Uigizaji wa Wabunge wetu na hatma ya Bunge lenyewe

August 21, 2005 at 10:58 am 6 comments

Nazungumzia Bunge letu tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo kwakweli hivi sasa kuna watu wamekuwa wakijitahidi kwa kadiri wawezavyo kuhakikisha kuwa wanaufuta utukufu wake na badala yake kulifanya sehemu ya kupotezea wakati. Na HII HAPA ni moja ya kazi nyingi sana ambazo ninatarajia kuwa wasomaji wangu watashirikiana nami katika kuibua hoja za msingi kabisa za kurekebisha baadhi ya mambo ambayo ni wazi kabisa yanaenda kombo.

Entry filed under: maskani.

Upele umewapata wenye kujua kukuna? Mbowe, Mlikuwa wapi wakati huo?

6 Comments Add your own

 • 1. Indya Nkya  |  August 22, 2005 at 7:17 pm

  Kama hakutakuwa na utaratibu wa kuwawajibisha hata kabla ya kumaliza hicho kipindi cha miaka mitano basi wataendelea kuigiza maisha yao yote ya ubunge.

 • 2. Husein Bakari  |  August 24, 2005 at 1:15 pm

  @Idya Nkya
  Wakuwawajibisha atakuwa nani ilhali wenyewe ndio wanaoweka mazingira ya kuwajibishwa au laa, sema kuwa kama wasipojali kilichowapeleka hapo, hakika ipo siku wataungana na Wadanganyika katika kilio chao. We waache tu waendelee kuchekelea hawajui sisi tukianza kucheka itakuwa kilio kwao

 • 3. Anonymous  |  August 24, 2005 at 1:18 pm

  Kurejesha utukufu uliokuwepo wa Bunge letu, utukufu ambao aliuanzisha hayati baba wa taifa itakuwa ngumu kiasi maana karibu wote walioko sasa katika chombo hicho sio watukufu wataurejesha vipi unadhani?, Hata wachache waliobado watukufu wanashindwa nguvu na waliopoteza uelekeo, Ibilisi daima ana nguvu bwana Msangi

 • 4. Egidio Ndabagoye  |  August 24, 2005 at 2:22 pm

  Kaka wewe tayarisha tumbo lako kwa pilau.Hawa watu mimi nimewachoka yaani midomo yao ina maneno matamu kama kasuku ukishawachagua enhe! wanakuja mijini kueneza magonjwa

 • 5. Indya Nkya  |  August 25, 2005 at 11:45 am

  Wa kuwawajibisha ni wapiga kura. Kwa hiyo wapiga kura inabidi wajue wajibu wao. Mpiga kura ni mimi na wewe. Tunatakiwa tuwaelimishe wapiga kura wengine pia. Kama mbunge ataonekana kutowatumikia waliompigia kura kama wanavyodai ndio kazi yao basi tuwaondoe kwa staili ya kuwafukuza na kuwakataa ikifanyika hivyo sheria zitarekebishika tuu

 • 6. Anonymous  |  August 27, 2005 at 1:01 pm

  Hakika nimefurahishwa sana na ndugu zangu hawa wawili Idya Nkya na Hussein Bakari na ningependa nami niwachangie yafuatayo:

  @ Idya:
  Huwa ni vigumu kuelewa kuwa kuna kazi gani katika kuielimisha jamii ikajua kuwa ndio inayohusika na inayoguswa moja kwa moja ukizungumzia serikali, Tuna utamaduni wa kuwa serikali ni dude fulani hivi ambalo likishakuwepo basi, hakuna wa kulinyooshea mkono, Kazi ipo jamani

  @ Hussein:
  Ndugu yangu, hivi unadhani uwezo unaopewa wa kuwachagua hao watu na kuwaweka hapo unaishia baada ya kuwachagua tu? Hivi ulishajaribu kuona kuwa unawawajibisha halafu ikashindikana?, Huu ndio wakati wa kubadilika, hata kama walikuwa hawataki kubadilika basi tunatakiwa, sisi sote tuwabadilishe sasa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 34,787 hits
August 2005
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031