Kwa wapinzani wangu katika soka

April 21, 2005 at 5:53 pm Leave a comment

Ni ukweli kwamba, kwa pengo ambalo lipo baina yetu sisi na wao, uwezekano wa kutwaa ubingwa kwa sasa ni suala ambalo ni ndoto zaidi. Kwa wale ambao ni mashabiki na wapenda kandanda kama mimi, naamini wanaelewa kuwa nazungumzia nini hapa, ila kwa wale ambao bado wanajiuliza, namaanisha Arsenal, ambayo katika wiki hili ilifanikiwa kutoka suluhu na vinara wa msimu huu katika ligi kuu ya soka Uingereza, Chelsea.

Kwamba tumeshindwa kuwazuia katika jitihada zao za kuelekea kutupokonya ubingwa, ni jambo la kusikitisha sana japo nawapongeza sana kwa mafanikio waliyoyapata katika msimu huu. Lakini kwamba wameshindwa kabisa kuvunja historia yao mbovu dhidi ya Arsenal, hakika hili ndilo jambo ambalo kwetu sisi mashabiki na wapenzi wa klabu hii, tunatakiwa kujivunia.

Ni wazi kabisa kuwa wanauchukua ubingwa safari hii, lakini kwamba wana historia ndefu sana hadi kuja kuweza kucheza mechi 49, bila kufungwa na kuvunja rekodi yetu ya msimu uliopita, hilo nalo ni jambo jingine linalonifurahisha zaidi, achilia mbali ukweli kuwa furaha yangu pia inatiwa chachu na ushindi wa wana-Msimbaazi palke jijini dar es salaam nikimaanisha Simba Sports Club, dhidi ya watani wao katika soka nchini Tanzania, na hawa ni wana-Jangwani ama Dar Young African Sports Club.

Hongereni na poleni wapinzani wangu katika ulimwengu wa soka

Entry filed under: maskani.

Tutampata kweli Mtakatifu? Kwa wapinzani wangu katika soka

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Blog Stats

  • 35,058 hits
April 2005
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930