Kichwa cha ajabu duniani

Unamjua mtu mwenye kumbukumbu za ajabu sana humu duniani? Mtu ambaye unaweza kumtajia tarehe fulani miaka kumi iliyopita na kisha baada ya sekunde tano akaanza kuielezea siku hiyo kuwa ilikuwa siku gani, ilianza vipi, alifanya nini na nini cha muhimu kilitokea siku hiyo?

 Wanasayansi nchini Marekani wameanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya uwezo wa kiakili/kumbukumbu wa raia mmoja wa nchi hiyo ambaye inasemekana kuwa ndiye binadamu mwenye uwezo wa ajabu wa kuwa na kumbukumbu kichwani mwake. Soma zaidi habari hii kwa kubonyeza hapa..

February 24, 2008 at 11:59 am 2 comments

Kilichomng’oa Lowasa madarakani

kwa marefu na mapana, naomba wasomaji wangu mpate fursa ya kupitia kitu kipya leo ambacho loicha ya kuwa si picha, lakini kimeleta picha mpya katika historia ya taifa la Tanzania. Namaanisha ripoti kuhusu kashfa ya Kampuni hewa ya kuzalisha Umeme iitwayo Richmond. Ripoti hiyo iliwasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katikati ya wiki linaloelekea ukingoni, na kusababisha kishindo kikubwa sana katika medani za siasa za Tanzania.
Najua si wote mliiona ripoti hiyo ilipokuwa ikiwasilishwa Bungeni, na si wote mliosikia, na pia si wote mmeweza kuipata. Sasa kwa wale ambao hawakubahatika kote huko, naomba muipitie kwa kubonyeza hapa.

February 9, 2008 at 10:54 am Leave a comment

KENYA: Mabadiliko hayabadiliki..

Mazungumzo ya kusaka muafaka baina ya pande zinazosababisha umwagaji damu nchini Kenya yamevunjika. Soma hapa au hapa kujua ilikuwaje.

 Nimekuwa nikifuatilia mambo yanayoendelea kwa jirani zangu hawa, kupitia njia mbalimbali zikiwemo za mawasiliano na vyombo vya habari. Katika kipindi hiki kigumu sana, miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana ni jamaa zangu waandikao mtandaoni ama Bloggers.

Mwana blogi Thinkersroom, ameandika makala kadhaa zenye kunivutia kuzisoma na bilashaka nawe msomaji wangu ungependa kuziona habari hizo. Bonyeza hapa kusikia kile anachosema huyu jamaa. na pia bonyeza hapa kusoma kile anachosema bloga mwingine, Kenyananalyst.  

 Lakini wakati hayo yanaendelea, rafiki yangu mmoja ambaye nitamtaja jina baadae kama akiniruhusu anasema mabadiliko ni lazima nchini Kenya… kwa maneno yake anasema kuwa Mabadiliko hayabadiliki

January 10, 2008 at 7:45 pm 1 comment

Una ushahidi wa yanayojiri Kenya?

Ni hulka ya binadamu, kujifunza kupitia makosa. na hili ndilo linalojitokeza nchi jirani na hapa kwetu TZ.

Wakati ambapo hakuna mtu ambaye alidhania kuwa yanayojiri nchini Kenya hivi sasa yangetokea, na wakati kila mtu akiwa anasikitika kutokana na hayo yanayoendelea huko, kwa upande wa pili, wanablogu wa nchini humo wameonyesha mchango wao mkubwa sana katika kuona hali inabadilika.

 Jitihada za mwanzo kabisa zilikuwa zile za kuhakikisha kuwa dunia inatambua kilicho, kinacho na hata kitakachotokea nchini mwao, kwa kutusambazia habari na matukio mbalimbali kwa kadiri walivyoweza. jitihada ya karibuni kabisa imekuwa ni kuanzishwa kwa zana inayoitwa Ushahidi.

Kwa sasa pengine sitokuwa na mengi sana kuihusu zana hii, maana nami niliipitia juu juu tu baada ya kupata taarifa hizi kupitia kwa kaka yangu Ndesanjo wa Jikomboe. ambaye naye aliipata kupitia kwa Mwafrika Mweupe….nitawaomba tu muitembelee na muone mambo yanayoendelea huko.

Na wakati mkifanya hivyo, ni vyema tukakumbushana umuhimu wa kuungana na kuzidi kuiombea heri nchi ya Kenya.

January 10, 2008 at 3:04 pm 1 comment

Kuna haja ya chaguzi katika nchi za Afrika?

Hili ndilo swali ambalo niliulizwa na mmoja kati ya watu niliobahatika kukutana nao na kuongea mawili matatu kuhusu kinachoendelea nchini Kenya. Na hakina hata mimi najiuliza kuna haja ya kuwa na chaguzi katika nchi zetu hizi?

Hali si shwari nchini Kenya. Hali si shwari kwa jirani zetu, hali si shwari kwa ndugu zetu, hali si shwari kwa kaka na dada zetu, …..pengine hili ndilo linaloweza kutamkwa kufuatia kinachoendelea nchini Kenya.

