Wote ni waswahili, Wote ni waandishi na Wote ni wanasiasa!!

May 19, 2005 at 12:54 pm 4 comments

Napenda kwanza nikiri kuwa nimeandika kazi hii kutokana na kazi ya Bw. Ezuckerman, ambayo aliiandika katika Global Voices. Unaweza kuusoma waraka wake huo kwa kubonyeza hapa. Kuna mambo mengi sana ambayo aliyazungumzia katika waraka wake, lakini kuna baadhi ambayo yalinivutia sana. Licha ya kuonyesha kukubali kwake jitihada za watanzania katika kublogu kwa kutumia lugha ya Kiswahili, alikuwa na mambo kadhaa ambayo mbali ya sisi kuweza kumjibu, bilashaka yanatakiwa kuwa changamoto mpya kwetu sisi.

Kwanza alibaini kuwa sehemu kubwa ya Wanablogu wa Kitanzania ni waandishi wa habari, akajiuliza je hilo linamaanisha nini?, Pili alibaini kuwa karibu wote wamekuwa wakijadili zaidi masuala ya Kisiasa, je hakuna mambo mengine ambayo wanaweza kujadili zaidi ya hayo?

Kwa kuanzia, labda nadhani nianze kuwauliza wanablogu wenzangu wa Kitanzania swali hili, Je, Hayo mawazo ya Bw. Ezuckerman, yanamaanisha nini kwetu sisi? Kisha tutaendelea zaidi kwa kuanzia hapo.

Entry filed under: maskani.

Muziki wa Tanzania Kutoka KILIMANJARO hadi KILIMACHAO

4 Comments Add your own

 • 1. Anonymous  |  May 21, 2005 at 2:42 pm

  Hakika nami namuunga mkono japo sio asilimia miaa ila nadhani naweza kumpa asilimia 75 kuwaa utafiti wake alioufanya ni kama una ukweli asilimiaa kadhaa ndani yake kutokana na kuwaa hata ukijaribu kupitia website nyingi kama hazijazungumziaa maoja kwa moja siasa ila lazima utakuta kuna kurasa hata moja yaelezeaa siasa hii piaa inatoka na watanzania kuangalia mambo kwa kutokuyapima kiundani na kuiga piaa akiona bwana nanihii kafanikiwa na ayuko kwenye mkodo wa siasa basi na yeye anaiga sio kuiga tu ila wakati mwinginee nikutafu ridhiki kwa hali flani mtu anajikuta anatumbukiaa mahali mkono uingia kinywani hii ikiwa na baadhi ya wandishi ukifuatiliaa hata kama tunasema vitu vinginee ni vipaji ila kwa kweli wenginee hiyo fani inawaburuza mana hawana mda wakujifunza wenzao wamefanya nini hawapendi kusomaa hasa majariba na vitabu mbali mbali ili kuwaweka katika hali yakujuwa mambo mengi wanadhani ukishaweza kuandikia gazeti flani basi huoo ndio uandishi laah Hasha.

  Nisionekane nagongeleaa msumari net upande mmoja tu bali ni kweli wavuti na sio hizo hata magazeti mengi nchini kwetu asilimia kubwa ni mambo ya siasa tu tubadilike mambo yako mengi.

  Elly Msuya
  Dodoma

 • 2. Baraka  |  May 23, 2005 at 9:31 am

  Tatizo kubwa sana hapa ni kuwa watu hatutaki kufahamu kuwa maisha yetu ya kila siku yamekuwa yakiendeshwa kisiasa siasa zaidi kuliko ukweli na ndio maana haishangazi kuona kuwa kila kona, sio vijiweni, sio mahotelini sio kwenye shirika lolote lile, porojo zilizopo ni za siasa zaidi. Kwa kifupi ni kuwa siasa ndio kila kitu hivi sasa sio Tanzania tu bali duniani. Mimi nawaunga mkono wote waliobobea katika siasa kwakuwa wana nafasi ya kuweza kubainisha kuna nini ndani yake na kisha wakatujuza nasi tukombolewe kutoka makucha ya WANASIHASA wetu.

 • 3. Mariam Ally  |  May 23, 2005 at 9:37 am

  Hivi ni nani anayeweza kuniambia mahali popote pale duniani ambako maisha sio siasa au siasa za mahali hapo sio maisha ya hapo? Nadhani waandishi wetu wanatakiwa kupewa moyo wa kuweza kujua kuna nini katika nguvu ya siasa ili watuhabarishe sisi wanajamii na ikiwezekana wao ndio wawe wakombozi wetu katika harakati za jamii kuhakikisha kuwa nguvu hizo zinashindwa katika jina la maendeleo ya jamii.

 • 4. ELLY MSUYA  |  May 23, 2005 at 10:20 am

  Hello wapendwa watanzania kama sio wazalendo waliojaaa na Uzalendo halisi wa Tanzania nimefurahi kuona kuwaa kuna wenginee pia wamechangia hoja ila bado mimi kwa mawazo yangu naona kuwa sio Kweli kuwa hakikaa kila mtu sasa abobee kwenye siasa ni kweli siasa ina nafasi kubwa katika ulimwengu lakini sio kweli kuwa hakuna mambo mengine yakufuatilia kuandika na kutoa taarifa kwa wazalendo wajuwee maisha ya kila siku mfano Je hatuna waandishi wanaojaribu hata kuchambua mambo kama vile wananchi wajuee jinsi yakutunza miili yaoo kiafya kuijifahamu hasa kama mtu uliyee hai uufanyiee nini mwili wako huoni kuwaa wakiandiika elimu hiyo na wakaitiliaa maanani tunawezaa kujenga Taifa kupitia waandishi piaa mana wanasiasa haoo haoo ndio leo hii unasikiaa shinikizo la damu ila anageelezwa jinsi yakula jinsi yakufanya mazoezi na mambo kama hayo huoni kuwa tungeepukana na kupoteza nguvu kazi ambayo ukiangalia kwa makini ni watu wenye ujuzi na wenye nguvu katika ajamii yetu yani nazungumziaa nguvu yakiuchumi iko mikononi mwa watu wenye afya njema.

  Vile vilee tunaweza kutumiaa muda wetu piaa kueleza jamii Historia ya nchi yetu ikiwa bial kusahau maliasili na elimu ya Uraia ambayo ni haki ya kila mwananchi katika nchi yake.

  ASANTE

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

 • 35,058 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031