Mzee Malecela akata rufaa!

May 3, 2005 at 5:23 pm Leave a comment

Kwa wengi wenu naamini kuwa tayari hadi wakati huu mshajua kuwa nini kinaendelea mjini Dodoma, mahali ambako ‘Baraza la Mapapa’ wa CCM limekutana kwa ajili ya kufyeka wagombea kumi kati ya 11 walionunua fomu zao, na hatimaye kubakia naye mmoja tu ambaye watamtangaza kuwa ‘Papa’ wao. Kwa wale ambao walikuwa bado hawajajua lolote nadhani wanaweza kujua kwa kusoma hapa au hapa. na kisha baada ya hapo waungane na wenzao ambao tayari walishajua kutambua kuwa, baada ya matokeo ya kamati kuu kumwengua katika kinyang’anyiro hicho, mmoja kati ya wagombea wanaouwania kweli kweli urais, John Samwel Malecela, ameamua kukata rufaa kupinga kitendo cha yeye kupigwa panga.

Ingawa hakukutolewa sababu maalum na wasemaji wakuu wa chama hicho, duru za kisiasa ndani ya chama zimedai kuwa, ameamua kutaka rufaa kutokana na kutokuridhiswa na yeye kupigwa kumbo, kisha akabakia Fredrick Sumaye katika kinyang’anyiro hicho.

uamuzi huo, ulitarajiwa kuleta shughuli nzito zaidi katika kikao cha halmashauri kuu tofauti na hapo awali ambapo ilidaiwa kuwa halmashauri kuu isingekuwa na kazi katika kuwachuja wagombea watano waliokuwa wamesalia. lakini hili sasa litamaanisha kuwa mkutano huo ungejadili kwanza rufaa kabla ya kuingia hatua ya kutafuta tatu bora.

Ugumu wa zoezi hilo, unatokana na ukweli kuwa, licha ya kuwa anaweza kuwa hana vigezo, lakini mlalamikaji ni mmoja kati ya watendaji wenye nguvu ndani ya chama, na huenda ikiwa ataendelea kuonekana kuwa hafai kuendelea kuwania nafasi hiyo, akalazimika kufyerkwa na mtu wake anayemlalamikia.

Tuombe Mungu tusione tu moshi mweupe.

Entry filed under: maskani.

Moshi bila damu? Mzee Malecela akata rufaa!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

  • 35,058 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031