulia kwamba ndio rasmi juu ya makazi yako mapya.Kila la kheri mkoani Mbeya.

 • 11. kivale  |  October 10, 2005 at 9:05 pm

  sisi kwa sisi wangine mafisi hivyo ndivyo unachotakiwakujua katika maisha yako nimishakweleza machache juu ya safari yako kuwa ndio kwaaanza imeanza hivyo kaza buti Babuuu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
October 2005
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31