Archive for May 10, 2005

Kutoka mwanaharamu Rushwa hadi Mtakatifu Takrima

Hata kama watu wataandamana kwa namna gani, bado haitosaidia kitu, ukweli utabakia pale pale kuwa tatizo la rushwa humu Duniani sio tu kwamba lipo bali pia linazidi kutukuzwa sana hasa na watawala wetu na haishangazi kuwa wamekuwa wakijitahidi sana kuihalalisha kwa kuipa majina mbalimbali kama hili Wadanganyika waliloambiwa ndio lenye kufaa sasa, TAKRIMA.

Ukiuliza kuna tofauti gani baina ya maneno haya, utaambiwa eti Takrima ni Bahshish na wala sio rushwa bali pale itakapokuwa imezidi, na ukiuliza kuwa kipimo cha kuijua kuwa imezidi kiasi cha sasa kuweza kuitwa rushwa kiko namna gani utaishia kuambiwa ‘ooh sijui kimepandia hapa kisha kikashukia kule, ooh sijui hili neno bwana lina asili ya kiarabu likimaanisha asante na mambo meeeeeengi yasiyo maana.

Imekuwa jambo la kawaida hivi sasa kuwa kujadili suala la Rushwa na mtu yeyote yule hasa awe kwenye hili kundi la hawa Watakavitu wetu, ni sawa na kupoteza muda wako bure maana utaishia kupigwa ngonjera za ajabu ajabu zisizo na kichwa, miguu wala kiwiliwili, utaishia kuambiwa mambo ambayo Watoto wa mitaa ya jiji la Dar es salaam hivi sasa wanakiita Longolongo, Lakini je ni kweli kuwa suala hili haliwezi kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa japo kulimaliza kabisa imeshindikana??, huu ndio mjadala ambao napenda tushiriki kuujadili wanablogi wenzangu, karibuni

May 10, 2005 at 7:14 pm 2 comments

May 10, 2005 at 7:14 pm Leave a comment

“Nilikwambia tu kuwa utakuwa ‘Papaa’ si umeona mwenyewe!!

alaa
Originally uploaded by Ramadhani Msangi.

Hivi ungekuwa umepewa kazi ya kubashiri hawa jamaa walikuwa wakiteta jambo gani hapa ikiwa ni muda mfupi tu, yaani dakika kadhaa baada ya Bw. Jakaya Mrisho Kikwete (Kushoto)kutangazwa kuwa yeye ndiye atakuwa mrithi wa Bw Benjamin William Mkapa, pale katika lile jumba jeupe (Ikulu. Hebu jaribu kunieleza kuwa walikuwa wakisema nini, japo mimi nadhani Mkapa alikuwa akimwambia mdogo wake kuwa yeye alijua tu kuwa baada ya Papa Benedicto XVI kule Vatican, kwa huku Bongo ilikuwa zamu yake kuukwaa ‘Upapaa. tehe tehe tehe!!!

May 10, 2005 at 11:01 am 3 comments

"Nilikwambia tu kuwa utakuwa ‘Papaa’ si umeona mwenyewe!!

alaa
Originally uploaded by Ramadhani Msangi.

Hivi ungekuwa umepewa kazi ya kubashiri hawa jamaa walikuwa wakiteta jambo gani hapa ikiwa ni muda mfupi tu, yaani dakika kadhaa baada ya Bw. Jakaya Mrisho Kikwete (Kushoto)kutangazwa kuwa yeye ndiye atakuwa mrithi wa Bw Benjamin William Mkapa, pale katika lile jumba jeupe (Ikulu. Hebu jaribu kunieleza kuwa walikuwa wakisema nini, japo mimi nadhani Mkapa alikuwa akimwambia mdogo wake kuwa yeye alijua tu kuwa baada ya Papa Benedicto XVI kule Vatican, kwa huku Bongo ilikuwa zamu yake kuukwaa ‘Upapaa. tehe tehe tehe!!!

May 10, 2005 at 11:01 am Leave a comment

Blog Stats

  • 34,787 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031