Kumbe ‘Uhishimiwa’ ni Mtamu sana

July 9, 2005 at 9:36 pm 5 comments

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Tanzania, mwaka huu wa 2005, ambako Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu ambao utashirikisha vyama vingi vya kisiasa, vijana nchini humo wameamua kuwatolea uvivu waheshimiwa ambao wanatarajia kuzunguka mitaani siku chache zijazo kuanza kuwaomba Kura zao.

Wakiwa wanaunda sehemu kubwa ya Watanzania, (kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 vijana ni zaidi ya aslimia 65), vijana safari hii wameona kuwa haiwezekani wawape Kula jamaa zetu hawa, kwa kurubuniwa na peremende na makopo ya Juice. Wameamua kuhakikisha kuwa safari hii anapatikana kweli kiongozi au viongozi wa serikali ambayo itawajali hasa kwa kuwa wao ndio watakaokuwa sehemu kubwa ya kuwaingiza madarakani.

Katika kujiandaa na mchakato mzima wa kuhakikisha kuwa anapatikana kiongozi ambaye atakuwa mwenye kuvipa umuhimu vipaumbele vyao, vijana takriban 120, toka mikoa yote ya Tanzania wamekusanyika jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kile walichokiita Bunge Kivuli la Vijana wa Tanzania.

Pamoja na mambo mbalimbali, Bunge hilo ambalo kwa hakika utukufu wake ni wa uhalisia na wala sio wa ki-kivuli-kivuli kama walivyopenda kuliita, Vijana hao wameamua kujadili kwa kina juu ya mada kuu mbili ambazo zimekuwa zikiwaumiza sana kwa miaka nenda rudi sasa. Mada hizo ni Sheria ya mwaka 1971 kuhusiana na masuala ya Ndoa, pamoja na Sera ya Kitaifa ya Vijana.

Bunge hili limeandaliwa na taasisi ya vijana inayojulikana kwa jina la Youth of United Nations Association (YUNA), Tanzania, kwa ufadhili mkubwa wa shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la African Youth Aliance (AYA)

Katika siku za karibuni nitawaletea hatua kwa hatua, msisimko na kila lililojiri ndani ya Bunge hili ambako nami kwa mara ya kwanza kabisa niliuonja Uhishimiwa, sijui haya ndio maandalizi kwa ajili ya kwenda kuwania jimbo la mtu au vipi. Haya tusubiri tuone.

Entry filed under: maskani.

Wanywaji Tanzania Mmejikomboa Mnataka kujua tulilipana kiasi gani bunge letu!!!

5 Comments Add your own

 • 1. Idya Nkya  |  July 10, 2005 at 1:54 pm

  Tutangoja utueleze kila linalojiri. Ni muhimu sana vijana kuleta mabadiliko halisi sasa na si uigizaji.

 • 2. Martha Dickson Mtangoo  |  July 11, 2005 at 6:31 pm

  Ulikuwa Unabeep Ee Mheshimiwa Kivuli wenzio wamepokea!

 • 3. Anonymous  |  July 12, 2005 at 2:10 pm

  guyz hizi ni zama mpya kabisa mnatakiwa kuwa na hari mpya na nguvu mpya kabisaa semeni kila mnaloona ni baya ambalo litaangamiza jamii semeni tu msiogope!

 • 4. Reginald Simon  |  July 14, 2005 at 3:18 pm

  Kweli Uhishimikwa mtamu, ukizingatia kuna posho, mbona hukutueleza posho zenu zilivyokuwa ili tulinganishe na wanachogombania wale Wahishimiwa wenzako

 • 5. Ramadhani Msangi  |  July 17, 2005 at 3:31 pm

  @Reginald Simon
  Mnataka kujua posho zetu? Nadhani haya ni masuala ya binafsi zaidi na pengine ndio maana unaona sisi hatupigi kelele maana tunachokipata chatutosha japo hakijafikia cha kugawana na wenzetu kama cha Q-Chief–>

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,061 hits
July 2005
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031