Pengine habari kuhusu uchaguzi wa nchini Kenya, wengi tulishazisikia toka wakati wa maandalizi na hata siku ile yenyewe ya uchaguzi. Lakini sidhani kama habari hizo zina umuhimu sana masikioni mwetu kwa sasa, kuliko zilivyo habari za matukio yatokanayo na uchaguzi huo.

Ni zaidi ya wiki sasa toka yalipotangazwa matokeo ya uchaguzi ule, na katika kipindi hiki ndugu na jirani za kenya waliokuwa wamejawa na matumaini makubwa baada ya uchaguzi, ni kama wamebakia na hakuna mikononi, mioyoni na hata katika nafsi zao. Ndio, wamebakia na hakuna.

Si tu kuwa yale matumaini waliyokuwa nayo yamefutika, bali yamefutika kwa njia isiyo ya kawaida. Njia ya kutisha, kuogofya na ambayo hakuna aliyekuwa akiiota kama ingetokea katika nchi ya Kenya, baada ya jitihada kubwa sana za taifa hilo kuwa msuluhishi wa mgogoro wa Dafur.

Damu za watoto wetu wasio na hatia zimemwagiga, wengine wamebanikwa na kuteketea kwa moto kama inavyochomwa mishikaki, wengine wengi wameachwa na majeraha na vilema vya maisha. Watu wazima wameuawa, wamechomwa moto, wameumizwa vibaya na na kuachiwa machungu makubwa katika vipindi vilivyosalia vya maisha yao.

Damu ya mtu kwa ajili ya kuingia Ikulu? Kibaki na Odinga, mnahitaji damu za watu kwa ajili ya kuingia Ikulu? Hapana. Sitaki kuamini. Natamani iwe tamthilia tu, ambayo haina ukweli. Mtu aliyekuwa shujaa wa taifa katika muda wa zaidi kidogo ya miaka mitano iliyopita, hivi sasa amekuwa chanzo cha mauaji ya watu waliomuamini.

Miaka zaidi ya mitano iliyopita, alipoingia madarakani kwa kura halali – ofcourse kupitia ule ule utamaduni wa unafiki wa kisiasa uliowatawala viongozi wetu wengi wa Afrika. Kibaki alibeba dhamana kubwa sana ya kulipeleka taifa la Kenya katika nchi ya ahadi. Lakini leo hii baada ya unafiki wake kudhihirika, kwamba hakuwa amemaanisha yale aliyoahidi wakati ule, lakini akiwa bado anazitamani raha za Ikulu, ameona njia bora ya kuparejea ni kwa kusababisha vifo na umwagaji damu zisizo hatia?

Nachelea kusema kuwa kilichotokea Kenya ni wizi wa kura, kwani huo si wizi wa kura, bali ubakaji wa demokrasia na ubakaji wa maisha na haki ya msingi ya kuishi ya Wakenya.

Natamani niseme mengi sana kwakweli, lakini midhali wapo wengi ambao wanaendelea kusema kuhusu hali inavyoendelea huko, naomba nijiweke katika kundi lile la wanaokesha na kutumia muda wao mwingi kuwaombea mamilioni ya Wakenya wasio na hatia ambao wako katika hatari ya kupoteza maisha yao kutokana na tamaa za madaraka za genge la watu wachache waliowaamini na kuwaheshimu.

Jambo pekee ninaloweza kusema kwa kuhitimisha mistari yangu hii michache ni kuwaeleza ndugu, rafiki, dada, kaka, wadogo, baba, mama, babu na bibi zetu mlioko Kenya kwamba, tuko pamoja nanyi katika kipin di hiki kigumu.

Hamkutenda dhambi kubwa kwa kutumia akili zenu kufanya kile mnachoona ni bora katika nchi yenu, kiasi kwamba Mungu awaadhibu kwa njia hiyo. Naamini upande wa haki utashinda na ule wa dhuluma utaadhibiwa.

Mungu ibariki Afrika ……….Mungu ibariki Kenya
Mungu inusuru Kenya…….Mungu wanusuru wasio na hatia.

January 5, 2008 at 12:57 pm 1 comment

HERI YA MWAKA MPYA

Niliandika awali, siku chache sana kabla mie na wewe unayesoma hapa hatujauona, lakini midhali hivi sasa naamini tumeuona… si vibaya tukitakiana Heri ya Mwaka mpya wa 2008. Tumshukuru Mungu kwa wema aliotutende mwaka wa 2007, na kumuomba atujaze nguvu na kututia moyo kwa kila tunalofikiria kulitenda katika mwaka huu wa 2008

 HERI YA MWAKA MPYA….HAPPY NEW YEAR 2008

January 1, 2008 at 1:56 am 1 comment

heri ya mwaka mpya wana Jukwaa la Uchambuzi wote

salaam

December 30, 2007 at 6:34 pm 1 comment

Older Posts


Blog Stats

  • 34,787 hits
April 2020
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930