Endeleeni kupiga mayowe, Ipo siku mtasikika
September 5, 2005 at 7:31 pm 1 comment
Kwa wale wapenzi wa muziki, bilashaka hizi ni taarifa nyeti sana kwao. Na hizi ni kuhusu lile tamasha kubwa la wasanii wa muziki wa kizazi kipya (japo na cha zamani kinaupenda), nchini, namaanisha tamasha la Tanzania Hip Hop Summit, ambalo kwa mwaka huu, waandaaji wake kwa makusudi kabisa naambiwa wameonelea lifanyike mwezi Oktoba, kusudi liweze kusambaza ujumbe wa uchaguzi wetu mkuu. Endeleeni kufuatilia maendeleo ya tamasha hili kupitia Webu hii.
Entry filed under: maskani.
1.
bakari juma | September 19, 2005 at 2:50 pm
hapo kaka kazi ni kubwa sana maana duh, watanzania tunavichwa vigumu sana sijui kama kuna mtu anaelewa somo, lakini kama ulivyowaambia waendelee kupiga tu kelele huenda wakasikika wao