Moshi bila damu?

May 3, 2005 at 12:51 pm 1 comment

Poleni sana ndugu zangu ambao mmekuwa mkiusubiri kwa hamu sana Moshi utakaoufuka kutoka katika Sestine ya wana-CCM (Chimwaga), kujua kuwa utakuwa wa namna gani. Najua ni kwa kiasi gani mmekuwa na hamu sana ya kujua moshi huo utakuwa wa aina gani, mwekundu, mweusi, kijani, njano au cheche kama ninavyoamini mimi; lakini jambo moja ninalowaombeni mtambue ni kwamba, moshi huu mnaousubiri bwana sio sawa na ule wa Vatican.

Huu ni moshi ambao ili uweze kutoka ni lazima kwanza “damu imwagike”. Unashangaa!. Waliokuwa wamenunua (Kuchukua??), fomu ni watu 11, kati ya hao ni mmoja tu ambaye anatakiwa, unadhani hawa wengine watafanywa nini?. Kuchinjiwa baharini, kama wenyewe wanavyoita zoezi hilo la mchujo, ndio maana nawaambia kuwa subira yenu ni muhimu sana kwasababu ni lazima ‘damu’ za watu 11, zimwagwe baharini kwanza ndio moshi uweze kutoka.

Kwamba moshi utakuwa wa aina gani, hilo ni swali jingine kabisa lakini ni lazima utoke na ni lazima kwanza utanguliwe na kumwagika kwa damu za watu watakaochinjiwa baharini. Wakati naandika kaujumbe haka, tayari sita wameshachinjiwa baharini zamaaaaani sana, na tunasubiri wengine wawili kisha wawili tena ili tumpate mmoja na mgombea mwenzake.

Kigumu Chama cha Mapinduzi

Entry filed under: maskani.

Moshi bila damu? Mzee Malecela akata rufaa!

1 Comment Add your own

  • 1. yakub nyembo  |  May 4, 2005 at 11:46 am

    Ni siku kadhaa sasa toka nalipokuwa naangalia kivuli cha mti kunacholifunika kwa upendo kaburi la mwana wangu pekee mbarikiwa wa amani na msuluhishi wa migogoro ya Afrika Tanzania,ndio ni kaburi lililoandaliwa rasmi,kaburi linalohitaji kumuweka kiumbe kisichohatia,najiuliza ni kwa nini?saa sita na dakika kumi na tano sasa napata wokovu wa mawazo naambiwa kwa ujumbe mfupi wa simu kiganjani kuwa muuaji,katili,mwizi na kibaka wa mwanangu tanzania tayari katupwa kwa hoja Malekela CHIGWEMISI,hana lake amekwisha kwa kuwa hakuna haja ya kuiuwa tanzania,nakumbuka yule mtukufu mzee aliyemuona mtoto yesu na kusema”sasa bwana waweza kumruhusu mja wako akaenda kwa amani kwa maana nimeuona utukufu wako.”namshukuru mungu lakini nashindwa kusema maneno yale ya mtukufu kwa kuwa bado benedict wa tz hajapatikana na moshi wa kaki na damu ya hatia inanukia yupo MUHUNI,hili si tusi ni neno katika siasa hata MWALIMU KALITUMIA KATIKA WAKATI NYETI KAMA HUU WA KUMTAFUta Musa wa tz ama kumtafuta SULEIMANI baada ya kumuona Adonia akihitaji mamlaka ya Daudi ,nini?NA nani mmeacha ambae kamshika shati mwanangu tanzania,ni siku ya pili sasa nauona mwanga wa Mungu katika giza la saa tatu karibu,nasikia yule aliyesema kuwa ni mkulima nae analia,kabaki na shati la yusuph baada ya kushindwa kufanya ufisadi,nasema sasa naweza kulala kwa amani,Mungu wangu!msangi upo mkubwa wangu na je Ndesanjo umepata habari hizi zilizonenwa katika vitabu vy manabii kuwa wenye macho wataona na wenye masikio watasikia kwa maana yuaja yule ambae si msafi lakini ni mteule aliyeteuliwa na wale kutoka vijijini ambao si wasomi bali ni wenye maamuzi ya upendo wa nafsi na akili zao je,ni nani huyo Mark,salim,ama Kikwete?yeyote lakini tunawajua hawa, tuwakumbushe kuwa hatutafuti katibu wa chama bali mgombea urais wa watanzania.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

  • 35,061 hits
May 2005
M T W T F S S
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031