Archive for April, 2005

Uwazi wa Mkapa huu hapa

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Chama tawala nchini Tanzania, CCM, na pengine katika historia nzima ya Tanzania, uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, kwa mwaka 2005, unatarajiwa kurushwa moja kwa moja toka katika ukumbi wa Chimwaga. Soma tamko la katibu mkuu wa CCM, Bw. Philip Mangula hapa

April 29, 2005 at 5:53 pm Leave a comment

Hawa ndio wabunge wetu, na haya ndio madudu yao

Sakata la waheshimiwa wabunge wetu ambao tuliwateua kwenda kutuwakilisha katika chombo cha kutunga sheria (Bunge), la kuhusika katika tuhuma za kuwatafutia Visa wanawake wawili wa kisomali kwa ajili ya kuwapeleka ng’ambo, limezidi kuwa mjadala mkubwa nchini Tanzania toka Bunge lilipoamua kuwatimua hadi mwezi Agosti mwaka huu.

Siku moja baada ya kutimuliwa kwao, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti tukio hilo. Soma kilichoandikwa siku hiyo katika magazeti ya Majira na Nipashe kisha utoe maoni yako kuhusiana na kashfa hii kubwa kuwahi kumkumba kiongozi wa ngazi hii.

April 29, 2005 at 12:12 pm Leave a comment

Nukuu maridhawa

Katika kipindi hiki ambapo tunauelekea uchaguzi mkuu, pilika pilika kibao zenye lengo la kuchafuliana majina hasa kwa wawania nafasi ya kuwa wagombea ‘Urahisi’ kwa tiketi ya CCM, zimekuwa zikipamba moto kila kukicha.

Inavyoelekea ni kuwa wamesahau kabisa wajibu wao kuwa ni kutushawishi sisi kuwa wamefanya mambo gani kwa ajili ya kustahili kuwa mashujaa wa taifa hili na badala yake wameelekeza juhudi zao katika kuchafuliana majina. Watanzania kadhaa wamekuwa wakijiuliza kuwa mwisho wa hali hii ni nini hasa kama sio kulipeleka taifa sehemu mbaya?

Mmoja kati ya waandishi waandamizi wa gazeti moja la kila wiki ambaye sipendi nimtaje kwakuwa sijaomba ridhaa yake amesema haya, kuhusiana na hali hii “Silaha ya kupandikiza ubaguzi na chuki katika jamii ni silaha mbaya na ya maangamizi kwa jamii, tunayo mifano hai juu ya hilo”
Hakika maneno haya yanatakiwa kufanyiwa kazi kimamilifu

April 28, 2005 at 5:28 pm Leave a comment

Older Posts Newer Posts

Blog Stats

  • 35,058 hits
April 2005
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930