Archive for June, 2005

Majibu yangu yako tayari

Wapendwa vijana wenzangu, mabibi na mabwana, napenda kuwaambia kuwa hatimaye majibu yangu kuhusiana na afya yangu kama ambavyo niliahidi kuwa nitawataarifuni nikitoka Angaza, yako tayari na niko tayari kuyapandisha hapa wakati wowote, lakini kabla sijafanya hivyo, naomba kwanza tushirikiane kufanya hili.Naomba kila mmoja wenu ajaribu kuotea kuwa yamekuwa ya namna gani na kwanini yamekuwa hivyo unavyodhania wewe, na unanishauri nini kutokana na majibu unayodhania kuwa nimepewa huko??

June 23, 2005 at 12:36 pm 1 comment

Kila unachohitaji kiko hapa

Hii ni nzuri zaidi kwa waandishi wa habari na wanafunzi na kwa ujumla jamii ambayo imekuwa na shauku ya kutaka kujua historia au wasifu wa mataifa mbalimbali duniani. Mambo yote haya yanaweza kupatikana hapa.

June 20, 2005 at 11:51 am Leave a comment

Uchaguzi wa Iran katika Blogi

Bilashaka hii itakuwa changamoto kubwa sana kwa wanablogi wa Kitanzania, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Soma hapa kujua kile Ma-bloga wa Iran wanachowafanyia wananchi wa Iran katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wao. Haya sasa ma-bloga wa kiswahili, kazi kwetu

June 20, 2005 at 11:35 am Leave a comment

Mapambano dhidi ya UKIMWI bado sana

Wapo ambao wanajitahidi kuishi kwa matumaini kama hawa, na hakika wapo ambao wanajitahidi zaidi kufanya hivyo wakiwa wanajua kuwa hakuna jinsi zaidi ya kuukubali ukweli kama huyu, na wapo wale ambao wanaonyesha mfano mzuri kwa wapenzi wao licha ya kuwa wamesha athirika kama huyu, lakini je, kwa haya yaliyomkuta jamaa huyu, kweli mapambano dhidi ya Ukimwi yatafanikiwa kweli, tena basi serikali ndio inayokuwa imeshiriki? Hakika mapambano dhidi ya UKIMWI bado yana safari ndefu sana

June 20, 2005 at 11:08 am Leave a comment

Bajeti anayotuacha nayo Kaka Beni hii hapa

Bw. Basil Pesambili Mramba
Hatimaye kile kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kubwa na mamia kama sio mamilioni ya Watanzania kilielezwa jana. Bajeti ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2005/06, kama ambavyo ilisomwa na Waziri mwenye dhamana yawizara hiyo Bw. Basil Pesambili Mramba.

Kama ilivyokuwa inatarajiwa, wapo ambao wameshaanza kuiponda (na haishangazi kwakuwa wapo ambao walishaponda hata kabla haijatoka), wapo ambao wanaisifu na wapo ambao wako kwenye lile kundi la Wenzangu na mimi ambao kwao.. ah! bora siku zinakatika tu. Ingesomwa isingesomwa kwao sawa.
Je wewe unaizungumziaje bajeti hii ya mwisho ya serikali ya awamu ya tatu iliyosomwa wakati enzi za serikali hiyo zikiwa zinaelekea ukingoni?? Isome hapa bajeti hiyo.

June 9, 2005 at 1:26 pm 1 comment

Older Posts Newer Posts


Blog Stats

  • 35,061 hits
June 2005
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930