Walahi Tunajenga dunia ndani ya Tanzania

August 9, 2005 at 1:42 pm 1 comment

Ungeliwaona ungewaonea huruma sana kwa jinsi walivyokuwa wakihangaika kila kukicha. Kulikuwa na vikao vya kila mara na kila mahali, kulikuwa na hujuma za kila aina, kulikuwa na ubabe wa hapa na pale, lakini kubwa zaidi ni kuwepo kwa matendo yaliyokithiri ya Rushwa.

Nazungumzia zoezi la kuwasaka “WAGOMBEA” <em>(na hakika waligombea) wa nafasi za ubunge kupitia CCM. Zoezi ambalo limedhihirisha wazi ni kwa kiasi gani ndani ya CCM yenyewe kulivyojaa Wanafiki, Waongo, Wasaliti na Mafisadi wa aina yake. Ndio najua kuwa wapo ambao wakisoma hapa wataanza kunitolea macho lakini sijali kusema ukweli.

Ni nani ambaye hakushuhudia umwagwaji wa fedha kwa wananchi ulivyokuwa ukifanywa na mabingwa hawa wa kupambana na Rushwa, ambaye kwamba anaweza kuniambia nisiwaite wanafiki na waongo waliopitiliza?

Ni nani ambaye hajui kuwa baadhi ya vigogo walitumika katika kuwapepelea njia baadhi ya waliokuwa wameshayakoroga ilimradi warejee tena katika nafasi zao kwa ajili ya kuendelea kutoa harufu zinazowachefua wananchi wao za uvundo wa mawazo, fikra na hata mitizamo?

Potelea mbali bwana, atakayethubutu kuninyooshea kidole aninyooshee tu na wala sitojali kwasababu baadhi ya matukio haya nimeyashuhudia kwa macho yangu, yakiwemo pia ya baadhi yao kuiba wapiga kura na kuwahamisha maeneo yao ili wenzao wasiwakute na kuwarubuni.

Lakini sasa wakati tukiendelea na hali hii kuna mambo ambayo kwahakika yanastahili kabisa kukaa vichwani mwetu kuwa, kinachojiri sasa ni kuunda Ulimwengu uliooza kwa kila aina ya uozo unaoweza kuujua wewe, humu humu ndani ya Tanzania hii.

Tunajenga tabaka la Wamarekani wetu, ambao watatumia mabavu na vijisenti vyao katika kutunyanyasa sisi akina yakhe wa ulimwengu wa tatu, ambao pia kimsingi tunaishi nao humuhumu ndani ya Bongo hii hii ya Wadanganyika. Astakafirulahi walahi.

Sijui ndio dalili za kukata tamaa, kutojua kile kitakachokuja mbeleni mwetu au nini lakini hakika tumejitia msambweni, kwa kuwa Tanzania inaelekea sasa kuwa na tabaka la Viongozi matajiri, watakaokuwa wakiongoza masikini wa kutupwa ambao kimsingi watageuka kuwa wakutumikishwa, kuburuzwa na …………, dah ngoja niishie hapa maana wajameni, hali ni mbaya

Tutaendelea kuichambua hali hii kwa kipindi kiasi kwahiyo tuzidi kuwa karibu katika darasa hili.

Entry filed under: maskani.

Hivi kukimbia ni kwenda mbele tu???? Yaliyojiri kikao cha 1 cha Bunge la awamu ijayo!!

1 Comment Add your own

  • 1. Ndesanjo Macha  |  August 9, 2005 at 11:46 pm

    Ukweli ni ukweli. Watakaokunyooshea kidole na wanyooshe. Kwani nani asiyejua kuhusu ufisadi uliojaa kwenye siasa Tanzania? Sijashuhudia uliyosema ila siwezi kubisha hata kidogo. Uchaguzi uliopita nilikuwepo na nilishuhudia na ninajua niliyoona haikuwa mwisho bali ndio mwanzo…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

  • 35,058 hits
August 2005
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031