Archive for May, 2005

Haya ndio aliyoyaombea Msamaha?

papa
Huyu ni hayati Baba Mtakatifu, John Paul II, ambaye katika enzi za uhai wake, siku chache sana kabla hajatangulia mbele za haki, aliwahiwashangaza sana baadhi ya waumini na wasio waumini wa Kanisa katoliki kote duniani, kwa kusimama hadharani na kuomba msamaha kutokana na makosa mbalimbali ambayo alisema kuwa kanisa limeyafanya kwa kipindi kirefu yasiyokuwa ya kimaadili na ambayo yalikuwa yakiiumiza jamii na (bilashaka), kuliweka kanisa katika hali tata.

Inawezekana kabisa kuwa wengi kati ya waliomsikia akisema hayo, hawakujua kuwa alimaanisha nini, lakini ushahidi kuwa kweli mambo hayo yalikuwepo na kwamba sio ajabu kuwa yataendelea unazidi kujionyesha wazi wazi. Unajua ni kwanini? Soma hapa na kisha utoe maoni yako kuhusiana na hili.

May 25, 2005 at 7:29 pm Leave a comment

Wote mmekombolewa

Ni kutokana na ushauri (japo haukuwa rasmi) wa Ethan, nimeamua kwa makusudi kabisa na kwa manufaa ya wengi wetu kuanzisha safu mpya kadhaa katika Blogi yangu. Safu hizo ni pamoja na ile ya Vijana, Maisha na Mahusiano pamoja na ile ya Burudani na Vitimbwi.

Kona ya Maisha na Mahusiano, itakuwa na mambo mbalimbali hasa kuhuisiana na aina ya maisha ya kila siku tunayoishi, matatizo tunayokumbana nayo, changamoto mbalimbali za kimaisha na hata kushauriana mambo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha hali zetu za kimaisha na kimahusiano kwa ujumla.

Kona ya Vijana, itakuwa na mambo mbalimbali ambayo kundi hili lililokuwa kubwa sana katika jamii licha ya kusahaulika au kutotiliwa mkazo, limekuwa likikumbana nayo. Yapo mambo kadhaa ya kujadiliana hapa likiwemo tatizo la janga la UKIMWI, ukosefu wa Ajira, madawa ya kulevya na mengine kadhaa wa kadha. hakika huu utakuwa ukumbi kwa ajili ya vijana kukutana na kujadiliana kuhusu hayo na zaidi ili kubadilishana uzoefu wa kimaisha.

Na kwakuwa kazi huwa ni lazima (sijui falsafa hii ilianzishwa na nani hasa), iende na dawa, kutakuwa na ukumbi wa Burudani na Vitimbwi mbalimbali. hapa tutakutana na Hadithi mbalimbali nilizozitunga mimi au kutungwa na watunzi wengine ambao watapenda kushiriki katika kona hii. Pia utakutana na vituko mbalimbali vinavyotokea mitaani na pengine zaidi utakutana na Katuni za kukufanya Uburudike na kujifunza pia.

Je, wewe ni kijana, mzee, mtoto au mtu wa rika gani? hakika naamini kuwa wote sasa tunakaribia kuwa na sehemu inayotufaa katika Blogi hii. Karibuni tujikomboe kwa kubadilishana uzoefu wa maisha.

May 24, 2005 at 8:10 pm 2 comments

May 24, 2005 at 8:10 pm Leave a comment

Ilikuwa Siku ya Kufa Nyani?

tumeshinda

Hakika kila achekaye mwisho hucheka sana, sijui kuwa ilikuwa siku ya kufa nyani, miti yooote ikawa inateleza au yalikuwa yale ya “Yakhe, kufungwa twafungwa lakini vyenga twawala”, sijui kwakweli jambo moja ninalojua na ambalo nina uhakika nalo ni kuwa tumebeba kombe la FA, tena sio hivyo tu, bali pia tumelibeba toka mikononi mwa Manchester United. Poleni mlioumia

May 24, 2005 at 10:57 am 4 comments

Kutoka KILIMANJARO hadi KILIMACHAO

Kutoka 'Kilimanjaro' hadi 'Kilimachao'
Hii ni sehemu ya kilele cha Mlima ambao awali sio tu kwamba ulikuwa umefunikwa kwa theluji kwa zaidi ya asilimia 75 ya eneo lake, bali pia rasilimali muhimu sana kwa Watanzania, rasilimali ambayo ingeliweza kulifanya taifa hili kuvuna mabilioni ya Dola kupitia mlima huu.
Lakini dah!, yaliyoupata mlima huu ni makubwa mno. Sio tu kuwa Watanzania tulishindwa kabisa kuudhihirishia ulimwengu kuwa mlima huu ni wetu (uko Tanzania), bali pia tumeshindwa kuutunza hadi theluji iliyokuwa imeufunika imebakia kuwa sehemu ya masimulizi ya kale. na unajua nini, sio ajabu miaka kadhaa ijayo ukajasikia kuwa mlima huo kakabidhiwa mwekezaji ili auendeleze kwa maana sisi tumeshindwa.
Alahaula jamani

May 19, 2005 at 8:18 pm 3 comments

Wote ni waswahili, Wote ni waandishi na Wote ni wanasiasa!!

Napenda kwanza nikiri kuwa nimeandika kazi hii kutokana na kazi ya Bw. Ezuckerman, ambayo aliiandika katika Global Voices. Unaweza kuusoma waraka wake huo kwa kubonyeza hapa. Kuna mambo mengi sana ambayo aliyazungumzia katika waraka wake, lakini kuna baadhi ambayo yalinivutia sana. Licha ya kuonyesha kukubali kwake jitihada za watanzania katika kublogu kwa kutumia lugha ya Kiswahili, alikuwa na mambo kadhaa ambayo mbali ya sisi kuweza kumjibu, bilashaka yanatakiwa kuwa changamoto mpya kwetu sisi.

Kwanza alibaini kuwa sehemu kubwa ya Wanablogu wa Kitanzania ni waandishi wa habari, akajiuliza je hilo linamaanisha nini?, Pili alibaini kuwa karibu wote wamekuwa wakijadili zaidi masuala ya Kisiasa, je hakuna mambo mengine ambayo wanaweza kujadili zaidi ya hayo?

Kwa kuanzia, labda nadhani nianze kuwauliza wanablogu wenzangu wa Kitanzania swali hili, Je, Hayo mawazo ya Bw. Ezuckerman, yanamaanisha nini kwetu sisi? Kisha tutaendelea zaidi kwa kuanzia hapo.

May 19, 2005 at 12:54 pm 4 comments

Muziki wa Tanzania

Hivi umeshawahi kujiuliza kuwa huu muziki wa Tanzania ambao katika siku za hivi karibuni umekuwa ukisifiwa saaaaana kuwa unakua tena kwa kasi ya ajabu, ulianza anza vipi?, Hebu soma hapa kujua yote hayo

May 19, 2005 at 11:49 am Leave a comment

Older Posts Newer Posts

Blog Stats

  • 34,787 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031