Archive for April 28, 2005

Nukuu maridhawa

Katika kipindi hiki ambapo tunauelekea uchaguzi mkuu, pilika pilika kibao zenye lengo la kuchafuliana majina hasa kwa wawania nafasi ya kuwa wagombea ‘Urahisi’ kwa tiketi ya CCM, zimekuwa zikipamba moto kila kukicha.

Inavyoelekea ni kuwa wamesahau kabisa wajibu wao kuwa ni kutushawishi sisi kuwa wamefanya mambo gani kwa ajili ya kustahili kuwa mashujaa wa taifa hili na badala yake wameelekeza juhudi zao katika kuchafuliana majina. Watanzania kadhaa wamekuwa wakijiuliza kuwa mwisho wa hali hii ni nini hasa kama sio kulipeleka taifa sehemu mbaya?

Mmoja kati ya waandishi waandamizi wa gazeti moja la kila wiki ambaye sipendi nimtaje kwakuwa sijaomba ridhaa yake amesema haya, kuhusiana na hali hii “Silaha ya kupandikiza ubaguzi na chuki katika jamii ni silaha mbaya na ya maangamizi kwa jamii, tunayo mifano hai juu ya hilo”
Hakika maneno haya yanatakiwa kufanyiwa kazi kimamilifu

April 28, 2005 at 5:28 pm Leave a comment

Hizi ndizo sheria zitazowahukumu wagombea CCM

Niandikapo makala haya, kumebakia takriban wiki moja tu kabla ya Watanzania kumjua mtu atakayesimama kuwania nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mtu ambaye pia wananchi wengi wamekuwa wakimtarajia kuwa ndiye atakayeingia katika lile jumba jeupe pale jijini Dar es salaam, baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Mgombea huyo ambaye atatoka kati ya walionunua (kuchukua?) fomu za kuwania kuteuliwa, ambao jumla yao walikuwa ni 11. Je unajua au pengine unakumbuka kuwa mgombea huyo, na uteuzi wote utakwenda kwa utaratibu upi? Hebu bonyeza hapa ujikumbushe kanuni za uteuzi huo

April 28, 2005 at 5:20 pm Leave a comment

Wabunge wetu wanapotudhalilisha

Unaweza kuiita vyovyote uwezavyo. Ni kashfa ya kwanza na ya aina yake kuwahi kuwakumba wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wale ambao ndio wamekuwa siku zote wakishiriki katika kujadili sheria mbalimbali za kuwabana ‘Wadanganyika’ ambao watabainika kuwa wametenda makosa mbalimbali kisheria. wale ambao tuliwapa dhamana na imani zetu zoooote wakatuwakilishe katika chombo hicho kikubwa cha kuunda sheria katika nchi yetu. Wale wale ambao, ilifikia wakati wakaamua kwa dhati kabisa kuhalalisha kuwa wao waitwe waheshimiwa.

Nawazungumzia wabunge watatu kutoka chama cha upinzani cha CUF, ambao waliamua kutumia madaraka yao kuudhalilisha umma wa ‘Wadanganyika’, kulidhalilisha Bunge letu tukufu na kuharibu kabisa imani na uaminifu waliojijengea Wadanganyika kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita, katika jumuiya za kimataifa.Mmoja kati ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano ulioanika hadharani maovu yao aliandika hivi: Bonyeza hapa usome na utoe maoni yako kuhusu waheshimiwa hawa.

April 28, 2005 at 5:11 pm Leave a comment

Older Posts

Blog Stats

  • 35,058 hits
April 2005
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930