Archive for October 4, 2005

Eti unasemaje?

Nina mlolongo mkubwa sana wa watu wa kuwashukuru hadi hivi sasa, ingawa kwa hakika bado safari yangu ndio kwaaaanza inaanza, lakini haidhuru kwa wale ambao wameniwezesha kufikia kituo cha basi ni haki yao kupata pongezi zangu za dhati.

Naandika maandishi haya nikiwa niko mkoani Mbeya na hususan Mbeya mjini, baada ya kupata uhamisho wa kikazi, ulionitenganisha na mji niliokuwa nimeuzoea sana na kuupenda mno licha ya kuwa kila dakika hata nyakati za mvua sio ajabu kukuta vumbi likitimuka, nazungumzia Dodoma.

Naam, niko Mbeya, katika mkoa ambao siku kadhaa zilizopita sikumbuki ni ngapi maana sikjuwahi kuwa na urafiki wa karibu na mahesabu, uliwahi kuwa gumzo kutokana na biashara ya kuchuchunana ngozi baina ya hawa hawa Wana wa Adamu, Astakafirulahi laadhimu.

Kwa hakika ni kamji ambako bilashaka kamekuwa na maendeleo makubwa sana kiasi cha kustahiki kuitwa jiji, na bilashaka ndio maana hata hiyo biashara ikatoweka kimya kimya japo naambiwa kuwa bado ipo maana majasiri huwa hawaachi asili ati.

Ni mji ambao maisha kwa ujumla sio ya gharama sana kama nilikokuwa nimetoka, kwa maana shughuli mbalimbali zinaendelea hapa ziwe za kilimo, biashara na zinginezo nyiingi sana. Unaweza kupata kila kitu hapa Mbeya ikiwa tu utaweza kuendana haraka sana na wakazi wa mji huu ambao bado wanakasumba fulani ya kaukabila. Lakini ukiwajulia tu, wewe aahhh maisha murua kabisa.

Nikiwa bado najipanga namna ya kutoka nikiwa makazi mapya, nadhani niwakaribishe saaaaaana Mbeya.

October 4, 2005 at 6:45 pm 11 comments


Blog Stats

  • 34,787 hits
October 2005
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31