Mambo Motomoto Ukumbi wa Vijana

May 31, 2005 at 8:05 pm 5 comments

Makala hii itakuwa ni moja kati ya kazi zangu nyingi sana ambazo zitakuwa zikiwagusa kwa undani sana vijana (wenzangu wa CCM, wanajua namaanisha hadi umri gani), kuhusiana na maisha yao ya kila siku na hasa katika harakati zao za kila siku za kupambana na gonjwa harati la UKIMWI.
Pamoja na mambo mbalimbali yatakayokuwemo katika kona hii, pia katika siku za karibuni utaweza kukutana na historia yangu kwa undani kiasi chake na nini hasa nimeweza kufanya katika harakati za kupambana na ukimwi. Je wajua kwanini niliamua kwenda kupima na unajua kuwa matokeo yangu yalikuwaje?, Basi kaa tayari kwa ajili ya kusoma kazi hii hivi karibuni.
Wakati tukiwa tunasubiri kwa hamu kazi hii, naomba tuendelee na kazi ambazo ziko tayari tukianzia na hii hapa.

Entry filed under: maskani.

Mambo Motomoto Ukumbi wa Vijana Kuelekea Kongamano la BlogHer ’05

5 Comments Add your own

 • 1. J4 wa Dar  |  May 31, 2005 at 8:09 pm

  Mshkaji umekuwa na moyo wa namna gani hadi kufikia hatua hii, maana inatushinda vijana wengi sana (Hakika nami nikiwa mmoja wapo), nadhani itabidi nifuatilie kwa sana mkasa huu ili niweze kujifunza jambo katika maisha yako. Tutawasiliana zaidi kwa ushauri katika anwani zako kama ulivyozionyesha hapo kwenye web yako naamini zinafanya kazi kaka au sio???

 • 2. Martin Joseph  |  May 31, 2005 at 8:13 pm

  Sasa naanza kuamini kitu kimoja kuwa Tanzania ina watu wenye ari na wakweli tena kweli kweli wala sio hawa wana-SIHASA wetu ambao ndio wanaohimiza hizo sera za uwazi na ukweli. Itabidi kujua kuwa kuna vijana wangapi wameweza kufanya kama ulivyofanya, au unavyotarajia kufanya wewe. au mradi nini maana watu wanaokuwa wazi namna hii huwa na malengo yao

 • 3. Wakuchonga  |  May 31, 2005 at 8:15 pm

  Huo uchunguzi haujatulia kaka, uchunguzi gani ambao unaongea na watu 300 na kisha kutoa tathmini yako tena mwenyewe, kama unataka kufanya uchunguzi wasiliana na wadau kisha wakweleze la kufanya sio kukurupuka tu. Kuwa makini ndugu ila kazi njema sana (blogi yako)

 • 4. Mama Junior  |  June 1, 2005 at 10:12 am

  watu wengine bwana, bado wako zama za mawe za kale! wakati watu wako katika ulimwengu wa sayansi na teknlojia, kwani uchunguzi unatakiwa ufanywe kwa watu wangapi? kwa taarifa yako wa kuchonga uchunguzi unaweza kufanywa hata kwa watu wawili tu na ukapata kile unachohitaji, hao 300 aliofanya kijana anatisha bwana mpe pongezi zake usimbanie. Unatisha kaka!

 • 5. Zainab Yusuph  |  June 21, 2005 at 11:33 am

  hongera sana kaka kwa kazi nzuri unayofanya kwani inataka moyo kuamua kufanya jambo kama hilo hasa kwa vijana wa leo ambao uchunguzi wako umeonyesha hawako tayari kwenda kujua afya zao. makala nzuri na ningependa kujua zaidi kuhusu matokeo ya majibu yako baada ya kupima na ni hatua gani utachukua endapo utakuwa umepata virusi.
  Big up sana mungu atakusaidia!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031