Archive for April 29, 2005

Amka mwanamke wa Kitanzania, Amka mwanamke wa Kiafrika

Amka mwanamke wa Kitanzania, amka mwanamke wa Kiafrika. Popote pale ulipo katika dunia hii, amka SAA YA UKOMBOZI NI SASA.Jitihada za mwanamke kutaka kujiondoa katika mfumo wa kukandamizwa kimawazo, kifikra, kimtizamo na kwa kila kitu ambacho amekuwa akidhania kuwa hakimstahili, hazijawahi kuwa na wakati mzuri kuliko sasa.

Harakati za kuhakikisha kuwa mwanamke kokote kule aliko duniani, anaendana na mazingira ya kisasa ya Utandawazi, Sayansi na Teknolojia, hususan katika eneo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) au (ICT) kama wanavyofupisha wenye lugha zao, zinatarajiwa kuchukua sura mpya hivi karibuni kufuatia mkutano mkubwa ambao utawakutanisha wanawake ambao wamekuwa wakitumia mfumo huo, kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Nauzungumzia mkutano ambao utawakutanisha wanawake ambao wamekuwa wakitumia teknolojia ya mtandao wa kompyuta katika kuwasiliana na kusambaza habari sehemu mbalimbali, mkutano ambao umepewa jina la BlogHer, ambao utafanyika nchini Marekani, mwezi Julai mwaka huu.

Mkutano huu pamoja na kuwa utakuwa fursa nzuri kwa wanawake kuweza kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazowakabili wao wakiwa kama wanawake, katika ulimwengu wa sasa, pia unatarajia kuwa mkombozi wa wanawake wengi duniani ambao hawatoweza kubahatika kuhudhuria wenyewe, ambapo jitihada kadhaa tayari zinafanywa kwa ajili ya mambo yatakayozungumzwa na kujadiliwa huko, kuchapwa katika lugha mbalimbali, kikiwemo Kiswahili.

Je wewe ni mwanamke wa Kitanzania au wa Kiafrika ambaye unadhani kuwa teknolojia imekuwa ikikutupa nyuma kila unavyojitahidi kufuatana nayo?, Ulikosea, hebu kaa mkao wa kusubiri kujua kuwa wanawake wenzako wana ushauri gani kwako wewe ambao utaweza kukufanya nawe uende sambamba kabisa na kasi ya teknolojia hii ya mawasiliano na habari kwa njia ya mtandao wa kompyuta.

Unaweza kusoma maelezo zaidi kuhusu mkutano huo kwa lugha ya kiingereza kwa kuingia hapa, au hapa. Na kwa wale wenye kupenda kufuatilia katika lugha ya Kiswahili au lugha zinginezo, mnaweza kubonyeza hapa kwa ajili ya kujua nini kitakuwa kikitokea wakati tukielekea mkutano huo.

Amka mwanamke wa Kitanzania, Amka mwanamke wa Kiafrika, saa ya ukombozi wako ni sasa

April 29, 2005 at 8:44 pm Leave a comment

Unayafahamu haya kumhusu Dk. Salim?

Kashfa, matusi, kuchafuliana majina na mengineyo mengi, ni miongoni mwa mambo ambayo yametawala, wakati huu Watanzania wakiwa wanasubiri kwa hamu kumjua ni nani atakayeteuliwa kwa ajili ya kuwania nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM. Miongoni mwa kashfa ambazo mmoja kati ya wagombea wa nafasi hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, alitupiwa ni pamoja na kuwa alihusika katika mauaji ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume.

Hata hivyo, kumekuwa na habari za kufurahisha kwake yeye baada ya mmoja kati ya wahusika wakuu katika kesi hiyo kumsafisha kupitia gazeti moja la kila siku nchini Tanzania. Unajua mhusika huyo kamsafisha vipi mgombea huyu? Soma hapa

April 29, 2005 at 7:14 pm Leave a comment

Uwazi wa Mkapa huu hapa

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Chama tawala nchini Tanzania, CCM, na pengine katika historia nzima ya Tanzania, uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM, kwa mwaka 2005, unatarajiwa kurushwa moja kwa moja toka katika ukumbi wa Chimwaga. Soma tamko la katibu mkuu wa CCM, Bw. Philip Mangula hapa

April 29, 2005 at 5:53 pm Leave a comment

Older Posts

Blog Stats

  • 35,058 hits
April 2005
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930