Upele umewapata wenye kujua kukuna?

August 12, 2005 at 12:47 pm 3 comments

Kwa haraka haraka, wapo wale wenzangu na mimi ambao watakuwa wameshangazwa kama sio kushtushwa na matokeo haya, lakini ndio hivyo tena. Hayawi hayawi, hatimaye yamekua. Inawezekana kuwa yalikuwa Maajabu, kama yale ya mzee Rajabu ya kushangaa kababu akavikwa hijab, lakini ukweli utabakia palepale kuwa ndio waliopita na WENYE WIVU WAJINYONGE TU, ila wenzenu haoooooooooo, wanaingia Bungeni pale (sijui kwenda kusinzia sawa na wenzao au vipi, tuwaachie wenyewe hayo).

Kwa kutizama sifa zao tu, hakika wanastahili hicho walichokifikia. Nawazungumzia ndugu zangu hawa wawili ambao majuzi wamefanikiwa kuteuliwa kuwa wawakilishi wa vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nawazungumzia Amina Chifupa Mpakanjia na mwenzake (katika uwakilishi) Lucy Thomas Mayenga. Kwa kweli kama ni kutosha kura zilitosha, lakini je ndio upele umempata mwenye kucha kweli,au kucha zimempata mwenye upele???

Entry filed under: maskani.

Yaliyojiri kikao cha 1 cha Bunge la awamu ijayo!! Uigizaji wa Wabunge wetu na hatma ya Bunge lenyewe

3 Comments Add your own

 • 1. Anonymous  |  August 18, 2005 at 9:29 pm

  Eh bwana ee, Chifupa kashinda ila sina hakika kama ana uwezo kitaaluma unaoendana na dunia ya kileo.Kwa hiyo kama ni kusinzia nafikiri ndio walewale.
  Nafikiri ni tamaa ya pesa na ujiko ndio vilivyomshindisha bila shaka.Sina wivu ila kwa ninavyomjua nimemfuatilia ktk kazi yake ya utangazaji sikuwahi kumsikia akianda kipindi makini yaani issue nzito nzito kuhusu mustakabali wa nchi yetu.
  Tusubiri tumwone,ila ana kimbola cha kashfa asipoangalia kitamuandama zaidi sijui awape nini wanahabari wamstahi.

 • 2. Anonymous  |  August 18, 2005 at 11:11 pm

  Nadhani wengi hupendelea vitu ambavyo si makini ndi maana amekwaa umaarufu mkubwa namna hiyo hadi ubunge. Kwa usanii wa bunge letu kila mtu anaweza anyway!!

 • 3. Mihwela Mapembe  |  September 4, 2005 at 12:58 pm

  Ni kwela uyasemayo maan ndani ya kipindi cha uchaguzi tu Amina Chifupa wa Mpakanjia alilopoka nasema kulopoka maana pale si mahala pake kwa maneno kama kasheshe, alipoambiwa tu achague wa kumsimamia kura akasema kasheshe sasa kwa maoni yangu nashindwa kuelewa je huko bungeni itakuwaje? maana tabia haina dawa ingawa tunambiwa ameanza kujirekebisha lakini alikuwa wapi kujirekebisha tangu akiwa form two kwani inasemekana alifukuzwa shule kwa utovu wa nidhamu pale jangwani.

  Ila tumuachie spika kazi hiyo analo la kumrekebisha tabia binti yule na je vile vijisuruali vya kubana atavivalia wapi na je pochi yake ina sehemu ya kubebea vitabu vya maswali na majibu kama si atajaza vipodozi kama kwaida yake kaka tutaendelea kesho Tchao

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
August 2005
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031