Ilikuwa Siku ya Kufa Nyani?

May 24, 2005 at 10:57 am 4 comments

tumeshinda

Hakika kila achekaye mwisho hucheka sana, sijui kuwa ilikuwa siku ya kufa nyani, miti yooote ikawa inateleza au yalikuwa yale ya “Yakhe, kufungwa twafungwa lakini vyenga twawala”, sijui kwakweli jambo moja ninalojua na ambalo nina uhakika nalo ni kuwa tumebeba kombe la FA, tena sio hivyo tu, bali pia tumelibeba toka mikononi mwa Manchester United. Poleni mlioumia

Entry filed under: maskani.

Kutoka KILIMANJARO hadi KILIMACHAO Wote mmekombolewa

4 Comments Add your own

 • 1. Martha Mtangoo  |  May 24, 2005 at 12:42 pm

  Siku hii ilikuwa nzuri sana kwetu washika Bunduki lakini kwa upande wa wale wenzetu mashetani wekundi ilikuwa msiba, wengine walikuwa hawataki hata kupigiwa cm kupokea ikawa kaazi, ni raha sana kijana me naendelea na raha mpaka hapo fainali nyingine. furgeson ajiuzulu/

 • 2. Anonymous  |  May 24, 2005 at 4:42 pm

  Jamani,tuachane na haya mambo ya utumwa wa kiakili.Hivi kweli inakuwaje mtanzania kuwa mshabiki wa timu za Uingereza mpaka kudiriki kusema eti “tumebeba kombe”??Huoni kwamba huko ni kujidhalilisha na kuukosea heshima uzalendo wetu?Wapi mashabiki wa Yanga,Simba,Mtibwa,Kagera Rangers na wengineo?Sikatai mtu kuvutiwa na jinsi timu kama Arsenal au Man U inavyosakata kabumbu ila suala la kujiona kwamba na wewe sasa umekuwa muingereza kwa kweli siliafiki.Jivunie chako bwana hata kama kinatia kinyaa.Peace

 • 3. Yahaya Abdallah  |  May 24, 2005 at 8:19 pm

  @Anonymous
  Unamuonea gere mwenzako kwasababu kama umefuatilia vyema blogu yake kuna sehemu alikiri wazi kuwa yeye ni shabiki wa Simba ya Tanzania. lakini ulichukulie hilo kuwa ni kukata tamaa na mambo yetu kuwa ya hovyo ndio maana tunapenda vya nje. Toka lini aliyeko katika ndoa akatoka nje kama sio kutukuwepo kwa yaliyobora ndani kwake??, VIVA ARSENAL.

 • 4. Martha Mtangoo  |  May 26, 2005 at 1:43 pm

  uwanja wa kuchangia ni kwa wale tu wasio na jazba, sasa inakuwaje wewe bw. Said uwe unachangia hoja huku una jazba? inaonekana kabisa kuwa wewe ni Shabiki wa Man United live, sasa kutokana na kufungwa na Arsenal unaonyesha jazba zako kwa wanablog acha hizo kijana Tanzania ni nchi yenye uhuru na kila mtu ana uhuru wa kufanya kile anachojisikia ili mradi tu asivunje sheria. VIVA ARSENAL!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031