Archive for July, 2005

Kauli ya Vijana kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2005

Katika mfululizo wa upashanaji wa habari mbalimbali kuhusiana na yaliyojiri katika Bunge Kivuli la Vijana wa Kitanzania, lililofanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, hivi karibuni jijini Dar es salaam, leo hii nimeona niwajulishe kile walichokisema wakati wa uzinduzi wa ajenda yao. Isome ‘Hotuba ya Vijana wakati wa Uzinduzi wa Ajenda ya Vijana kuelekea Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005’ pamoja na kuufahamu kwa undani mchakato uliowezesha kupatikana kwa ajenda hiyo

July 20, 2005 at 9:33 pm 2 comments

Yaliyojiri kwenye Bunge la Vijana …1

Kulikuwa na mambo mengi sana ambayo tulijadili katika kikao chetu kilichofanyika kati ya Julai 8-10, jijini Dar es salaam. Hata hivyo jambo la msingi kabisa ambalo lilijiri ni uzinduzi wa Ajenda yetu vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2005. Isome ajenda hiyo hapa, pamoja na baadhi ya nukuu muhimu sana ambazo zilijiri wakati wa kikao kizima. Soma nukuu za mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe, Bw. Ibrahim Kaduma, ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo hapa. Pia soma nukuu za vijana wenyewe wakati wa kikao hicho hapa.

July 16, 2005 at 11:55 am 5 comments

July 16, 2005 at 11:55 am 4 comments

Hapo zamani za Kaaaaaaale hali ilikuwa hivi!!

Hapo zamani za kaaaaaaaaale Ningelikuwa na uwezo, hakika ningerejelea zama hizi haraka iwezekanavyo maana sikuwa na taabu yoyote enzi hizo lakini sasa, duh!!!
Enzi hizo bwana!!!
Kweli zama hizo za kale………!!!!!!!!!!!!
Picha za utoto wangu hizo wajameni

July 15, 2005 at 11:19 am Leave a comment

Mnataka kujua tulilipana kiasi gani bunge letu!!!

Hawa ni baadhi ya Vijana walioshiriki katika Bunge la Kwanza kabisa katika historia ya Tanzania, Bunge Kivuli la Vijana, ambalo lilifanyika kwa muda wa siku tatu tu, katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es salaam, lakini huwezi amini kuwa siku hizo tatu zilikuwa na maana kubwa sana katika uelekeo wa Tanzania.

Endelea kuwa mkao wa kujua nini hasa kilichojiri huko, kaka yangu mmoja anataka kujua posho zilikuwa je ili alinganishe na zile zinazowatoa roho wahishimiwa wenzetu kule Idodomya.

July 15, 2005 at 10:42 am 2 comments

Kumbe ‘Uhishimiwa’ ni Mtamu sana

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Tanzania, mwaka huu wa 2005, ambako Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu ambao utashirikisha vyama vingi vya kisiasa, vijana nchini humo wameamua kuwatolea uvivu waheshimiwa ambao wanatarajia kuzunguka mitaani siku chache zijazo kuanza kuwaomba Kura zao.

Wakiwa wanaunda sehemu kubwa ya Watanzania, (kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 vijana ni zaidi ya aslimia 65), vijana safari hii wameona kuwa haiwezekani wawape Kula jamaa zetu hawa, kwa kurubuniwa na peremende na makopo ya Juice. Wameamua kuhakikisha kuwa safari hii anapatikana kweli kiongozi au viongozi wa serikali ambayo itawajali hasa kwa kuwa wao ndio watakaokuwa sehemu kubwa ya kuwaingiza madarakani.

Katika kujiandaa na mchakato mzima wa kuhakikisha kuwa anapatikana kiongozi ambaye atakuwa mwenye kuvipa umuhimu vipaumbele vyao, vijana takriban 120, toka mikoa yote ya Tanzania wamekusanyika jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kile walichokiita Bunge Kivuli la Vijana wa Tanzania.

Pamoja na mambo mbalimbali, Bunge hilo ambalo kwa hakika utukufu wake ni wa uhalisia na wala sio wa ki-kivuli-kivuli kama walivyopenda kuliita, Vijana hao wameamua kujadili kwa kina juu ya mada kuu mbili ambazo zimekuwa zikiwaumiza sana kwa miaka nenda rudi sasa. Mada hizo ni Sheria ya mwaka 1971 kuhusiana na masuala ya Ndoa, pamoja na Sera ya Kitaifa ya Vijana.

Bunge hili limeandaliwa na taasisi ya vijana inayojulikana kwa jina la Youth of United Nations Association (YUNA), Tanzania, kwa ufadhili mkubwa wa shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la African Youth Aliance (AYA)

Katika siku za karibuni nitawaletea hatua kwa hatua, msisimko na kila lililojiri ndani ya Bunge hili ambako nami kwa mara ya kwanza kabisa niliuonja Uhishimiwa, sijui haya ndio maandalizi kwa ajili ya kwenda kuwania jimbo la mtu au vipi. Haya tusubiri tuone.

July 9, 2005 at 9:36 pm 4 comments

July 9, 2005 at 9:36 pm 5 comments

Blog Stats

  • 34,787 hits
July 2005
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031