Kutoka mwanaharamu Rushwa hadi Mtakatifu Takrima

May 10, 2005 at 7:14 pm 2 comments

Hata kama watu wataandamana kwa namna gani, bado haitosaidia kitu, ukweli utabakia pale pale kuwa tatizo la rushwa humu Duniani sio tu kwamba lipo bali pia linazidi kutukuzwa sana hasa na watawala wetu na haishangazi kuwa wamekuwa wakijitahidi sana kuihalalisha kwa kuipa majina mbalimbali kama hili Wadanganyika waliloambiwa ndio lenye kufaa sasa, TAKRIMA.

Ukiuliza kuna tofauti gani baina ya maneno haya, utaambiwa eti Takrima ni Bahshish na wala sio rushwa bali pale itakapokuwa imezidi, na ukiuliza kuwa kipimo cha kuijua kuwa imezidi kiasi cha sasa kuweza kuitwa rushwa kiko namna gani utaishia kuambiwa ‘ooh sijui kimepandia hapa kisha kikashukia kule, ooh sijui hili neno bwana lina asili ya kiarabu likimaanisha asante na mambo meeeeeengi yasiyo maana.

Imekuwa jambo la kawaida hivi sasa kuwa kujadili suala la Rushwa na mtu yeyote yule hasa awe kwenye hili kundi la hawa Watakavitu wetu, ni sawa na kupoteza muda wako bure maana utaishia kupigwa ngonjera za ajabu ajabu zisizo na kichwa, miguu wala kiwiliwili, utaishia kuambiwa mambo ambayo Watoto wa mitaa ya jiji la Dar es salaam hivi sasa wanakiita Longolongo, Lakini je ni kweli kuwa suala hili haliwezi kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa japo kulimaliza kabisa imeshindikana??, huu ndio mjadala ambao napenda tushiriki kuujadili wanablogi wenzangu, karibuni

Entry filed under: maskani.

Kutoka mwanaharamu Rushwa hadi Mtakatifu Takrima Timua timua ndani ya Simba na Yanga na hatima ya soka la Tanzania

2 Comments Add your own

  • 1. Indya Nkya  |  May 10, 2005 at 9:48 pm

    Msangi hii hoja si mchezo kabisa. Watu wanapojaribu kuhalalisha uoza wana mambo. Watabadilisha majina watafanya kila kitu. Watasema ikizidi ndiyo rushwa bila kuwekwa kiwango. Kuzidi ndio kupi? Hakuna tofauti ya rushwa na takrima.

  • 2. ELLY MSUYA  |  May 23, 2005 at 10:40 am

    Haya haya Trafiki huyo hebu tuajaribu kama tuatapiata jamani wagosi mko wapi achanani na wala Rushwa wadogo hao Trafiki shughuli iko huku kwa watu wenye maneno utazani wamakula Redio ukisema hivi unabadilishiwa ainakuwaa vilee sasa jamani hawa wataka vitu mm mimi sisemi sana ila tuje kwenye ukweli halisi “TAKRIMA” NI MFUKO unaofunika neno RUSHWA kwa wnzangu watu wa kompyuta kama mimi naweza seama hiyo ni Folder ila ukiingiaa ndani ndio waweza juwa hakika File linaitwaje na linazungumziaa nini ningerudi katika hali ya uhalisi ni kuwaa sawa na mtu aliyevaa nguoo safi juu lakini ngani akawa na nguo chafu ukiwaita watu wasafi na yeye atatoka na kusema nami pia ni msafi ila sasa ukianza kusema kila mtu asaulee nguo moja moja ili tumpatee msafi halisi watakimbia wote sasa na watu wanaosema TAKRIMA ndio mana ukiwafuatilia sanaa unakuta hakuna kitu ni Nyumba tu imepakwa rangi ila ni ya Zamani rangi ya zamani ilikuwa inaitwa RUSHWA YA KISASA INAITWA TAKRIMA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

  • 35,058 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031